20 Kali za Judith Mbibo Lameck Wambura

20 Kali za Judith Mbibo Lameck Wambura

Chanzo hasa cha kutoelewana na marehemu Ruge ilikuwa Nini? Au alimtaka akakataa??
Na pia kipindi hiko Jidee alikuwa mke wa mtu pia
Alimkosea sana, huwez kutongoza mke wa mtu ilihali mumewe unamfahamu
 
Mamaaa mama nimeshakuoa, kama chakulaaa nimeshanunua,. TID huyo na Jide😍
"...mke wangu tulia nyumbani, acha wewe kisirani, kurudi leo nitawahi..."

Moja ya ngoma kali kabisa, "Understanding"
 
Ila kinachonishangaza kwanini baada ya kufariki Ruge ameamua kuukacha muziki,,,au alikuwa anafanya ili Kumkomoa Marehemu Ruge???
Nadhani pia muziki wa hisia ndo unaodumu!

Ama utunge ukiwa na huzuni sana, furaha sana, hasira sana, masikitiko, malalamiko, umezama sana penzini, n.k

Kero zote alizopitiwa, zilimfanya atoe ngoma kali, ashukuriwe Gadner kwa kumsababishia vyote hivyo na hivyo kutoa ngoma kali hata za kushirikishwa.

Zaidi ni wakati, zama! Atabaki kuwa msanii bora wa kike kuwahi kutokea kwenye Bongo fleva, na hakuna aliyefikia nusu yake mpaka sasa!
 
Chanzo hasa cha kutoelewana na marehemu Ruge ilikuwa Nini? Au alimtaka akakataa??
Biashara na control, Ruge hakuwa na masihara kwenye biashara wakati utamaduni uliokuwa umezoeleka ni wa 'kusaidiana kishkaji'. He was a through and through capitalist sasa ukizingatia huyu ambaye walikuwa wakivuana chupi kimbana mbavu kibiashara hakuona kama ni sawa, in short kulikuwa na changanyiko wa vitu vingi na Ruge ilikuwa mkikosana anakubania kila kona ili urudi kwake ukubaliane na terms and conditions zake lakini sasa strong personality ganja lady Jide naye ana principles zake kwa hivyo ikageuka kuwa clash of egos ambapo unajua kupatikana mshindi inakuwa ngumu(kwao haikuwezekana).
 
Na pia kipindi hiko Jidee alikuwa mke wa mtu pia
Alimkosea sana, huwez kutongoza mke wa mtu ilihali mumewe unamfahamu
Jide na Ruge walikuwa na uhusiano kitambo sana kabla hajawa mke wa 'mtu', wakati ndiyo anaanza career yaani kabla hajawa hata na nyimbo za kutunga mwenyewe time bado ainaimba nyimbo za kukopi za nje ile walivyokuwa wakipiga simu redioni(live) kuonyesha talents zao ndipo yeye akaitwa na akawa Clauds family member. Gardner amemuoa Jide wakati imeshapita miaka kibao toka ameachana na Ruge.
 
I wish nije kufanya nae collab kabla hajastaafu muziki
Inawezekana
 
"Usiusemee Moyo" ni wimbo wake ninaoupenda kupita maelezo. Mwenyezi Aendelee Kumfanikisha.
 
Ni zaidi ya hayo, ukumbuke wakati anaanza career yake walikuwa wanatiana(pika pakua) hivyo ujue beef lao lilikuwa na mchanganyiko wa mambo mengi. Bila hilo beef muziki wa Jide kwa hali ilivyo sasa soko linaugumu sana kwake pamoja na kipaji kikubwa alichonacho.
Nyakati. Kwani Usher Raymond wa leo ndio yule wa 2005!?
 
20 KALI ZA JUDITH MBIBO LAMECK WAMBURA
LADY JAY DEE, KOMANDO, MAMA SOME FOOD, JIDE, ANACONDA
THE BONGO FLAVOUR FIRST LADY

1. Amechanganya damu kutoka mikoa miwili; Shinyanga na Mara, wilayani Bunda. Na ni dada wa mwanamuziki mwingine aitwaye DABO MTANZANIA.

2. Alianza kama rapa, akageukia utangazaji wa redio, lakini alijitafuta zaidi na kuona anatosha kuwa MWIMBAJI.

3. Ni msabato na kama walivyo wasanii wengi, alianzia kuimba kanisani na hivi karibuni kuna video moja imetembea mtandaoni ikimwonesha akiwa kanisani anaimba na kwaya.

