2019 Africa Cup of Nations Special Thread

TZ wanakuambia changia Taifa stars ishinde. Pesa tunachanga lakini mpira tuuangalia kwa channel za Kenya. Uganda. Dubai na South Africa. Si Bora tuchangie harambe stars au bafana bafana.
Dona kantri inaomba michango tena!!
 
Hyo channel ata sisi ambao hatujalipa kifurushi chochote tunaipata bure?
 
Ipo search upya channel kwenye kisimbusi chako 101 kwa DTT and 447 kwa DTH
Asante mkuu kwakutupa moyo sisi timu mchina kuna watu walishatukandia umu ..nitaisachi hadi niipate asee
 
Hiyo Channel ndiyo ilinitoa matongotongo 1994 Kombe la Dunia.Nilikuwa sijawahi kuona Mpira live.Rafiki yangu mmoja tukiwa wadogo sana baba yake alikuwa na satellite dish akanialika kwenda kwao kuangalia mpira live mechi ya Italia na Brazil nadhani ilikuwa fainali akina Dino Baggio,Roberto Baggio,Bebeto,Dunga,Romario,nk.R. Baggio alipaisha penati.....
 
Asante mkuu kwakutupa moyo sisi timu mchina kuna watu walishatukandia umu ..nitaisachi hadi niipate asee
Hata ukiipata wataitoa hao jamaa! Nta sports ya nigeria wanaonyesha ila startimes baada ya kugundua ilo nayo wameitoa! Sisi tim mchina tuandike tu maumivu mkuu 😢
 
azam tv ni makenge kwa tulonunua dish zao nje na tanzania hicho ki utv hakioneshi sijui wanadhani kila mtu anapenda hayo movie yao wanayotafsiri kwa kiswahili??
shwain
Fanya deep searching mkuu itakuja automatically uzuri inapatikana kwenye vifurushi vyote mpaka lite.
 
Fainali za 32 za mataifa ya Afrika zinaanza leo nchini Misri kwa kushirikisha mataifa 24, ikiwa ni mara ya kwanza kihistoria.

Mataifa hayo yamegawanywa katika makundi sita yenye timu nne nne ambapo baada ya kutamatika kwa hatua ya makundi timu 16 zitafuzu kucheza hatua ya 16 bora.

Mchezo wa ufunguzi leo ni baina ya wenyeji Misri dhidi ya Zimbabwe ambao utaanza saa tano usiku majira ya Afrika mashariki sawa na saa nne kwa saa ya Afrika ya kati.

Wageni mbalimbali mashuhuri wameshawasili nchini Misri kushuhudia sherehe na mchezo wa ufunguzi akiwemo rais wa Shirikisho la kandanda duniani FIFA, Gian Infantino, Katibu Mkuu wake Fatuma Samoura.

Aidha viongozi mbalimbali wa kisiasa akiwemo rais wa Misri Abdel Fattah Al Sisi na waziri mkuu mstaafu wa Kenya Raila Amollo Odinga watahudhuria tukio hilo.

Baadhi Dondoo muhimu

Ni fainali za 32 za Afrika tangu kuasisiwa kwa mashindano hayo mwaka 1957

Kwa mara ya kwanza mataifa 24 yatashiriki fainali hizo

Nchi za Burundim Mauritania na Madagascar zimefuzu kucheza fainali hizo kwa mara ya kwanza katika historia

Tanzania inashiriki fainali hizo tangu ilipofanya hivyo mwaka 1980, fainali zilizofanyika nchini Nigeria.

Uganda ni taifa pekee la Afrika amshariki lililowahi kufika hatua ya fainali ya mashindano hayo, mwaka 1978 dhidi ya Uganda.

Misri imeshinda taji la Afrika mara saba na inanuia kushinda mara ya nane katika ardhi ya nyumbani.

rfi
 
Uganda dhidi ya Uganda.
 
Mm naswali kidogo naomba mnitoe tongo tongo
Mataifa yapo 24
Makundi 6
Tim toka kila kundi 2
Jumla ya timu= 6×2


Sasa hizo 16 wanazipataje??
 
Mm naswali kidogo naomba mnitoe tongo tongo
Mataifa yapo 24
Makundi 6
Tim toka kila kundi 2
Jumla ya timu= 6×2


Sasa hizo 16 wanazipataje??
Plus best loosers yaani mshindi wa tatu mzuri kutoka makundi manne.
Kwa maana hiyo ni kwamba kuna makundi yatatoa timu 3 na mengine 2
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…