Kombe la Dunia la wanawake halina mvuto sana, walipe promo bana lisikike vizuri
Kwa upande wangu ilikua ni penalty halali kabisa....ila ilivyorudiwa daaah ...anyway kwenye mkeka nilimuua nigeria...Naskilizia copper americano sasa nione kama Brazil na Chile watanipa hayo mamilioni.I hope hawataniangushaNigeria ilicheza mchezo mzuri sana dhidi ya Ufaransa lakini wamekatishwa tamaa sana na refa kwa kutoa penalty halafu akarudia tena hiyo penalty baada ya ile ya kwanza kwenda nje huku akimpa kipa yellow card na mchezaji mmoja red card. Dakika kumi za mwisho zilikuwa ngumu kwa Nigeria kwa vile ilikuwa na wachezaji kumi tu lakini iliwadhibiti sana Ufaransa. Yule refa alikuwa mwepesi sana kupiga filimbi na kutoa kadi dhidi ya Nigeria lakini kwa upande wa ufaransa Nigeria lakini ufaransa ikifanya makosa yale yale hachukui hatua yoyote.Hata hivyo nadhani Ufaransa wanajua kuwa ushindi walioupata wa 1-0 ulikuwa siyo halali yao.
Sweden illifunga Thailand 5-1; golikipa wa Thailand alikuwa hakufanya jitihanda za kutosha kuzia magoli.
USA illifunga Chile 3-0, ila golikipa wa Chile Bibie Endler alizuia mabao mengi sana; ilifikia watanangazaji wanamwita kuwa ni the best goalkeer in the world. Ifingekuwa jitihada zake Chile pia ingenyeshewa mvua ya mabao
China na Spain wametoka sare ya 0-0 wakati Ujerumaniimeibugiza South Africa 4-0. Kwa hiyo South Africa mbio zao zimefikia ukingoni. China imekuwa ya tatu kwa sababu GD inawa ina point sawa na Spain kwenye kundi B
Kuna wachezaji wa kike huko wanacheza kuliko Taifa StarsBado lina safari ndefu lakini katika baadhi ya nchi lina mvuto mkubwa sana hata TV ratings ziko juu pia lakini hazifiki hata 10. Uchezaji pia wa baadhi ya nchi hasa zile zenye ligi ya wanawake umepanda sana kiasi ambacho baadhi ya wacheza wanavyosukuma ball unaweza kufanya double take ili kuhakikisha ni KE na si ME. 😎
Anakipiga na PSG ya ufaransa, Endler ni hatari huyu binti, sema wachezaji wa Chile ndo wanamuangushaKipa wa Chile ni mzuri sana, kama hachezi kwenye ligi za wanawake Europe basi msimu ujao timu nyingi zinaweza kumfukuzia ili kumsajili.
Penalty inawezekana kuwa ni halali, lakini haikuwarrant mchezaji kupewa ticket. Halafu kipa kuruka msitali wakati wa penalty hakuhitaji apewe ticket. Kipa wa Jamaica juzi alikumbwa na kadhia hiyo naye, penalty ikarudiwa lakini hakupewa ticket; inakuwaje sasa huyu wa Nigeria apewe ticket kwa kosa lile lile.Kwa upande wangu ilikua ni penalty halali kabisa....ila ilivyorudiwa daaah ...anyway kwenye mkeka nilimuua nigeria...Naskilizia copper americano sasa nione kama Brazil na Chile watanipa hayo mamilioni.I hope hawataniangusha
Hebu mwangalie Christiane Endler akiwa kazini; ilifikia washambuliaji wa USA wanajitahid kupiga mpira mbali zaidi naye kwa kuogopa kuwa ukifika karibu naye atauzuia tu, ndiyo maana wakajikuta wanapiga penalty nje.Anakipiga na PSG ya ufaransa, Endler ni hatari huyu binti, sema wachezaji wa Chile ndo wanamuangusha
Ratiba hii ni mbaya sana sasa kwa sababu mechi mbili zinafanyika kipindi kimoja; nililazimika kuhamisha TV moja kutoka kwenye family room na kuiweka kwenye social room kusudi niweze kuangalia michezo yote miwili kwa pamoja; picture in picture haikuwa option nzuri kwangu. Nadhani in Future FIFA watafikiria tena upangaji wa ratiba zao vizuri; kwani hakukuwa na sababu ya maana kwa michezo yote kufanyika 21GMT wakati siku za nyuma kulikuwa na michezo 15GMT na 18GMT. Timu zote zilicheza mchezo mzuri sana; inaonekana kuwa kadri siku zinavyokwenda ndivyo timu zinapofanya vizuri zaidi. Matokeo ya leo yamishia kuwa Brazil imewalamba Italy 1-0, na Australia imewalamba Jamaica 4-1;
Msimamo huo unaziweka timu tatu katika kundi C za Italy, Australia, na Brazil zote kuwa na point 6; ila Itally ina goal difference kubwa ya magoli 5 ambapo Australia na Brazil zote zina magoli matatu matatu. Tiebreaker inayotumika kuchagua kati ya Brazil na Australia ni namba ya yellow na red cards walizopata, ambapo Brazili walipata kadi nyingi, kwa hiyo Australia na Italy ndizo zinazovuka automatically kuingia kwenye knockout stage. Brazil, China na Nigeria zinawania nafasi nne za washindi wa tatu. Kulingana na idadi ya points na tofauti ya magoli, inaonekana kama vile China tayali imeshachukua nafasi moja kati ya hizo nne. Kulingana na michezo iliyobaki, inaonekana pia kua Brazil imeshaukua nafasi ya pile kati ya hizo nne; kwa ingawa Nigeria bado ina nafasi ya kuendelea njia yake inazidi kuwa nyembamba. Chile ikiifunga Thailand mabao matatu bila kupata kadi yoyote, na Cameron nayo ikaifunga New Zealand bao moja tu bila kadi yoyote, basi Nigeria nayo itakuwa imefunga virago.
Hahahaha, Wewe unatafuta maneno na washika bunduki.Endler "ananiudhi" sana akiwa kazini kwa sababu anakuwa anafanya vizuri zaidi ya yule wa Arsenal !!