4. TOFAUTI na ilivyokuwa imekaririwa kuwa ili uwe MSANII mkali, lazima uingie Bongo Records na kurekodiwa na P FUNK. Jide, alikuwa kwenye mikono ya Master Jay na ameingia Bongo Recs kufanya chorus ya KADI NA UA ROSE ya Fid Q, NIMEAMINI ya Prof Jay na kufanya "chorus ya mtoto wa P" ajiitaye Rapcha kwenye ngoma iitwayo AMEN. Kwenye hili anaungana na MR BLUE, MR NICE, na SAIDA KALORI, wasanii waliotamba kwa NYAKATI TOFAUTI kwa kipindi kile na kuishika Bongo bila MIDUNDO ya BAMAGA.

5. Jide ni miongoni mwa wasanii wa awali kumiliki studio yake mwenyewe iliyoitwa JAG RECORDS huku mipini ya hapo ikisukwa na mtaalam HERBALIST.
LAWAMA - CHID BENZ FT MATONYA
NISHIKE MKONO - K LYNN FT BLUE
Ni miongoni mwa ngoma zilizosukwa na HERBALIST lakini pia ngoma kadhaa za Ismail wa WASHKAJI au SOUL n FAITH.

6. Alikiri mara kadhaa kuwa asingekuwa mwanamuziki, angekuwa mtu wa mapishi. Kuthibitisha hili akafungua NYUMBANI LOUNGE, AMBAYO Pengine imekuja KUZALISHA mawazo mapya kama SHISHI FOOD.

7. Amewahi kumiliki kiwanda cha maji ya kunywa lakini kikapigwa pini kabla ya uzinduzi rasmi. Na hii ilikuwa way back before TANZANIA YA VIWANDA au GARI LA MASOUD KIPANYA. JIDE IS ALWAYS AHEAD OF TIME.

8. Jide amewahi kuwa na kipindi kinachoangazia maisha yake ya kila siku, JIDE REALITY SHOW, hapa akaungana na CHID BENZ na WEMA SEPETU, ambao wamewahi kufanya vipindi vyao pia kwa NYAKATI TOFAUTI.

9. Jide ni mmiliki wa tuzo za Kili, tuzo TOFAUTI za Afrika Mashariki ikiwemo KISIMA lakini pia ukienda bondeni, Kuna jina lake kwenye zilizokuwa tuzo kubwa sana kwa kipindi kile, KORA AWARDS.

10. Jide anamiliki Kolabo nzito na majina makubwa kwenye muziki;
Muziki ft Samba Mapangala
I am ft Oliva Mtukudzi
Sirimba - Ngoni
Kiboko yao - ft Chameleone
Nimpate wapi - Longombaz
Kwa Bongo hapa, wasanii wote wakubwa wamefanya kazi na Jide, ukimtoa AFANDE SELE, SOLO, MOE na DIAMOND.

11. Jide amesafiri mara kadhaa kwenda nchi tofauti kujifunza lugha za mataifa mengine ikiwemo Kifaransa.

12. Anamiliki albums nyingi lakini album ninayoipenda kuliko zote ni SHUKRANI. Album AMBAYO alisema aliitoa kwa ajili ya kuwashukuru MASHABIKI zake, ambao mimi ni miongoni mwao. Hapa anaungana na Sugu, Mr Ebbo, na Wakazi ambaye yeye, ametoa zaidi mixtapes.

13. Ni miongoni mwa wasanii wa awali kabisa kumiliki bendi, MACHOZI BAND, ambayo ilikuwa inafanya shows zake palepale kwake Nyumbani lounge, hivyo, nyimbo za Jide zikampa hela na kuimbwa live na bendi yake lakini pia akapata pesa kwa kuuza msosi palepale kwake.

14. Ni miongoni mwa wasanii wengi walioingia kwenye mtafaruku mzito na 'klaudzi' mpaka bosi wao akatangaza kuwa siku ile iliyokuwa climax ya ugomvi wao USIPIGWE WIMBO WOWOTE WA BONGO FLEVA. HAPO NIKAAMINI JIDE IS BIGGER THAN BONGO FLEVA. IF IT IS SAFE, I MAY SAY, JIDE IS THE BONGO FLEVA ITSELF.

WAKATI "WANAUME" WALIPIGISHWA MAGOTI, JIDE HAKUSANDA NA BADO YUKO PALE WAKATI ILIAMINIKA UKIGOMBANA NA JAMAA UNAPOTEA MAZIMA.

15. Amekuwa akiandaa maonesho yake mwenyewe na kutomlalamikia mtu kwa kutomwita kwenye maonesho yao. Viingilio huwa ni 20,000 mpaka 100k na bado watu wanaingia.

