'MAANDALIZI ' YA UCHAGUZI YANAENDELEA
TAFITI ZINA MENGI ZAIDI YA NAMBA
GOLI LA MKONO NI UKWELI AU UZUSHI?
Kuelekea uchaguzi, tumewaasa wapinzani kuhusu uchaguzi. Tumesisitiza, mikutano tu na sanduku la kura haitoshi
Katika nchi zenye demokrasia za mashaka kuna mambo yanayotakiwa kuangaliwa kwa upeo mpana
Majuzi wameteuliwa wajumbe wa tume ya uchaguzi
Hatujui ni kwasababu zipi lakini busara hazionyeshi kama hilo lilikuwa jambo la kufanywa kwa muda huu.
Tumesikia kauli za mwenyekiti wa tume akikemea udini kwa wapinzani.
Huko mitaani kampeni za ukanda na ukabila zinafanyika bila wasi wasi
Kilichoshtua wengine ni mwenyekiti wa tume alipopuuza kauli za CCM kwamba wapinzani hawawezi kwenda Ikulu kwa njia yoyote
Kauli hiyo si ya kampeni tukiiangalia vema. CCM wakiwa na vyombo vyote vya dola na serikali, kauli hiyo ni kuashiria hali isiyo nzuri.
Kwamba, inaweza kuwa ni maagizo ya chama tawala au inaweza kutokea hataka kama haipaswi.
Kuidharau kauli hiyo kwa kisingizio cha kampeni ni jambo tunaloliona ni la hatari na halikuwa na mizania
Siku za karibuni taasisi za tafiti za uchaguzi zimetoa matokeo.
Huko nyuma taasisi iliyokuwa inaongoza kwa tafiti hizo ni REDET ambayo wananchi wametokea kuidharau.
Viongozi wa REDET wameonekana kushiriki shughuli katika hali ya ukada wa vyama vya siasa
CCM kupitia tafiti zao zisizojulikana ziefanyikaje nayo imetoa tafiti zake ikionyesha namba zinazofanana sana na tafiti zinazoendelea
Tafiti ya Twaweza imekuja kukiwa na malalamiko mengi katika jamii juu ya usahihi wake.
Malalamiko hayo yameondoa ile thamani 'tarajiwa' ya tafiti hizo
Leo synovate wametoa tafiti, ambayo haina matokeo tofauti na yale ya CCM na Twaweza
Pengine inaweza kuwa ni msisito mzuri kuwa tafiti za Twaweza na CCM zinawiana na tafiti nyingine ili kuondoa sintofahamu
Tafiti zinaweza kufanana hata hivyo, hata kama zimefanyika nyakati tofauti au za karibu sana kama hizi tunazoona
Tafiti hizi zimekuja ikiwa ni takribani mwezi mmoja kamili hadi uchaguzi.
Zimekuja kukiwa na mkanganyiko wa kampeni na hali kutokuwa nzuri hasa kwa upande husika.
Hatuwezi kupingana na takwimu zao, isipokuwa tunazihoji kwa kina na kubaki na maswali mengi kuliko majibu
Kwa mtazamo wetu, taasisi zote zinaonekana kukaa ''kikao'' na kuamua tafiti zianze lini na zimalizike lini.
Katika kipindi cha wiki moja tafiti zote ikiwemo ya CCM zimetoka, ndani ya mwezi mmoja kuelekea uchaguzi.
Pengine huo ni muda wa kutosha, hata hivyo kuna maswali yanatatiza sana
Katika nchi za wenzetu, tumeshuhudia tafiti zikiwa kichocheo au kivunja moyo cha kambi husika.
Na mara nyingi sana tafiti hutegemea upande kama sehemu ya kampeni ukiacha zile za kimataifa zinazohifadhi hadhi na heshima yao
Huko nyuma MwanaCCM mmoja alizungumzia goli la mkono. Kwamba, iwe iwavyo CCM itashinda hata kwa goli la mkono
Kauli hiyo imefuatiwa na ile ya wapinzani hawawezi kuingia Ikulu kwa njia yoyote
Goli la mkono katika nchi ya kidemokrasia si jambo zuri. Na wala goli la mkono si kura au wizi tu.
Goli la mkono ni lazima laweza kuwa la kisaikolijia kwa wahusika.
Ni kwa njia hiyo goli la mkono linaweza kupata uhalali hata referee kupeta ikiwa limejengewa mazingira mazuri toka mwanzo
Goli la mkono walilosema CCM inaweza kuwa mzaha, hata hivyo, lisidharauliwe maana linawezekana kabisa.
Haiwezekani kauli ya goli la mkono ianguke kutoka hewani tena wahusika wakiwa kimya na viongozi wakiwa kimya!
Goli la mkono hatujui ni kitu gani, inaweza kuwa kauli ya kampeni kama ile ya hawezi kwenda Ikulu.
Tume ya uchaguzi inaweza kutusaidia maana hatujui goli la mkono katika uchaguzi wa kura lina maana gani
Tusemezane
Mwalimu wangu Nguruvi3 kwema? Unisamehe kwa kukaa kimya muda mrefu Jamvini, nilikua na majukumu mengi kdg, japo huwa nakusoma sana pamoja na wadau wengine wa Jamvi.
back to the topic, nimeufuatilia uchaguzi huu kwa karibu sana na mpaka sasa kumekua na sintofaham nyingi sana kwa pande zote CCM na Upinzani ( hapa nawazungumzia UKAWA maana ACT kwa hakika wanasikitisha na sidhani kama ni wapinzani halisi kwa mienendo yao). Pia nafasi ya tume na vyombo vingine vya dola Nitawazungumzia kdg hapo chini ACT na nafasi yao kwa uchaguzi huu.
