2019 Africa Cup of Nations Special Thread

2019 Africa Cup of Nations Special Thread

FT 2:2

Punguza siasa Bw Ahmed Ahmad🙂
Madagascar wanamtukuza Ahmad Ahmad kuwa kawaletea neema kaingia madarakani tu CAF na nchi yake inaenda AFCON.

Wakati kiuhalisia ni afadhali hata ya timu ya Bongo, sasa amekutana na watu wanaopiga chenga hadi golikipa ndio wafunge.

Guinea wamefunga goli la dharau sana, ingekuwa ni mimi na kisirani changu ngumi zishawaka
 
Umejisema mwenyewe! Yaani buku tu!!
Ndiyo buku, siko peke yangu tukiunganisha buku nyingi inakuwa si buku tena, kuliko kuolewa kama mfanyavyo, ona sasa Mme wenu anataja kuwapa talaka.
 
unajuwa wamefungwa lakini kitu cha kufurahisha ni kuwa hawakucheza kutafuta draw wapate sifa hapana kama ni boxing basi wameenda round 12 toe to toe hawakuogopa jina. sasa tusitie aibu kesho kwenda kuweka bus ni lazima tu perform idara zote. wenzetu nimeona tactic wako vizuri hawakupoteza shape hata walipokuwa wana shambulia kama Uganda walivyocheza nidhamu ya juu.tuombe tu ila nikisikia tu wanasiasa wameanza nahamia Senegal....
 
FT 2:2

Punguza siasa Bw Ahmed Ahmad🙂
Siasa gani niliyoleta? Kuna mahala nimesema Madagascar amefungwa nimezungumzia Goli la kwanza tu ambalo ni la fedheha na nilihisi wangefungwa
 
Ndiyo buku, siko peke yangu tukiunganisha buku nyingi inakuwa si buku tena, kuliko kuolewa kama mfanyavyo, ona sasa Mme wenu anataja kuwapa talaka.
Acha ubinafsi, toa hela!!
 
siyo kwamba natania.... senegal 6-0 taifa staccmrs.
Mie gundu nimeliona baada eti spika Ndugai kusikia eti naye kaenda kama kiongozi wa msafara wa wabunge.
Kwa nini hatujifunzi kuwa sio vyema kwenye jambo la baraka kwa nchi kumpeleka mwenye nuksi?
Bora hata Hugo Pierre ndio angepewa uongozi wa washangiliaji
 
Kila nikitaka kuishangilia taifa stars dhidi ya Senegal ,naisikia sauti ikinambia, usimjaribu bwana mungu wako
 
Sisi wengine Mpira ni ulevi wetu nitakubali unidanganye chochote ila sio mpira

Timu yetu ya Taifa ndio kikosi kidhaifu kuliko vyote vilivyoenda huko misri (tuwashukuru ndugu zetu Uganda kwa kutusaidia kukata tiketi kwani wangeamua kucheza mpira wao tuliouzoea tusingeenda)

Tunajua watalambwa na Senegal na Algeria goli za kutosha tu

Ila tunaomba mjikakamue mpate hata sare dhidi ya harambee stars ili wasitupigie kelele mitandaoni

Pia benchi la ufundi linaliingozwa na yule mcheza kamari wa kinaigeria ni bovu mno
 
Back
Top Bottom