2015-uchaguzi mkuu na hatma ya nchi

2015-uchaguzi mkuu na hatma ya nchi

TATHMINI YA DURU KUHUSU KINACHOENDELEA

TUME YA UCHAGUZI NA UKIMYA WA MATUKIO

MATOKEO YA REJA REJA NA HOFU INAYOTANDA

Ndugu wana duru

Kama mtambuka, lipo bandiko tuilosema uchaguzi katika nchi masikiniau zinazoendelea kama yetu ni Zaidi ya sanduku la kura.


Kwamba, kuna mengi nyuma ya pazia. Tumewahi kuhoji kuhusu tume huru y uchaguzi

Matokeo yachaguzi bado anakusanywa, hatuwezi kuzungumzia lolote kwa sasa kwani ni mapema mno kufanya hivyo

Yapo tunayoweza kuyazungumzia kulingana na wakati. Kabla ya hayo,tuseme kuwa uchaguzi umefanyika kwa mujibu wa sheria zilizotokana nakatiba ya 1977 .

Katiba hii imepigiwa kelele sana kuhusu muundo wake uliojengwa kwa mfumo wachama kimoja.

Hivyo, sheria nyingi nazotumika zimeegemea upande wa chama chenye serikali, tume ya uchaguzi, kutangaza na kupinga matokeon.k

Kwa matiki hiyo , wanaofaidika na 1977 ikiwemo watendaji wa taasisi zenye masilahi wamekataa kubadili sheria ziendane na matakwa ya wakati

itihada zote za kubadili mfumo kama wa uchaguzi kupingwa kwa sheria zile zile za katiba ya 1977

Katiba ya 1977 ina matatizo ambayo watawala ima kwa ulevi wamadaraka au kiburi cha kutumia katiba ya 1977 waligoma kusuhghulikia

Hali imebadilika kiasi cha kuwashtukiza watawala.

Mfano, katiba ya 1977 haiongelei nini kitatokea iwapo mihimili miwili itamilikiwa na vyama tofauti, serikali na bunge

Katiba ya 1977 haifafanui nini kitatokea iwapo upande mmoja wa muungano utaongozwa na chama tofauti

Haielezi Rais anaundaje serikali ya mseto hilo likitokea

Ni lazima ziwepo 'busara' zitakazomwezesha Rais ajaye kupata nafasi ya kufanya kazi na majukumu yake kulingana na katiba ya 1977

Kazi ya kutafuta 'BUSARA' inahitaji umakini , ufundi na Muda wa kutosha

Inaendelea.....
 

Inaendelea....

Tume ya uchaguzi ipo kila siku na mwishowa uchaguzi mmoja ni mwanzo wa maandalizi ya uchaguzi mwingine

Tume imekuwa na muda wa kutosha kuandaa uchaguzi wa mwaka huu

Pamoja na miundo mbinu hafifu bado tuna teknolojia inayoweza kuharakisha mawasiliano kati ya mkoa na mkoa, wilaya na wilaya n.k.

Tunao mkongo wa taifa wa mawasiliano pamoja na zana nyingine za kisasa za kutuwezesha kufanya mambo kwa wepesi kuliko miaka ya nyuma

Kama miaka ya 80 na 90 tulitumia siku 4 kupata matokeo na mwaka 2015 tunatumia muda huo huo, kuna tatizo

Kazi ya tume ni kujumlisha kura zilizopigwa, haraibika n.k. ili kupata matokeo ya mwisho na kumtangaza mshindi

Inapotokea muda unakuwa mrefu kiasi kinachoonekana, hilo linazua maswali kuliko majibu

Inawezekanaje jimbo la Kigoma likamaliza uchaguzi na kupata maokeo huku Temeke,Ilala au Kinondoni zikiwa hazina kwa siku zaidi ya 2

Tume inawezaje kupata matokeo ya pembezoni na kushindwa kupata ya karibu na makao au makao makuu ya mikoa na wilaya?


TUME NA MATOKEO REJA REJA

Tume imeanza kutoa matokeo reja reja tena mengine kutoka sehemu za mbali.

Katika hali ya kawaida, tume wengi walitaraji tume imalize kazi na kutangaza matokeo ya jumla mara moja.

Kitendo cha kutoa matokeo reja reja kinatia baadhi ya watu shaka

Tukizingatia shaka iliyopo juu ya tume, inazidisha wasi wasi kwa kuzingatiatume ni kwa mujibu wa katiba ya 1977, iliyoonekana kutoafikiwa na makundi ya jamii na inayotia shaka juu ya uhuru wa tume

Kuna hoja kuwa, ikiwa kiongozi wa chama kimoja ameweza kukusanya takwimu za matokeo kwa muda mfupi, nini kinashindikana kwa tume?

Pengine wananchi wangepuuza takwimu za kiongozi huyo kama tume ingekanusha , kutoa karipio n.k. Tume imeshindwa kufanya hivyo

Itakapotokea matokeo yaliyotolewa na kiongozi huyo kwa bahati tu yakaona na ya tume au kukaribiana, tume itaeleza nini?

