2019 FIFA Women's World Cup

2019 FIFA Women's World Cup

Inaonekana kama vile viwanja vile unateleza sana, kwani watoto wa kike wamekuwa wanateleza na kushindwa kutimiza plani zao mara nyingi sana. Je ni kweli vina majani ya plastic?
 
Kwa bahati mbaya, mchezo wa pili nao umekwisha kwa China kuibuka kidedea kwa kuifunga South Africa 1-0. Ingawa Banyana Banyana walianza mchezo kwa woga vile na kuwaacha China wapte bao moja katika kipindi cha kwanza, kadri muda ulivyokwenda ndiovyo Banyana banyana walivyokuwa wakiongeza nguvu na kasi ya mchezo kiasi kuwa kipindi cha pili kilikuwa ni kigumu kwa pande zote. Kwa jumla mchezo huu pia ulikuwa wa nguvu na wa kussimua sana. South Africa ilikuwa na makosa machache ya ball control, lakini walikuwa na organization nzuri sana.

Michezo ya kesho ni hii hapa
1126881
 
Bingwa France au USA
USA inaweza kukumbana na kizingiti itakapopambana na Sweden tarehe 20 June kwani Sweden nayo siyo ya kudharau. Kumbuka kuwa kwenye Olympic kule Rio mbio za marekani zilifutwa na Sweden kwa njia ya penalty; na wakati huo Marekani ilikuwa na timu maveterani sana. Sasa hivi nadhani maveterani wamebaki watano tu, wengine wote ni chipukizi.
 
Mchezo wa kwanza baina ya Japan na Scotland umemalizika kwa Japan kushinda 2-1. Mwanzoni Scotalnd walikuwa kama hawajiamini na kusababisha Japan itawale mchezo sana hadi wakajipatia magoli hayo mawili, moja likiwa kwa njia ya penalty. Baada ya kipindi cha kwanza Scotland iliamka usingizingi ikaanza nayo kucheza kwa haraka na kwa nguvu kwa hiyo mchezo ukawa balanced kwa muda mrefu sana. Ilipofika mwishoni ndipo Scotland wakajipatia bao lake la pekee. Kuna wakati mlinzi mmoja wa Japan alionekana kuunawa mpira kwenye eneo la hatari lakini refa (kutoka Eithopia) akasema twende mbele, wala hakuchukua trouble ya kuangalia VAR system na wala kutoa penalty ambayo Scotalnd walikuwa wakiitaka sana. Mshika kibendera mmoja alikuwa ametoka Kenya, na mshika kibendera wa pili alitoka Zambia, kwa hiyo mchezo huo ulisimamiwa na waamuzi kutoka Afrika.

Mchezo wa pili umekwisha baada ya Itally kuwafunga Jamaica bao 5-0. Jamaica walikuwa na upungufu sana kwenye ulinzi ingawa wacheazi wa kiungo na washambuliaji walijitahid sana. Timu yote ilikuwa haina ball control nzuri, kwa hiyo hata wanapokuwa na nafasi wanashuiindwa kuumudu mpira ama unapotelea nje au unachukuliwa na upende wa adui. Golikipa wao bado alipangua penalty moja lakini refa akasema irudiwe. Itally wana washambuliaji wazuri na vile vile ball control yao ni nzuri, kwa hiyo ilikuwa ni dhahiri kuwa ushindi kwao ulikuwa umehakikishwa. Baada ya kufungwa bao tatu, Jamaica walionyesha kukata tamaa.

Mchezo wa mwisho ndio umekwisa sasa na England wameibuka kidedea kwa kuwafunga Argentina bao 1-0. Mchezo huu ulikuwa ni burudani ya aina yake has hasa kutokana na ball controll ya hali ya juu sana iliyoonyeshwa na England. Timu zote mbilie zilicheza kwa nguvu sana na kwa ufundi ingawa England ilioneakna wazi kuwaelemea Argentina. Sifa kubwa ya Argentina ilikuwa ni kwenye defense yao kwani walipandua mashambulizi ya hatari zaidi ya kumi. Sifa zaid zimwendee golikipa wa Argentina Vanina Correa ambaye alifanya kazi ya ziada kupangua mashambulizi ya england ikiwa na kupangua penalty moja. Nadhani huu utakuwa ni mmoja kati ya michezo ya kukumbukwa mwaka huu.

Week-end hii kutakuwa na michezo miwili miwili kwa siku kama ifuatavyo. Nasubiri sana michezo ya jumapili kwa sababu ni maandalizi ya USA vs Sweden

1127655
 
Kombe la Dunia la wanawake halina mvuto sana, walipe promo bana lisikike vizuri
Hata wakilipa promo bado sana wanawake kwenye soka daaah .. ..haka kajinsia bwana...Kama leo nimecheki game ya Italy na Jamaica inapigwa kross mchezaji anaruka anagongana na mpira unaingia nyavuni hajui hata kama amefunga goli khaa....Ila Marekani,Australia,Brazil,na wale watoto wa Newzealand hata Japan kidogo wakicheza na Taifa Stars ya Amunike siku hiyo Sibeti kabisa.
 