Kwa upande wa upinzani nimewaona kama vile walikua bado hawajajipanga kwenye kugawana majimbo vizuri na hii inawaletea migogoro ambayo kimsingi haikupaswa kuwepo kabisa, maana inawapa mwanya adui yao kujipenyeza miongoni mwao na kuwachezesha shere bila sababu ya msingi, hii athari yake ni kubwa sana kwenye umoja wao na pia kujipanga zaidi kwaajilinya nafasi ya uraisi, pia bado msisitizo wa kuelewa kwamba sio UKAWA wanaogombea bali ni CDM maana kama vile watachanganyikiwa. Pia viongozi wengi wa UKAWA ni kama hawajielewi wanakurupuka sana na kujikuta wanakosa focus.
Ka CCM kwa mara ya kwanza nimeona kampeni za kipekee na zinazojaa kahsfa, matusi na personal attacks kwa upinzani tena wazi wazi bila kukemewa kuna "character assassination" ya wazi kabisa, mfani juzi nilimshuhudia mtu anaitwa Msukuma anasema mgombea alijisaidia jukwaani (alitumia abusive language ambayo siwezi kuiweka hapa), nilitegemea angalau akemewe au hata kuombewe radhi, looo kumbe ndio mmtindo, kimsingi ni siasa za kupanic sana. Zamani wapinzani walikua wanasiasa za namna hii na za hofu kubwa ila sasa ajabu CCM ndio wamekua na panic ya ajabu mno ya personal attacks, mgombea anajitahidi kutokwenda huko ila jopo lake linamdrag kwenda huko.
Udini na ukabila, kipekee hili jambo hata kama hatulitaki bado linaonekana kuchomoza na ninhatari sana kwa taifa, mgombea wa UKAWA aliropoka kanisani Tabora kuhusu dhehebu lake, akaomba radhi haraka, ila sasa ikazid7 kuchichewa na wapinzani wake saaana na kuchichewa kuni mpaka kuifanya big deal na kete kwao, ila sidhani kama ni uugwana kwa hawa watu kuendelea kueneza propoganda za namna hii maana ni hatari.
Pia suala la Ukabila ni risk sana kwa taifa, tumeshuhudia makada wakipiga kampeni na kuomba kura kikabila tena kwa kuongea kwamba huyu mtu ni wa kwetu, yale yale ya kanisani, inatisha sana, siasa za amna hii zitalipasua taifa siku za usoni, ni mbegu mbaya sana na nadhani tume na msajili wanaona haya.
Juzi nimeona tamko la jumuia fulani hivi ya kiislam imetoa tamko lake, ukilisoma lile tangazo na maudhui yake, utaona kwa jicho la tatu kwamba kuna shida mahali na kuna kitu nyuma yake, kwa kipindi hiki sitarajii kabisa eti taasisi huru kama ya dini ielekeze wafuasi wake eti wasipigie kura mtu fulani au chama fulani, ni ajabu sana.
ACT, mkuu Nguruvi3 kwa hili nakukumbuka sana, mada yako ya ACT mpini wa CCM kuua upinzani, mwanzo sikukuelewa kabisa, ila sasa nakuelewa vizuri kwa nn uliyaona haya miezi mingi nyuma, chaajabu kabisa watu wa chama hili kutwa kucha kazi yao ni kushambulia CDM kuliko CCM, klimsikiliza Mchange pale Zakiem, yeyekwake yeyekwake adui ni CDM na Lowassa tu sio CCM. Nimewafuatilia makada wao mitandaoni nao ni balaa, wanawapiga mawe wapinzani kuliko CCM, nabaki kujiuliza wapo kutaka dola inayoshikiliwa na CCM au wapo kutaka kuwa chama mbadala wa upinzani?? Kwamba wao wana vision ya kuwa wapinzani tu tena chini ya CCM na sio kushika dola.
Tume na vyombo vya dola, ni muhimu sana sasa tume iwe balanced kuwakemea wote wanaovunja kanuni bila kuangalia chama atokacho mtu, mathalani wengine wakikamatwa kwa kuzidisha wengine wakaachwa inazua maswali mengi sana kwamba hii sheria ipo kwaajili ya watu fulani tu au wote, hili pia ni kwa polisi, kama wameamua ku exercise nguvu yao kwa wavunja kanuni kama kuwakamata viongizi basi iwe ni kwa wote ili kundoa maswali na sintofaham.
Mwisho, kuna maisha baada ya uchaguzi, heshima na staha ni jambo la msingi sana, pia mambo yanayoelekea kuligawa taifa hili either kwa ukabila au udini basi ukemewe kwa uwazi bila aibu kabisa kwa yoyote anayetumia mbinu hizi chafu, maana tunaweza kuona ni lugha za kisiasa au kampeni, ila kimsingi tunajenga precedence na sumu mbaya sana kwa taifa.
Kimsingi nautazama uchaguzi huu kwa jicho la pekee sana na ni amuomba Mungu atuvushe salama