Hili limeleta shaka kwa kuzingatia,vyama na vyombo vya habari vimezuiliwa ili kuepuka uvunjifu wa amani

Inashangaza kiongozi huyo ambaye si mara ya kwanza ,ameachwa na tume aendelee na propaganda kana kwamba ana kinga 'immunity' dhidi ya sheria zilizotangazwa na tume na kubana sehemu nyingine ya jamii

Hatudhani kiongozi huyo ameweza kupata takwimu ikiwa tume ya uchaguzi haijaweza kutangaza matokeo ya majimbo kama Kigamboni , Ilala n.k.

KURA FEKI
Zimekuwepo habari za kukamatwa kwa maboksi ya kura feki kote nchini. Habari hizo zimekinasibisha chama kimoja kwa kiwang cha juu

Hizo ni tuhuma ambazo hazijathibitishwa katika chombo chochote cha sheria. Hata hivyo, tume iliwajibika kutoa taarifa juu ya hilo

Tume ilichagua kukaa kimya. Je ilihitaji kiasi cha gharama kuweka msemaji ili kutuliza sintofahamu hizo?

Uchaguzi umepita salama kwa kuzingatia mazingira yaliyokuwepo.

Hata hivyo, uzoefu unaonyesha matatizo hutokea pale kunakuwepo na sintofahamu, ucheleweshaji au viwango tofauti vya sheria miongoni mwa washindani.

Ndivyo ilivyotokea nchi jirani ya Kenya pale mwenyekiti wa tume ya uchaguzi alipozungumza na kuzua tafrani iliyosambaratisha taifa hilo kwa miezi kadhaa.

Hadi leo makovu hayajapona. Ni kutokana na haki kutoonekana kwa kila mmoja

ZANZIBAR NAKO BADO

Kwa nchi ndogo yenye wapiga kura chini ya laki 6, matokeo kucheleweshwa yanazua taharuki isiyo ya lazima
Tulitaraji matokeo ya Urais kutoka ZNZ pengine yangefika mapema kuliko ya vijijini kunakotangazwa na tume sasa

Huko nyuma, matokeo nchini yalitangazwa na tume hata kama wagombea waligoma kusaini. Haki ilitafutwa mahakamani

Zanzibar ina idadi sawa na wakazi wa jimbo moja kubwa la bara. Inapofikia kuna ucheleweshaji maswali yanazidi majibu

Tunafahamu, Znz wana tume yao. Hata hivyo, matokeo ya Rais husimamiwa kwa ushirikiano wa vyombo vya muungano na zanzibar

Huu ucheleweshaji wa matokeo, unaweza kuleta sintofahamu kubwa nchini.

Kunaweza kuzuka hisia tu kuwa zipo namna fulani zinaandaliwa hata kama si kweli.

Kunaweza kuzuka hisia kuwa matokeo yanaoananishwa ili kupata muafaka, hata kama madai hayo hayana ukweli

Kama ilivyosemwa hapo awali, muda na reja reja za matokeo unatia shaka na zoezi zima

Hali hiyo inaweza kuwalazimu wananchi kuamini kisicho na ukweli, kuwa muda mrefu ni katika kutafuta muafaka na 'busara'

Kutafuta muafaka unaoweza kumwezesha kiongozi atakayeshinda kuongoza akiwa na mamlaka ya mihimili na ya muungano

Busara zitumike kuweka masilahi ya taifa mbele, si 'busara' zinazoweza kuleta matatizo au usumbufu usio wa lazima


Tusemezane



 
KUGOMA KUSAINI MATOKEO

Kumekuwepo na wimbi la wagombea na mawakala wao kutosaini fomu inapotokea wameshindwa

Siku za nyuma NEC ilitoa matokeo tu na aliyehindwa aliambiwa aende mahakamani.
Kwasasa tume inasita kutoa matokeo tena ikikisisitiza kura zirudiwe kuhesabiwa

Hatudhani kuhesabu kura ni tatizo, tunajua tatizo ni kutaka maboksi yaliyopelekwa halmashauri yafunguliwe upya

Katika mazingira ya uwepo wa 'kura feki' ambao tume imeunyamazia kana kwamba ni sehemu ya uchaguzi, kurudia kuhesabu kura ni mbinu muhimu sana.

Katika masaa zaidi ya 72 masanduku ya kura hayajulikani yanalindwa na nani inatia shaka tume inapotoka hesabu zirudiwe

Tunasisitiza, tume imeshindwa kukemea kauli na tuhuma za wizi wa kura, hatudhani kama inajenga mazingira mazuri ya kushawishi umma kuwa inafanya kile inachotakiwa kwa mujibu wa sheria na si vinginevyo

HESABU ZA REJA REJA

Hizi hesabu za reja reja za matokeo ya Urais ni za kuangaliwa sana.

Wapinzani wasidhani mambo yanafanyika bila sababu.

Kuna maandalizi yanayoendelea ambayo lazima wawe mbele, penye tatizo waeleze mapema kwavile nao wana taarifa zao. Kinyume chake watakuja kushtukizwa kukiwa kumekucha

Hivi utaratibu wa kutoa matokeo reja reja una maana gani hasa? Tatizo ni kitu gani hasa?

ZANZIBAR NI LAKI 5

NEC haina maelezo kwanini kwa kushirikiana na ZEC zimeshindwa kuhesabu kura laki 5.

Kwa mwendo huo ni dhahiri watu milioni 22 itachukua zaidi ya wiki.

Kuna utaratibu unaotumika ambao wananchi wanapaswa kuujua.

