1jz GTE ni injini yenye nguvu sana

1jz GTE ni injini yenye nguvu sana

Hiyo mashine yako ilikuwa ni ya kawaida sana, km ulishawahi kuendesha 1jzgte au 2jzgte iliyofanyiwa mapping ndio ungenielewa zaidi, dragging race ya mwisho iliyofanyika Kenya gari za Tanzania zilizofungwa injini za 2jz gte ndio zilizokuwa zinapeform vizuri haijalishi imefungwa kwenye toyota alteza au supra lakini ilikuwa ni balaa wakenya na subaru zao walikuwa wanaipata fresh

Sent using Jamii Forums mobile app

Subaru hakuna kitu mkuu. Tunaviona mtaani vimefungwa mabuyu nyuma, vinapiga Kelele tu
 
Watu wengi bongo hapa ukiwaambia Crown Athlete wamezoea zile za 4Gr na 3Gr au zile za 2500cc na 3000cc ambazo ndio zimejazana kwenye ma yard humo.

Hii ninayo izungumzia hapa ni kinu cha 3500 cc, Gari ambazo watu wachache sana wanazo bongo hapa, maana ni gari ambazo kuzikuta yard ni Nadra sana.

Naombeni muitafute Crown Athlete GRS-184 muitest uwezo wake. Halafu mje mthibitishe hapa
 
Watu wengi bongo hapa ukiwaambia Crown Athlete wamezoea zile za 4Gr na 3Gr au zile za 2500cc na 3000cc ambazo ndio zimejazana kwenye ma yard humo.
Hii ninayo izungumzia hapa ni kinu cha 3500 cc,
Naombeni muitafute Crown Athlete GRS-184 muitest uwezo wake. Halafu mje mthibitishe hapa
kumbe zimefungwa katika gari za Crown Athlete basi nimeelewa
na kweli hizi saloon ni chache sana ila cc inatisha kwani inakaribia Land Cruiser
na kwenye mashindano (Racing, skidding) naona hazihusiki
labda barabarani Mwanza Mtwara
Je ulaji wa mafuta si itbwiya?
 
Watu wengi bongo hapa ukiwaambia Crown Athlete wamezoea zile za 4Gr na 3Gr au zile za 2500cc na 3000cc ambazo ndio zimejazana kwenye ma yard humo.

Hii ninayo izungumzia hapa ni kinu cha 3500 cc, Gari ambazo watu wachache sana wanazo bongo hapa, maana ni gari ambazo kuzikuta yard ni Nadra sana.

Naombeni muitafute Crown Athlete GRS-184 muitest uwezo wake. Halafu mje mthibitishe hapa
Wewe unaizungumzia Crown majesta sio crown athlete

Sent using Iphone 7s
 
Wewe unaizungumzia Crown majesta sio crown athlete

Sent using Iphone 7s

Mkuu ndio maana nasema watu wengi hawazijui hizi gari. Wengi wamezoea kuziona Crown Athlete kwenye Car Yard za bongo hapa ambazo ni Crown Athelete za kawaida kabisa ambazo nyingi ni GRS-180 and GRS-182 zenye Engines za 4GR na 3GR. ambazo zina uwezo mdogo ukilinganisha tu na hata 1JZ-GTE.

Wafanya biashara wengi wa magari hapa bongo wanaogopa kuziweka hizi kwa kuhofia kukosa wateja, na hii ni kwa sababu wabongo wengi hawapendi gari zenye CC kubwa. Ndio maana Crown Athelete GRS-184 yenye engine ya 2GR ni ngumu sana kuiona mtaani na wengi ambao wanazo hizi unakuta wameagiza wenyewe direct from Japan.

Angalia hii link hapa chini halafu thibitisha hiki ninachokiongea mkuu. Hizi ndizo wengi hapa bongo hawazifahamu

BE FORWARD : 2005 TOYOTA Crown

Wengi hapa bongo wanazijuwa hizi hapa kwenye hii link inayofuata hapa, ambazo ndio zipo kwenye Yard za hapa bongo
BE FORWARD : 2004 TOYOTA Crown
 
Ninayo hiyo 1jz ge ktk mark 2, nafikiria kuitoa na kufunga 1g kavu, je inawezekana Na nitapata kwa sh ngapi pale shaurimoyo.Kwani tayari mipango ya kuitumia imeshakwisha , ilikuwa kwa ajili ya safari ndefu Na sasa nataka kwa ajili ya mizunguko ya mjini
 
Zilitengenezwa na kampuni ya Subaru. Toyota sports karibu zote ni Subaru ila body Toyota

Sent using Jamii Forums mobile app
Nadhani uko sahihi kwa kiasi fulani.
Screenshot_20190829-103625.jpeg
 
Back
Top Bottom