2010 BMW 320i vs Mercedes Benz C Class

Mkuu sidhani kama gari ya 2010 inakuwa imechoka kihivo kwa mazingira yetu ya ‘Kibongobongo’!. Kuna watu kibao naona wanenunua Mercedes w203 (za mwaka 2006 kushuka chini) na bado wanavimba na kutimua vumbi road. Hata BMW nyingi zinazoingia nchini kwa sasa ni za mwaka 2005-2006
 

Inawezekana uko sahihi, mimi nimeongelea tu experience yangu najua wengi wenye VW Touareg ( model ya kwanza 2002-2010), Audis, BMWs na Mercedes wengi wao aidha hununua gari nyingine haswa toyota ya kutumia kila siku au zimepaki gereji kwa fundi au kama zinatumika zimeshachokonolewa na mafundi na kuunganishwa kufanyiwa modification za kila namna na ile original flavor ya kwamba unaendesha Bimmer haipo tena, nilichotaka kusema ni kwamba hizo gari ziko bomba lkn utaweza kuzienjoy kama kila kitu kinafanya kazi orignal form ( ofcourse hii ni pia kwa kila aina ya gari) na hilo linawezekana kama ukiipata/ ukimudu kuinunua mpya au karibu na mpya au kama ni zamani labda uinunue kwa mtu unayemjua ambaye aliinunua mpya na kuitunza kwa service na kuifanyia matengenezo kuweka spares mpya original jambo ambalo pia bongo ni nadra sana, ….
 
BMW 328 itamfaa? Au nayo magumashi?
 
BMW 328 itamfaa? Au nayo magumashi?
Kwa mwaka 2010 BMW ya kuchukua ni 323i au 335i(kama ana pesa ya wese na anataka kunyanyasa watu barabarani).

The rest atakuja kulalamikia watu humu ndani.

323i ya 2010 ina Cc2500 ikiwa na engine ya N52B25 wakati 335i ya 2010 ina Cc3000 N55 with twin scroll turbo...

The rest ndio zina engine kama N43, N45, N53, N54 ambazo zote ni engine za majaribio na zilifeli...
 
Honest opinion.
 
Hiyo nzuri.. Uhakika
328i kwa e90 ni kichomi. Ina N53 ambayo ni kama N43 iliyoongezwa cylinders mbili.

Nox sensor, Injector nozzle, coils packs, HPFP, Timing chain, Oil pressure relief valve, na mengine mengi. Hayo yote yakisumbua kwa pamoja lazima ufe kwa stroke.

Hayo matatizo yote yanatokea frequently.
 
Mjerumani hana urafiki na maskini.
 
Ahhh kumbe.. Nilijua ni N52B30..!
Then bora 330i..!
 
Engines bora za BMW zinaanzia B58 kwenda mbele.

Hizi za nyuma ilikuwa ni hit n miss.

Kama hela ipo, chukua BMW yenye engines za B58 au S58.
 
Ni kweli crown ni ndege ya chini,hakuna benzi wala bmw inaifikia kwa comfotability,ukimpa lift mtu hasa hawa dada zetu huwa hawataki kushuka
Wewe jamaa upo serious? Unavyosema hakuna Benz wala BMW umeunganisha na S Class na 7 series humo ndani sio? Hebu kuwa serious usianze kufananisha wajerumani na crown ndg
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…