Ni nini hasa kinachokwamisha matokeo?

Hivi inakuwaje kura laki 5 zihesabiwe siku zaidi ya 3?

Kuna utaratibu gani unaoandaliwa ziaid ya kura zizlizopigwa?

Kuna itifaki gani inayotaka kutumiwa katika kutoa matokeo?

Kura zimepigwa vituoni na matokeo kubandikwa. NEC inafuata itifaki gani katika kujumlisha na kutangaza kiasi kwamba wameshindwa kupata matokeo ya jimbo la Ilala lakini wameweza kupata ya kutoka Lindi?

Kuna itifaki gani inayofuatwa?

Kuna kitu hakipo sawa. Kuna jambo halipo sawa!
 
HALI YA ZNZ INAGUSA BARA

Hali ilivyo kule Znz inatia wasi wasi. ZEC wamegoma kutangaza matokeo wakati NEC wakienda 'taratiibu' na reja reja

Tumesema hapo juu, inahitajika 'busara' ili mipango iende kama ilivyokusudiwa na kumwezesha kiongozi ajaye kuwa na nafasi ya kutumikia sehemu zote za muungano au kutokuwa na kikwazo katika kuandaa miswaada na sheria

Huu mwendo wa jongoo ni katika hatua za kutoa nafasi ili watu waweze kufikiri vizuri namna gani tunaweza kudumisha amani na utulivu ili Rais ajaye wa awamu ya tano aweze kuwa na nafasi ya kuhudumia taifa na majukumu

Hata hivyo, inaonekana kuna hali ya wasi wasi sana visiwani.

Hilo linagusa huku bara kwa maana ile ile kuwa Rais atakayeshinda anatakiwa awe na udhibiti wa taifa kwa ujumla na si sehemu moja

Tunachojiuliza, hivi Rais wa awamu ya tano atawezaje kutumikia taifa akiwa hana mwenza upande mmoja wa muungano?

Hivi Rais atawezaje kuwa na ushawishi katika bunge ikiwa ikiwa masuala yanayohitaji 2/3 hayatafanikiwa kwa kukosa hiyo 2/3?

Tusemezane
 
Hivi Rais atawezaje kuwa na ushawishi katika bunge ikiwa ikiwa masuala yanayohitaji 2/3 hayatafanikiwa kwa kukosa hiyo 2/3?

Tusemezane

2/3 ya maamuzi ya Bunge haitokani na idadi ya wabunge wa vyama, inatokana na idadi ya wabunge walioshawishika na hoja husika. Ukiona hoja inashindwa kushawishi 2/3 ya wabunge basi hoja hiyo haina maslahi kwa taifa. Ndio maana tunataka Bunge mseto, ili hoja zisipitishwe kwa itikadi za vyama bali kwa maslahi ya taifa.
 
2/3 ya maamuzi ya Bunge haitokani na idadi ya wabunge wa vyama, inatokana na idadi ya wabunge walioshawishika na hoja husika. Ukiona hoja inashindwa kushawishi 2/3 ya wabunge basi hoja hiyo haina maslahi kwa taifa. Ndio maana tunataka Bunge mseto, ili hoja zisipitishwe kwa itikadi za vyama bali kwa maslahi ya taifa.
Hapana mkuu, unakumbuka suala la katiba?

Kwa utaratibu wetu wa bunge, masuala hayaumuliwi kitaifa bali kichama.
Narudia tena, unakumbuka suala la kitaifa la katiba? Je, haikuwa 2/3 iliyoahirisha mchakato?

Hoja hapa ni kuwa zipo kanuni za wingi (majority) ambayo ni ile ya 'Ndiyoo' na yapo masuala yanayohitaji 2/3
Haya huamuliwa ka utaratibu uliowekwa na CCM wa kichama kama ilivyokuwa katiba.

Hivyo Rais akikosa 2/3 ya upande mmoja au 2/3 kama ya bunge la katiba atafanyaje kazi?

Mkuu huwezi kubadili mawazo ya kichama, hakuna suala kubwa kama katiba, je tulilafanya kama taifa?


2/3 haikutoka. Sioni kama tunaweza kubadili hali iliyopo na inavyoonekana sasa itakuwa ngumu zaidi

Pili, si 2/3 tu, kuna mambo yanayohitaji kuridhiwa na pande zote za muungano.

Kwa hali ilivyo sasa Rais wa awamu ya tano ana wakati mgumu sana

Suala la katiba iliyokuwa kiporo linazidi kuwa gumu sana kwa Rais ajaye.

Hii ni kwasababu hatuna utaratibu wa masuala ya kitaifa bali kuwa loyal na vyama vya siasa.

Katiba kiporo inaonekana kufikia tamati, kitakachonusuru taifa ni muafaka
 
2/3 ya maamuzi ya Bunge haitokani na idadi ya wabunge wa vyama, inatokana na idadi ya wabunge walioshawishika na hoja husika. Ukiona hoja inashindwa kushawishi 2/3 ya wabunge basi hoja hiyo haina maslahi kwa taifa. Ndio maana tunataka Bunge mseto, ili hoja zisipitishwe kwa itikadi za vyama bali kwa maslahi ya taifa.
Mkuu hoja ngapi zimepingwa na wabunge wa vyama kama CCM na wakaitwa katika vikao?