16. Wakati inaaminika wanawake hawapendani kwenye muziki, Jide ameshafanya Kolabo na Ray C, Mwasiti, Karen, Atemi, lakini pia amewaalika watoto wa kike kibao kwenye shows zake na amewahi kufanya joint show na ZAHRA aliyetamba na kibao chake cha DESTINY.

17. Zililetwa COPIES nyingi kwenye game na zikaonekana kufunika original versions. Nani hakumbuki kuwa BARNABA ni carbon copy ya BUIBUI,
nani hajui kuwa Z ANTO aliletwa kumpoteza MB DOGGY, umewasikiliza vizuri VUMILIA na MWASITI, achana na Hawa akina ZILLA na BILNASS au RUBY na NANDY. Hebu niambie nani amewahi kumbite JIDE na akatoka salama?? Huamini, rudi kaisikilize ZAMANI ya Q CHIEF ft JIDE halafu sikiliza ZAMANI RMX ya BARNABA, LINAH na Q CHILA, uone namna LINAH SANGA alivyoelea kwenye vesi ya JIDE.

18. Jide amefanya mitindo yote kuanzia rap, RnB, Zouk, Mduara, Reggae, Dansi, Qaito mpaka Afro pop.

19. Jide amefanya official covers kali na nyingine zimekuwa kali kuliko hata original versions
Siwema - Marijani Rajab
Muhogo wa jang'ombe - Bi Kidude
Nimekusamehe - Hamza Kalala
Na nyinginezo.

20. Amesimangwa na magazeti na waja wengi kuwa hazai lakini amekuwa akitumia msemo wa SUGU kwenye HAYAKUWA MAPENZI, "WANGAPI WAMEZAA WATOTO NA BADO WAKAWA MATEJA"

KUNA MUDA NAJIONA KAMA MTOTO WA JIDE HIVI NA SIYO KAMA MTOTO WAKE ILA KAMA FIRST BORN WAKE KABISA, HIVYO MSISEME TENA KUWA HANA MTOTO.

MIMI NI SHABIKI NAMBA MOJA WA JIDE, HATA AKIACHA KUIMBA.

MADA GANI HAJAIIMBIA, ALBUM GANI ILIFLOP? WIMBO GANI KAIMBA CHINI YA KIWANGO??

Nimemwona mara mbili tu katika maisha yangu, mara ya kwanza alikuwa kwenye gari yake maeneo ya CCBRT na mara ya pili nimemwona akiwa na GARDNER G HABASH pande za MLIMANI CITY walipoenda kufanya shopping kwa ajili ya show kipindi kile Cha JOTO HASIRA.

UKINIULIZA MTU MMOJA AMBAYE NINATAMANI KUONANA NAYE NA KUPATA WALAU DAKIKA KUMI TU ZA KUONGEA NAYE, DUNIA NZIMA, MY ANSWER IS LADY JAY DEE, THE TRUE AND ONLY DEFINITE DEFINITION OF BONGO FLEVA.

JIDE, I LOVE YOU, MOM!!!

HILI SIYO ANDIKO KAMA MENGINE, HII NI BARUA YANGU YA WAZI KWA JUDITH.

MUZIKI WAKE UMENILEA, ITIKADI ZAKE ZIMENIKOMAZA NA FALSAFA ZAKE ZIMENIFIKISHA NILIPO.

SISUBIRI MPAKA AFE NIKUBALI SHE IS THE BEST.

MWANDISHI WA AINA YAKE.
LUAH.
Sawa tumekuelewa ila shabiki namba moja wa JIDE ni mimi.
 
"Usiusemee Moyo" ni wimbo wake ninaoupenda kupita maelezo. Mwenyezi Aendelee Kumfanikisha.
Usijigambee ye akupenda
Hujui akitoka ni nini afanyalo kwakoo
We wampenda
Katu usiusemee moyo wa mwezi wako wooouoo
 
Msikilizaji wa JF
Kula chuma hichooo


Ngoma za mwisho mwisho kabla hajapotea
 
Jide pia aliwahi tongozwa na Chid Benz, na kupelekea kukerekwa na kitendo kile alichofanya Benzino,,, na akaenda mbali akamuanika kwa mapaparazi,,, pia akafuta ile verce ya ule wimbo wa UKO JUU na akaacha kufanya kazi na Chid Benz,,,, akawa anafanya na Mr Blue na wakatoa wimbo unaitwa NALIA NA MOYO.

Ila kinachonishangaza kwanini baada ya kufariki Ruge ameamua kuukacha muziki,,,au alikuwa anafanya ili Kumkomoa Marehemu Ruge???
Adui yako ndo chachu ya maendeleo yako.....baada ya ruge kuondoka
C dhan kama kuliakua na adui yake mwingine
 
Back
Top Bottom