2010 BMW 320i vs Mercedes Benz C Class

2010 BMW 320i vs Mercedes Benz C Class

Najua, nilichomaanisha ni kwamba kununua Bimmer au Mercedes ambayo karibia kila kitu kimeshachoka itakuchukuwa gharama kubwa sana mpaka kuja kuiweka sawa na kuenjoy Bimmer ambapo hiyo gharama ni bora utafute gari za kawaida ( ambazo hazing majina) lkn mpya kidogo ambapo utaitumia kwa muda mrefu zaidi, kununua Mercedes au Bimmer iliyokwishachoka ni kupoteza hela na siyo clever kwani aidha utaipaki kwa kushindwa kuirepair au itakubidi utafute gari nyingine ya pembeni kama toyota ya kutumia kila siku, sasa ukijumlisha hizo stress zote ni bora ujinyime ununue gari ( siyo brand name lkn nzuri) ya miaka max 5 lkn utaishi nayo bila ya stress, …
Mkuu sidhani kama gari ya 2010 inakuwa imechoka kihivo kwa mazingira yetu ya ‘Kibongobongo’!. Kuna watu kibao naona wanenunua Mercedes w203 (za mwaka 2006 kushuka chini) na bado wanavimba na kutimua vumbi road. Hata BMW nyingi zinazoingia nchini kwa sasa ni za mwaka 2005-2006
 
Mkuu sidhani kama gari ya 2010 inakuwa imechoka kihivo kwa mazingira ya kibongo! Kuna watu kibao naona wanenunua Mercedes w203 (za mwaka 2006 kushuka chini) na bado wanavimba na kutimua vumbi road. Hata BMW nyingi zinazoingia nchini kwa sasa ni za mwaka 2005-2006

Inawezekana uko sahihi, mimi nimeongelea tu experience yangu najua wengi wenye VW Touareg ( model ya kwanza 2002-2010), Audis, BMWs na Mercedes wengi wao aidha hununua gari nyingine haswa toyota ya kutumia kila siku au zimepaki gereji kwa fundi au kama zinatumika zimeshachokonolewa na mafundi na kuunganishwa kufanyiwa modification za kila namna na ile original flavor ya kwamba unaendesha Bimmer haipo tena, nilichotaka kusema ni kwamba hizo gari ziko bomba lkn utaweza kuzienjoy kama kila kitu kinafanya kazi orignal form ( ofcourse hii ni pia kwa kila aina ya gari) na hilo linawezekana kama ukiipata/ ukimudu kuinunua mpya au karibu na mpya au kama ni zamani labda uinunue kwa mtu unayemjua ambaye aliinunua mpya na kuitunza kwa service na kuifanyia matengenezo kuweka spares mpya original jambo ambalo pia bongo ni nadra sana, ….
 
Chukua Benz..
C200 Kompressor imekuwa ikitumia 4 cylinders muda mrefu.. Engine itakuwa reliable..
320i ilikuwa ni 6 cylinders then wakahamia kwenye 4 cylinders.. New technology.. Engine ya majaribio.. Probability ya kuwa na matatizo ni kubwa..!
Kama unatafuta Bimmer achana kabisa na 4 cylinders.. Angalia za 6 cylinders.. Ziwe na cc angalau 2500..!
4 cylinders ni kama unataka logo ya BMW ila kwa pleasure tafuta 6 au 8 3000cc kwenda juu..!
BMW 328 itamfaa? Au nayo magumashi?
 
BMW 328 itamfaa? Au nayo magumashi?
Kwa mwaka 2010 BMW ya kuchukua ni 323i au 335i(kama ana pesa ya wese na anataka kunyanyasa watu barabarani).

The rest atakuja kulalamikia watu humu ndani.

323i ya 2010 ina Cc2500 ikiwa na engine ya N52B25 wakati 335i ya 2010 ina Cc3000 N55 with twin scroll turbo...

The rest ndio zina engine kama N43, N45, N53, N54 ambazo zote ni engine za majaribio na zilifeli...
 
Bro number’s don’t lie

Go for Mercie

Good Fuel economy,performance ni ya kawaida kiukweli japo ina top 260km/hr labda usichukue hizi cc1780

Comfotability inategemea una compare na gari ipi lkn haiifiki kwa gari kama crown.

All in all you buy mercides you buy pride
Kila utapoonekana wanajua una pesa[emoji28]

Maintenance ni expensive kiasi


Hizi C200 kompressor hazina magonjwa mengi ndo maana hutasikia kelele humu za wamiliki wa Benz


Ni gari reliable sana na ngumu mno.umeme kiasi

ONYO:kama hukai mjini kene barabara na mafundi wa uhakika achana nayo mkuu
Honest opinion.
 
Hiyo nzuri.. Uhakika
328i kwa e90 ni kichomi. Ina N53 ambayo ni kama N43 iliyoongezwa cylinders mbili.

Nox sensor, Injector nozzle, coils packs, HPFP, Timing chain, Oil pressure relief valve, na mengine mengi. Hayo yote yakisumbua kwa pamoja lazima ufe kwa stroke.

Hayo matatizo yote yanatokea frequently.
 
Sio Siri BMW 320i zipo nyingi Sana sikuhizi Hata Mimi unanipa mzuka Sana wa kujaribu kuinunua ...
Jamaa yangu kariakoo ameuza Toyota crown na amenunua BMW 320 huwa anaisifia Sana gari yake dhidi ya crown 👑 hata Mimi nakushauri nunua fasta hiyo BMW.
Baada ya miaka 5 mbele wengi tutaingia Tu Kwa mjerumani
Mjerumani hana urafiki na maskini.
 
328i kwa e90 ni kichomi. Ina N53 ambayo ni kama N43 iliyoongezwa cylinders mbili.

Nox sensor, Injector nozzle, coils packs, HPFP, Timing chain, Oil pressure relief valve, na mengine mengi. Hayo yote yakisumbua kwa pamoja lazima ufe kwa stroke.

Hayo matatizo yote yanatokea frequently.
Ahhh kumbe.. Nilijua ni N52B30..!
Then bora 330i..!
 
328i kwa e90 ni kichomi. Ina N53 ambayo ni kama N43 iliyoongezwa cylinders mbili.

Nox sensor, Injector nozzle, coils packs, HPFP, Timing chain, Oil pressure relief valve, na mengine mengi. Hayo yote yakisumbua kwa pamoja lazima ufe kwa stroke.

Hayo matatizo yote yanatokea frequently.
Engines bora za BMW zinaanzia B58 kwenda mbele.

Hizi za nyuma ilikuwa ni hit n miss.

Kama hela ipo, chukua BMW yenye engines za B58 au S58.
 
Ni kweli crown ni ndege ya chini,hakuna benzi wala bmw inaifikia kwa comfotability,ukimpa lift mtu hasa hawa dada zetu huwa hawataki kushuka
Wewe jamaa upo serious? Unavyosema hakuna Benz wala BMW umeunganisha na S Class na 7 series humo ndani sio? Hebu kuwa serious usianze kufananisha wajerumani na crown ndg
 
Back
Top Bottom