Utamaduni wa masuala ya kitaifa haupo, kilichopo ni ubabe na mwenye nguvu au kikundi chenye nguvu ndani au nje ya bunge kinaamua masuala yote ya kitaifa, tutake tusitake. Hakuna kuangalia uzuri au ubaya wa hoja

Hakuna suala la masilahi katika ubabe. Wenzetu wanachanja mbuga sisi tumechuchumaa!

Na kwa mwendo huu tunaona na reja reja inayoendelea, tuna safari ndefu sana
 
Mkuu hoja ngapi zimepingwa na wabunge wa vyama kama CCM na wakaitwa katika vikao?

Utamaduni wa masuala ya kitaifa haupo, kilichopo ni ubabe na mwenye nguvu au kikundi chenye nguvu ndani au nje ya bunge kinaamua masuala yote ya kitaifa, tutake tusitake. Hakuna kuangalia uzuri au ubaya wa hoja

Hakuna suala la masilahi katika ubabe. Wenzetu wanachanja mbuga sisi tumechuchumaa!

Na kwa mwendo huu tunaona na reja reja inayoendelea, tuna safari ndefu sana

That is when the party has overwhelming majority. When it needs other parties to pass the decisions it MUST learn to compromise.

It can't be easy though. I remember in US they had to shut down the government just because Republicans and Democrats couldn't agree in the house.
 
That is when the party has overwhelming majority. When it needs other parties to pass the decisions it MUST learn to compromise.

It can't be easy though. I remember in US they had to shut down the government just because Republicans and Democrats couldn't agree in the house.
Hapo ndipo naona ugumu maana kuna bad precedent tayari katika maamuzi ya mambo ya kitaifa. Unakumbuka miswaada iliyopitishwa kibabe mwishoni mwa bunge kwa kutumia slogan ya majority hata bila kuwa na faida kwa taifa

Unakumbuka mswada wa mitandao unaotumiwa leo kuwahukumu vijana bila sababu kwa kubambikiwa kesi

Hali itakuwa mbaya sana kwasababu kuna upande ulizoe ubabe na mwingine kuwa bitter, huyo Rais sijui ata balance vipi

Na hali ya uchaguzi na matokeo ya NEC ya reja reja inaongeza chuki zaidi si bungeni tu hadi mitaani

Kuna tatizo kubwa lazima tukubaliane. Tumefeli kama taifa kupanga na kuchagua.

Tunakwenda tu kwasababu jua linatoka na solar energy ipo.

Kama taifa tumefeli ! Tume feli kwasababu uchaguzi wetu hata wa DARUSO una credoibility

Rais ajaye atakuwa na kazi kubwa, kutenda na kushinda nafsi zilizojaa vinyongo na chuki.

Hakuna consensus kama taifa. Tutabaki na hadithi za wenzetu wanaendelea
 
MAKOSA YAVIJANA WA UKAWA
NA HAYA YATUME,LIPO NENO

Vijana waUKAWA wamekamatwa kwa kosa la cyber crime kwa mujibu wa mwenyekiti wa CDM

Tuwakumbushewasomaji kuwa, tuliwahi kusema miswada ya sheria iliyokuwa inakimbizwa bungeni na kupitishwa kwa nguvu siku za mwisho wa bunge zililenga uchaguzi. Hayo ndiyoyanayoendelea

Hatutaingia kwa undani kuhusu kesi ya vijana hao kwasababu ipo mahakamani.

Tunachowezakusema ni kuwa shtaka lao ni la kosa za mitandao . Haieleweki ni kosa gani la mtandao lakini ndiyo mashtaka yenyewe


Kwa mujibuwa mwenyekiti wa UKAWA, wao walikuwa na kituo cha kukusanya takwimu zao kama chama cha siasa.

Ndivyo ilivyo duniani kote. Lengo ni kujua mwendendo wa uchaguzi na hilo halijawa kosa


Katika haliya kitaalamu na kiufundi, kosa limewekwa kama cyber crime, likimaanisha uhalifuwa mtandao.

Katika sheria kosa hilo haliishii hapo ni lazima liende mbali kueleza aina ya uhalifu


Hiyo ni sawana kumshtaki mtu kwa kosa la ‘shambulio' au assault.

Kwa ufafanuzi, shambulio linaweza kuwa la mabavu au linalohitaji matakwa aina Fulani
kama kubaka

Kama ingesemwa tatizo ni kukusanya matokeo, hilo lingeleta utata.

Kampeni meneja waCCM mh January Makamba si kuwa amekusanya, bali pia kutangaza.

Hivyo, katika jitihada za kukwepa ukweli huo, shtaka linawekwa kwa ujumla


January alipaswa kushtakiwa kwa kosa la kutangaza matokeo. Naye kama Nape na goli la mkono au Bulembo na katazo la kuingia ikulu kwa namna yote, wameachiwa si na tumeya uchaguzi tu bali vyombo vya dola.

Katika mazingira ya namna hii, haki haionekani kutendeka.

Kwa tension iliyopo nchini mambo kama haya yanazidi kushadidia hoja kuhusu uhuru wa uchaguzi, vyombo vyadola n.k.


