2019 Africa Cup of Nations Special Thread

2019 Africa Cup of Nations Special Thread

View attachment 1130345

View attachment 1130346

Michuano ya kombe la mataifa ya Afrika inatazamiwa kuanza kutimua vumbi ijumaa tarehe 21/06/2019 kwa mechi kati ya wenyeji Egypt dhidi ya Zimbabwe

Michuano hiyo itahusisha mataifa 24 ambayo yamegawanywa katika makundi 6, kila kundi likiwa na timu 4

Tanzania imefanikiwa kufuzu kwenye mashindano hayo kwa mara ya pili katika historia yake, mara ya kwanza ilikuwa mwaka 1980 na imepangwa katika kundi C

Mara ya mwisho mashindano haya yalifanyika 2017 nchini Gabon ambapo Cameroon walifanikiwa kuchukua kombe baada ya kuifunga Egypt kwa magoli 2 -1 katika mechi ya fainali

Je nchi gani unaipa nafasi ya kuchukua kombe hilo?

Nini matumaini ya Tanzania kwenye mashindano hayo?

Tutakuwa tunatumia mada hii kuhabarishana tukielekea kwenye ufunguzi wa mashindano hayo, yanayojiri wakati wa mechi, matokeo na matukio yote yanayohusiana na mashindano hayo

UPDATES

Ratiba 21/06/2019: Egypt vs Zimbabwe

Matokeo: Egypt 1 - 0 Zimbabwe

Ratiba 22/06/2019: Congo vs Uganda | Nigeria vs Burundi | Guinea vs Madagascar

Matokeo: Congo 0 - 2 Uganda

Nigeria 1 - 0 Burundi

Guinea 2 - 2 Madagascar

Ratiba 23/06/2019: Morocco vs Namibia | Tanzania vs Senegal | Kenya vs Algeria

Matokeo: Morocco 1 - 0 Namibia | Tanzania 0 - 2 Senegal | Kenya 0 - 2 Algeria

Ratiba 24/06/2019: Ivory Coast vs South Africa | Tunisia vs Angola | Mali vs Mauritania

Matokeo: Ivory Coast 1 - 0 South Africa | Tunisia 1 - 1 Angola | Mali 4 - 1 Mauritania

Ratiba 25/06/2019: Cameroon vs Guinea Bissau | Ghana vs Benin

Matokeo: Cameroon 2 - 0 Guinea Bissau | Ghana 2 - 2 Benin

Ratiba 26/06/2019: Nigeria vs Guinea | Uganda vs Zimbabwe | Egypt vs Congo

Matokeo: Nigeria 1 - 0 Guinea | Uganda 1 - 1 Zimbabwe | Egypt 2 - 0 Congo

Ratiba 27/06/2019: Madagascar vs Burundi | Senegal vs Algeria | Tanzania vs Kenya

Matokeo: Madagascar 1 - 0 Burundi | Senegal 0 - 1 Algeria | Tanzania 2 - 3 Kenya
Siyo kwamba watz hawaipendi taifa stars , ila TFF wamekosea sana kuruhusu wanasiasa katika timu ya taifa

Ccm 2. Kenya 3

Stliglier gorge
SGR
ATCL
 
Daah! Hatimaye tumeshatimiza malengo ya kushiriki AFCON.

Kwa mbaali nilijutia usingizi wangu wa jana kukaa macho mpaka saa saba na mwishowe kuambulia kichapo.
Mi hata kabla ya michuano nilijua tz itaenda kutalii tu

Haitashinda mechi hata moja , kwahiyo hata Sina presha
 
Mi hata kabla ya michuano nilijua tz itaenda kutalii tu

Haitashinda mechi hata moja , kwahiyo hata Sina presha
Daah! Afadhali uliyajua hayo mapema mimi niliweka matumaini mechi ya jana kwamba ingetutoa kimasomaso ila kwa kuwa ilikuwa kinyume basi hapa najua ndio ishatoka kwani kwa Algeria hatuambulii kitu pale.
 
Daah! Afadhali uliyajua hayo mapema mimi niliweka matumaini mechi ya jana kwamba ingetutoa kimasomaso ila kwa kuwa ilikuwa kinyume basi hapa najua ndio ishatoka kwani kwa Algeria hatuambulii kitu pale.
Ila kitendo cha kushiriki ile michuano baada ya miongo karibia 4 ni ushindi mkubwa kwetu ila wakati wetu wa kufanya vyema haupo mbali.
 
Ila kitendo cha kushiriki ile michuano baada ya miongo karibia 4 ni ushindi mkubwa kwetu ila wakati wetu wa kufanya vyema haupo mbali.
Na kweli Mkuu japo tuombee kufanikiwa tena kushiriki safari ijayo kwani nje ya hapo ikapita miaka zaidi ya kumi basi tukija kushiriki tutaanza tena upyaaa.
 
Hahahaaaa. Msameheni bana best maana kajua kuwaudhi sana.

Poleni maana naona wana CDM wote mumeichukia Taifa Stars kisa hiyo Clip. Lol
Ana mambo ya ajabu sana huyo jamaa alissema Taifa stars itashinda kama CCM inavyoshindanga nikajiuliza CCM huwa inashinda au inaiba,nilitegemea kuona mikakati ya kuiba magoli jana lakini sikuona kitu labda alimkosa Jecha.
 
Back
Top Bottom