Marekani na Mwingereza nawapa nafasi ya kushinda kombe hili.
Hata wakilipa promo bado sana wanawake kwenye soka daaah .. ..haka kajinsia bwana...Kama leo nimecheki game ya Italy na Jamaica inapigwa kross mchezaji anaruka anagongana na mpira unaingia nyavuni hajui hata kama amefunga goli khaa....Ila Marekani,Australia,Brazil,na wale watoto wa Newzealand hata Japan kidogo wakicheza na Taifa Stars ya Amunike siku hiyo Sibeti kabisa.
 
Mpwa nipo likizo sijakosa game hata moja...Kuna Captain wa Italy anaitwa Gama nitaongea na TFF maana yule ni mngoni kabisa....Hapo Jamaica kuna winga anatetema hatari anaitwa Khadija Shaw mtoto mtamu balaaa.Ila kama unapenda mijimama Norway ni wanyakyusa wa Ulaya khaaaa
Duh mpwa mbona sijawaangalia kwa jicho hilo aisee...hebu labda nitajaribu game ingine
 
Mpwa nipo likizo sijakosa game hata moja...Kuna Captain wa Italy anaitwa Gama nitaongea na TFF maana yule ni mngoni kabisa....Hapo Jamaica kuna winga anatetema hatari anaitwa Khadija Shaw mtoto mtamu balaaa.Ila kama unapenda mijimama Norway ni wanyakyusa wa Ulaya khaaaa
Nilimwona Sara Gama nikajiuliza je huyu ana uhusiano wowote na Gama wa kitanzania au hilo ni jina la kireno kama lilivyokuwa Vasco da Gama. Nimefuatilia wikipedia inonyesha kuwa baba yake ni mkongoman
 
Timu ya Japan ni ya vitoto vidogo vidogo vingi sana, nadhani maveterani ni wanne au watano tu; lakini vina ball control kubwa sana. Vimewahenyesa sana Scotland leo
 
Hata wakilipa promo bado sana wanawake kwenye soka daaah .. ..haka kajinsia bwana...Kama leo nimecheki game ya Italy na Jamaica inapigwa kross mchezaji anaruka anagongana na mpira unaingia nyavuni hajui hata kama amefunga goli khaa....Ila Marekani,Australia,Brazil,na wale watoto wa Newzealand hata Japan kidogo wakicheza na Taifa Stars ya Amunike siku hiyo Sibeti kabisa.
Wakicheza na Taifa Stars, wewe bet tu kwa vile matokeo yatakuwa ni obvious; stars watalambwa. Hata japan na Ufaransa zitawalamba tu.
 
Hata wakilipa promo bado sana wanawake kwenye soka daaah .. ..haka kajinsia bwana...Kama leo nimecheki game ya Italy na Jamaica inapigwa kross mchezaji anaruka anagongana na mpira unaingia nyavuni hajui hata kama amefunga goli khaa....Ila Marekani,Australia,Brazil,na wale watoto wa Newzealand hata Japan kidogo wakicheza na Taifa Stars ya Amunike siku hiyo Sibeti kabisa.
[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3]
 
Dada zetu wa Cameron wamelwambwa 3-1 na Uholanzi. wasichana wale walicheza mchezo wa nguvu na wa kujiamni lakini ni kama vile refreee alikuwa akiwaonea sana mpaka wakapata ghadhabu. Kwa vile wao walikuwa wanatumia nguvu, yeye akawa anawap kadi ya njano kwa kutumia nguvu. Niliwaona kabisa walipata ghadhabau sana kutoka na refa kuwa anawap makadi kila wakati. Kijumula walicheza vizuri ingawa walikuwa na upungufu kidogo kwenye defense na vile vile forward line yao ilikuwa inashindwa sana kumalizia.

Canada imeifunga Newzaleand bao 2-0; na kwa jumla mchezo ulikuwa mzuri ingawa sikufurahia pande zote mbili.

Kesho dunia nzima inasubiri kuona mchezo wa US-Chile na ule wa Sweden-Thailand, kwa sababu mpaka hapo inaonekana kuwa kikwazo kwa US in Sweden na Chille. Ikiwa Chile itaibania US, halafu Sweden ikaifunga Thailand, matokeo yanaweza kuwa mengine kabisa kwa US. Kinachotakiwa kwa US ni kuona Sweden hata ikiifunga Thailand isifikishe mabao 13, halafu na yenyewe US iifunge Chile hata kwa bao moja tu.

Kwa bahati mbaya sana mwaka huu team US inamkosa huyu binti ambaye ni mja mzito akitegemea kupata mtoto wa pili. Huwa ni mshambuliaji mwenye spidi kubwa sana
1128879
 
Back
Top Bottom