Utata huo unazidishwa na NEC ambayo katika mazingira ya kuchekesha na kusikitisha,imeweza kupata matokeo kutoka maeneo yasiyo na miundo mbinu ya mawasiliano huku ikishindwa kutoa matokeo ya majiji na miji mkiubwa ikiwemo Dar es Salaam

Hililinaeleza jambo kubwa, kwamba suala si kukusanya takwimu na kuzijumlisha, bali inahusu kuzifanyia kazi kwa kina.

Huko ZNZ ZEC nayo ipo kimya ikiwasikiliza ndugu zao watakuwa na lipi

Tusem e ukweli kuwa uchaguzi wa Tanzania kama nchi umekosa credibility kuliko uchaguziwa DARUSO au chama cha mpira


Kama taifa tumeshindwa kuandika katiba yetu wenyewe.

Kama taifa tumeshindwa kuchagua viongozi wetu kwa utu na hekima


Alipo mkoloni ni kicheko, akisubiri mwaliko


Tusemezane
 
Nguruvi3 habari za asbh brodah!
Binafsi nadahan kwa katiba kutokuwa na kipengele kinachoo nyesha ikiwa rais atakosa idadi tosha ya wabunge watakao tengeneza serikal yake basi iundwe serikal ya mseto ndiyo inayopelekea mabao ya mkono tunayoyaona leo hii.

Iddi Azann kailazimisha tume ihesabu kura zake just like kama Hassanal alivyotaka huko Ilala. ona sasa za Iddi zilipohesabiwa eti zilitoshea kumpa ushindi na eti za Hassanal haziwez kuhesabwa mara ya pili.

Nape kafanyaje huko kwao yeye na mwakyembe?

Hivi unaweza kuamin Davidi Kafulila kashindwa ubunge? jaman inamaana wapiga kura awake hawakumkubali licha ya kufufua swalala escrow?

CCM imejitahd sana kuhakikisha bado inashinda kwa idadi kubwa ya wabunge na kukwepa kuja kuunda serikal ya mseto. hapo ndipo Nape anapofungwa na maneno yake mwenyewe

Hapana mkuu, unakumbuka suala la katiba?

Kwa utaratibu wetu wa bunge, masuala hayaumuliwi kitaifa bali kichama.
Narudia tena, unakumbuka suala la kitaifa la katiba? Je, haikuwa 2/3 iliyoahirisha mchakato?

Hoja hapa ni kuwa zipo kanuni za wingi (majority) ambayo ni ile ya 'Ndiyoo' na yapo masuala yanayohitaji 2/3
Haya huamuliwa ka utaratibu uliowekwa na CCM wa kichama kama ilivyokuwa katiba.

Hivyo Rais akikosa 2/3 ya upande mmoja au 2/3 kama ya bunge la katiba atafanyaje kazi?

Mkuu huwezi kubadili mawazo ya kichama, hakuna suala kubwa kama katiba, je tulilafanya kama taifa?


2/3 haikutoka. Sioni kama tunaweza kubadili hali iliyopo na inavyoonekana sasa itakuwa ngumu zaidi

Pili, si 2/3 tu, kuna mambo yanayohitaji kuridhiwa na pande zote za muungano.

Kwa hali ilivyo sasa Rais wa awamu ya tano ana wakati mgumu sana

Suala la katiba iliyokuwa kiporo linazidi kuwa gumu sana kwa Rais ajaye.

Hii ni kwasababu hatuna utaratibu wa masuala ya kitaifa bali kuwa loyal na vyama vya siasa.

Katiba kiporo inaonekana kufikia tamati, kitakachonusuru taifa ni muafaka
 
Last edited by a moderator:
Nguruvi3 habari za asbh brodah!
Binafsi nadahan kwa katiba kutokuwa na kipengele kinachoo nyesha ikiwa rais atakosa idadi tosha ya wabunge watakao tengeneza serikal yake basi iundwe serikal ya mseto ndiyo inayopelekea mabao ya mkono tunayoyaona leo hii.

Iddi Azann kailazimisha tume ihesabu kura zake just like kama Hassanal alivyotaka huko Ilala. ona sasa za Iddi zilipohesabiwa eti zilitoshea kumpa ushindi na eti za Hassanal haziwez kuhesabwa mara ya pili.

Nape kafanyaje huko kwao yeye na mwakyembe?

Hivi unaweza kuamin Davidi Kafulila kashindwa ubunge? jaman inamaana wapiga kura awake hawakumkubali licha ya kufufua swalala escrow?

CCM imejitahd sana kuhakikisha bado inashinda kwa idadi kubwa ya wabunge na kukwepa kuja kuunda serikal ya mseto. hapo ndipo Nape anapofungwa na maneno yake mwenyewe

gfsonwin

Za siku nyingi

Tatizo ni kubwa maana ZNZ inaonekana msumari umegota

ZEC hawajui nini cha kufanya

Kama tulivyosema hapo juu, hakuna aliyewahi kufikiri kuwa CCM inaweza kuwa katikawakati ilio nao

Leowanafikiria itakuwaje mhimili mmoja ukimilikiwa na upande mwingine?

Ndio maana matokeo yanatolewa kama kibaba cha mafuta ya kupikia huku maji yakipimwa

Tunachoshuhudia ni ze Comedy

Inasikitishasana, kwasababu hoja si nani kashinda.

