kuna rafiki yangu mmoja nilipomueleza kuhusu ishu hii akasema hizo statistics mbona siyo ajabu!, jamaa anadai anakumbuka enzi hizo anasoma skuli, vyoo vyao vilikuwa haviendeki, ukiingia chooni lazima uvue shati otherwise ukitoka tu shati lote linanuka kinyesi,jamaa akadai kulikuwa kuna kichaka near by huko ndo wanafunzi walipokuwa wanashusha haja zao, jamaa anadai tena sometimes mnakutana wengi na stori mnapiga kama kawaida huku mkishusha mambo
Mwulize jamaa yeyote aliyesoma Rungwe secondary school miaka ya 80.
Ulikuwa unaweza kwenda kulia msosi chooni na wala hata usipate taabu. Shule nzima ilikuwa safi, ilikuwa wajibu wa kila mwanafunzi kuhakikisha shule yote ni safi. Kulikuwa na mwalimu tulikuwa tunamwita Hitler, alitufundisha wote nini maana ya usafi. Ingawaje tulimlaumu sana wakati ule, lakini somo lake linaendelea kutusaidia wengine mpaka leo.
Nikaingia baadaye mlimani, vyoo vichafu, afadhali kwenda kichakani. Kama wanafunzi wa secondary wamefanikiwa kutengeneza mazingira yao kwanini wasomi wa mlimani washindwe?
Pale hakukuwa na ubunifu wowote, tulikuwa tunasubiri wasafisha vyoo mpaka waje hata kama ni baada ya siku nne. Watu kama nane tulikuwa tunashindwa kusafisha na kutengeneza mazingira ya choo chetu kimoja. Hapo kweli tulikuwa na haki ya kuilaumu serikali?
Ukipita wizara mbalimbali TZ, hali ya vyoo inatisha, why? Ukishindwa ku manage choo, utaweza ku manage mambo yote ya wizara?