20 Kali za Judith Mbibo Lameck Wambura

Chanzo hasa cha kutoelewana na marehemu Ruge ilikuwa Nini? Au alimtaka akakataa??
Na pia kipindi hiko Jidee alikuwa mke wa mtu pia
Alimkosea sana, huwez kutongoza mke wa mtu ilihali mumewe unamfahamu
 
Mamaaa mama nimeshakuoa, kama chakulaaa nimeshanunua,. TID huyo na Jide😍
"...mke wangu tulia nyumbani, acha wewe kisirani, kurudi leo nitawahi..."

Moja ya ngoma kali kabisa, "Understanding"
 
Ila kinachonishangaza kwanini baada ya kufariki Ruge ameamua kuukacha muziki,,,au alikuwa anafanya ili Kumkomoa Marehemu Ruge???
Nadhani pia muziki wa hisia ndo unaodumu!

Ama utunge ukiwa na huzuni sana, furaha sana, hasira sana, masikitiko, malalamiko, umezama sana penzini, n.k

Kero zote alizopitiwa, zilimfanya atoe ngoma kali, ashukuriwe Gadner kwa kumsababishia vyote hivyo na hivyo kutoa ngoma kali hata za kushirikishwa.

Zaidi ni wakati, zama! Atabaki kuwa msanii bora wa kike kuwahi kutokea kwenye Bongo fleva, na hakuna aliyefikia nusu yake mpaka sasa!
 
Chanzo hasa cha kutoelewana na marehemu Ruge ilikuwa Nini? Au alimtaka akakataa??
Biashara na control, Ruge hakuwa na masihara kwenye biashara wakati utamaduni uliokuwa umezoeleka ni wa 'kusaidiana kishkaji'. He was a through and through capitalist sasa ukizingatia huyu ambaye walikuwa wakivuana chupi kimbana mbavu kibiashara hakuona kama ni sawa, in short kulikuwa na changanyiko wa vitu vingi na Ruge ilikuwa mkikosana anakubania kila kona ili urudi kwake ukubaliane na terms and conditions zake lakini sasa strong personality ganja lady Jide naye ana principles zake kwa hivyo ikageuka kuwa clash of egos ambapo unajua kupatikana mshindi inakuwa ngumu(kwao haikuwezekana).
 
Na pia kipindi hiko Jidee alikuwa mke wa mtu pia
Alimkosea sana, huwez kutongoza mke wa mtu ilihali mumewe unamfahamu
Jide na Ruge walikuwa na uhusiano kitambo sana kabla hajawa mke wa 'mtu', wakati ndiyo anaanza career yaani kabla hajawa hata na nyimbo za kutunga mwenyewe time bado ainaimba nyimbo za kukopi za nje ile walivyokuwa wakipiga simu redioni(live) kuonyesha talents zao ndipo yeye akaitwa na akawa Clauds family member. Gardner amemuoa Jide wakati imeshapita miaka kibao toka ameachana na Ruge.
 
I wish nije kufanya nae collab kabla hajastaafu muziki
Inawezekana
 
"Usiusemee Moyo" ni wimbo wake ninaoupenda kupita maelezo. Mwenyezi Aendelee Kumfanikisha.
 
Nyakati. Kwani Usher Raymond wa leo ndio yule wa 2005!?
 
Sawa tumekuelewa ila shabiki namba moja wa JIDE ni mimi.
 
"Usiusemee Moyo" ni wimbo wake ninaoupenda kupita maelezo. Mwenyezi Aendelee Kumfanikisha.
Usijigambee ye akupenda
Hujui akitoka ni nini afanyalo kwakoo
We wampenda
Katu usiusemee moyo wa mwezi wako wooouoo
 
Msikilizaji wa JF
Kula chuma hichooo


Ngoma za mwisho mwisho kabla hajapotea
Your browser is not able to play this audio.
 
Adui yako ndo chachu ya maendeleo yako.....baada ya ruge kuondoka
C dhan kama kuliakua na adui yake mwingine
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…