Hoja yetu kubwa ni kufeli kila jambo katika maisha yetu. Sisi ni masikini sana duniani, hatuwezi kutumia rasilimali,hatuwezi kujiandikia utaratibu wa kutuongoza wenyewe yaani katiba. Sasahatuwezi kufanya uchaguzi wa serikali yetu.


Tumefeli kama taifa, bila kujali itikadi sisi ni felia kubwa sana

Ukilinganisha na wenzetu duniani, sisi ni felia.

Tunalaani madikteta wanaoingia madarakani kwa nguvu.

Huko mitaani sasa hivi kuna maguvu yote yakilenga kumweka kiongozi si kiongozi wa kuchaguliwa.


Tumefeli kama taifa, ni fedheha ni aibu
 
Last edited by a moderator:
Ni mtazamo wangu:


  • Hapakuwa na haja ya kuwa na BVR ikiwa upigaji kura ulikuwa ni wa makaratasi
  • Nchi imeingia gharama zisizo lazima kuendesha mradi wa vitambulisho vya Taifa na vitambulisho vya kupiga kura BVR
  • Tume imeshindwa kujifunza kutokana na matatizo ya 2000,2005,2010
  • Kulikuwa na kasoro ndogo ndogo nyingi za kutendaji
  • Tume iwe huru na ifanye tathmini ya madhaifu ya uchaguzi huu wa 2015 na kuyarekebisha kwa umakini kabla ya Januari ya mwaka wa uchaguzi wa Tamisemi 2019 na uchaguzi mkuu 2020
  • Fomu na vitabu vyenye shahada za kupiga kura hazikudhibitiwa vizuri na kuishia kuwa na walakini, upungufu na hata kutoweka na kutokea kwa kura zisizoeleweka
  • Vitabu vya kura viwe serialised, na kuwe na mfumo wa kuhakikisha vinahakikiwa kutoka kwa mchapishaji, vinafungwa na kufikishwa kituo cha kupiga kura vikiwa vimedhibitiwa
  • Uhesabu kura lazima ufanyike kwa umakini na bila kutoa fursa ya utata
  • Vyama viwe na mawakala wanaoaminika
  • Kura za kwenye vituo za udiwani, ubunge na urais zikishatangazwa kwenye kituo, ziwe kura halali na tamko la kwenye kituo liwe la mwisho. Kwenye tume iwe ni majumuisho ya jimbo na mkoa
  • Sheria za upigaji kura na matokeo zibadilishwe. Mshindi lazima apate 2/3 ya kura na si mwenye kura zote. Ikitokea hakuna mshindi wa 2/3, uchaguzi urudiwe upya ndani ya siku 90
  • Mchakato wa uandikishaji wapiga kura uanze katikati ya ngwe ya awamu (kwa uchaguzi 2020, uandikishaji na daftari la kupiga kura lifunguliwe Januari 2019, na kumalizika July 2019 kuruhusu upigaji kura wa Tamisemi 2019. Ifikapo July 2020, wapiga kura uchaguzi mkuu wawe wameshakamilisha kujiandikisha na kuhakikiwa na kutambua vituo vyao
  • Kampeni za kutafuta madiwani zianze mwanzoni mwa mwaka wa uchaguzi, kutoa fursa ya wagombea ndani ya vyama kujinadi. Majina ya mwisho ya wagombea Udiwani yatangazwe July ya mwaka wa uchaguzi
  • Kampeni za Ubunge na Urais, zianze miaka miwili kabla ya uchaguzi mkuu. Hii ni pamoja na michakato ya ndani kuruhusu wenwye nia kujinadi kwa wanachama wao na kupata ridhaa na udhamini. Aidha matokeo ya maamuzi ya wanachama kwenye majimbo yawe ya mwisho na yaheshimiwe
  • January ya mwaka wa uchaguzi, wagombea wateuliwa wa vyama kwa nafasi za ubunge na urais watangazwe na waendelee na kampeni zao mpaka siku moja kabla ya uchaguzi mkuu

Nafikiri tukifanya hili, tutakuwa na uchaguzi huru na wenye umakini 2019 na 2020
 
UCHAGUZI HURU NI PALE WATAKAPOSHINDA

ZANZIBAR YASEMA UCHAGUZI ULIGUBIKWA NA HILA


Katika mabandiko ya nyuma tumeeleza kuhusu utaratibu wa kumwezesha Rais ajaye aweze kutawala 'vema'

Tulisema, ''umakini'' unahitajika kati ya NEC na ZEC ili kuondoa sintofahamu zinazoweza kumkumba Rais ajaye

Kati ya hizo, ni ima kupoteza serikali au Bunge. Kwa mfano

Rais atakuwa na wakati mgumu ikiwa Bunge litatawali na upande mwingine.

Kwa maneno mengine Spika itabidi atoke upande tofauti na Rais huyo na hivyo maagizo ya serikali yanaweza kukwama

Na upo uwezekano baraza la mawaziri likawa la mseto. Katiba ya 1977 haina hilo na hata likilazimishwa, Rais atakosa nguvu ikiwemo za kuficha maovu kwani wapinzani watakuwa ndani ya baraza lake

Kwa upande mwingine, bunge linaweza kukataa miswada ya sheria kupitishwa kutokana na sababu mbali mbali ikiwemo kutokuwa na masilahi na umma. Hilo litampa Rais anayetarajiwa kutangazwa wakati mgumu sana

Muhimu sana ni ile hoja ya 2/3 ambayo masuala mengi kama ya muungano yatahitaji ipatikane

Tayari tumeshaona jinsi 2/3 ilivyomchezesha ngoma JK kwa kushindwa kuongoza taifa kuandika katiba.

Hili linamwacha Rais huyo aondoke akiwa na sifa mbaya ya kushindwa kuliongoza taifa kupanga utaratibu wa kujitawala.

Ni felia kubwa sana kwa kiongozi yoyote. Kwa maneno mengine nchi imefeli mikononi mwa Rais huyo

Kushindwa kuandika katiba ni sawa na kushindwa kupanga nyuma. Baba mwenye haya na aibu asingevulia hilo !!

Ili kuepusha balaa hilo, ''wataalamu'' wa mambo ya uchaguzi wanaangalia utaratibu.

Tunaona matokeo yakitolewa taratibu ili kuleta amani na utulivu. Tatizo limezuka kule Zanzibar

Mwaka huu haionekani kama CCM wameweza kufanya yao.

Inaonekana upinzani ulijipanga vilivyo na matokeo ya awali yanaonyesha CCM kupoteza dola ya Zanzibar.

Tunasema hivyo kwasababu hakuna takwimu kutoka CCM au ZEC zinazopinga zile za CUF

Katika spirit ile ile ya kuangalia pande za muungano na kumpa Rais wa muungano nafuu ya kutawala, uchaguzi uinaonekana kufutwa.

Ni mara nyingi CUF wamelalamika kuhusu kuibiwa lakini haikuwahi kutokea matokeo kufutwa

Kitendo cha maeneo mbali mbali kuzingirwa na jeshi kule znz kinaeleza zaidi na kwa sauti kubwa

Kurudia uchaguzi utakuwa mtego kwa CUF, na ni mtego mzito kwa Rais ajaye wa muungano


Ndio maana tunasema, bila kujali nani ameshinda au anaandaliwa kuongoza nchi, lazima tukubali kuwa kama taifa tumefeli

Tumepoteza maadili ya kusimamia wenzetu kwasababu sisi hatutendi tunachowaambiwa wenzetu

Kama tulivyo feli kuandika katiba, sasa tunafeli kwa uchaguzi.

Hakuna tunachoweza isipokuwa kuzunguka duniani na bakuli la omba omba.

Tumefeli tukubali hata kama hatutaki

Tusemezane
 
UCHAGUZI WAAHIRISHWA ZNZ

MAPITIO YA HOJA ZA MWENYEKITI WA ZEC

Huku kukiwa na sintofahamu kwa upande wa Tanzania bara,znz ,uchaguzi umeahirishwa na kuzua sintofahamu ya mzozo wa kikatiba

Awali, tuangalie kauli zilizotolewa na mwenyekiti wa ZEC kufuatia kauli aliyoitoa

1. Sehemu ya mwisho wa taarifa yake (Ipo JF) inasema
'' Kwa kuzingatia hayo pamoja na mengine ambayo sijayaeleza, mimi mwenyekiti wa tume ya uchaguzi ya Zanzibar nimeridhia kuwa uchaguzi huu haukuwa haki na kuna ukiukwaji mkubwa wa sheria na taartibu za uchaguzi...''

Hoja zetu
Ni sheria gani inayompa mamlaka mwenyekiti wa tume kuahirisha uchaguzi tena bila kushirikisha wajumbe wa tume?
Yapi mengine ambayo hakutaka kuyaeleza na kwanini. Je, mwenyekiti hajafungua mlango wa watu kuyaeleza mitazamo na fikra zao?

2. Aya ya kwanza ya barua yake anasema
' ...vikwazo nilivyokabiliana navyo ndio moja ya chachu iliyopelekea tume yangu ichelewe kutaoa matokeo ya uchaguzi huo ndani ya wakati uliopangwa kisheria.
..

Hoja yetu
Tume si ya mwenyekiti ni ya uchaguzi. Yeye kama mwenyekiti ni msimamizi wa tume, hakuunda tume hiyo.
Kutumia neno 'nilivyokabiliana navyo' inaonyesha ni vikwazo binafsi na si vya tume yake.
Anatumia neno 'Tume yangu' kuonyesha kuwa kazi hiyo ilifanywa na tume.
Haya maneno yanajichanganya na ni muhimu kadri tunavyoseonga mbele

3. Anasema
''Miongoni mwa vikwazo ni kutofahamiana miongoni mwa wajumbe wa tume na kufikia hatua ya baadhi ya wajumbe kuvua mashati na kuanza kupigana''

Hoja
Kutokana na namba 2 hapo juu, ni wazi wajumbe hawakuwa na muafaka kwasababu walipigana.
Hapa inaonyesha tamko ni lake kwasababu ameshatueleza kuwa wajumbe hawakufahamiana.

Tatizo la wajumbe kutofahamiana haliwezi kuwa tatizo la wapiga kura. Yeye kama mwenyekiti alitakiwa awasiliane na wateuzi wake kujua hatma ya tume na hili haliwezi kuwa sababu ya kuahirisha uchaguzi. Ngumi za wajumbe hazikuathiri upigaji wa kura

4, Anasema
''.. Ni dhahiri baadhi ya wajumbe wa tume badala ya kuwa makamishna wamekuwa wawakilishi wa vyama vyao na ikumbukwe vipo vyama vingi ambavyo havikupata fursa ya kuwa na makamishna na vimeathirika katika uchaguzi huu''

Hoja
Tume imeundwa kwa mujibu wa sheria. Siku zote mwenyekiti amesema tume hiyo ni huru.

Kitendo tu cha kusema vipo vyama visivyo na uwakilishi, ana maana hata yeye anakubaliana na uwakilishi, tatizo ni kuwa haukuwa wa jumla.Lengo la kauli hii ni kutaka kuungwa mkono na vyama vingine ili suala hili lisionekane kama tatizo la chamakinachomshinikiza

Vyama vidogo havikulalamika popote, hata CCM haikuwahi kutoa kauli.
Wapi amepata malalamiko hayo na je ana ushahidi wa hayo? Kwanini hakuutoa kama kielelezo

5. Anasema
''.. kumegundulika kasoro nyingi ikiwemo kule Pemba kuwa na daftari la wapoiga kura wengie kuliko daftari la wapiga kura''

Hoja:
Malalamiko hayo yameletwa na nani. Na kasoro hizo kwanini hazikutangazwa mapema wakati wa zoezi la kupiga kura.

Haikuhitaji uchunguzi ikiwa daftari linasema kituo kina watu 10 na badala yake kikawa na 20.
Ilikuwa suala la kufuta matokeo hayo mara moja. Kwanini imengoja siku zaidi ya nne kufikia hitimisho hili

Tutaendelea kupitia hoja
 
Nguruvi3 za siku njema sana ila tu hali ya siasa ya nchi ndo inayoumiya kichwa.

twende kwenye hoja za msingi, huko Zanzibar hivi ZEC ni ya CCM tu ama?
kimsingi ingekuwa CCM ndo imeshinda wala wasingesema haya ila kwakua wanajua CCM haitak kuachia dola ndio mana wanayasema haya. mimini miongoni mwa watu waliopewa namba mara mbili kwenye daftari la wapiga kura na hivyo daftari la kupigia kura likaja na jina la mtu mmoja mara mbili na kuwa na namba mbili tofauti.

nilichojiuliza ni je hili jina jingine nani atakayelipigia kura? ikiwa kwamba nataakiwa kupiga kura moja tu? sasa ?linapokuja swala eti daftari lilikuwa na majina mengi kuliko waliojiandikisha je waliona hilo siku ya uchaguzi tu? huwaga hawana nafasi ya kuproof read kabla?

nakubaliana na wewe kwamba kama nchi tumefeli.............tusubiri kuchekwa na akuzomewa na wenzetu
 
Last edited by a moderator:
Nguruvi3 za siku njema sana ila tu hali ya siasa ya nchi ndo inayoumiya kichwa.

twende kwenye hoja za msingi, huko Zanzibar hivi ZEC ni ya CCM tu ama?
kimsingi ingekuwa CCM ndo imeshinda wala wasingesema haya ila kwakua wanajua CCM haitak kuachia dola ndio mana wanayasema haya. mimini miongoni mwa watu waliopewa namba mara mbili kwenye daftari la wapiga kura na hivyo daftari la kupigia kura likaja na jina la mtu mmoja mara mbili na kuwa na namba mbili tofauti.

nilichojiuliza ni je hili jina jingine nani atakayelipigia kura? ikiwa kwamba nataakiwa kupiga kura moja tu? sasa ?linapokuja swala eti daftari lilikuwa na majina mengi kuliko waliojiandikisha je waliona hilo siku ya uchaguzi tu? huwaga hawana nafasi ya kuproof read kabla?

nakubaliana na wewe kwamba kama nchi tumefeli.............tusubiri kuchekwa na akuzomewa na wenzetu

Lowassa si alisema sisi tukapige kura, mambo ya NEC tumwachie yeye. Sasa huu ubishi unatoka wapi?
 
Napenda kuchukua nafasi kumpongeza Magufuli kwa ushindi aliyopata, Tumpe ushirikiano tusonge mbele..

Pia napenda kutoa pole kwa chama changu Chadema/Ukawa kwa kushindwa ila sina huruma nao maana tulisema miaka 5 iliyopita kuwa huwezi kutegemea kitu tofauti kwa tume ile ile iliyoundwa na Mwenyekiti kwa chama tawala.. kupata matokeo tofauti utakuwa ni muujiza.. Muda walikuwa nao, hoja walikuwa nazo, umma wa watanzania kulikuwa nyuma yao na kizuri zaidi hata Mwenyekiti wa CCM aliona dosari katika tume ya uchanguzi lakini Viongozi wa upinzani hawakutumia nafasi hiyo kuhakikisha wanapata tume uhuru..

Tumeona majeruhi wa hii tume akina Kafulila, Wenje, Mkosamali na wengineo lakini ninaweza kusema kwa madaa makubwa kuwa: "ngoja wajifunze"

Tushirikiane tujenge nchi yetu "labda Magufuli anaweza kufanya ambayo hayakufanywa na watangulize wake"
 
Maneno ya busara hayo Alinda.
The next big fight ya Upinzani sasa iwe ni tume huru ya Uchaguzi
 
Back
Top Bottom