dindilichuma
JF-Expert Member
- Dec 19, 2015
- 1,755
- 2,740
Naona majibu yako yanapingana na Mbowe wakati anampokea Lowasa alituaminisha Lowassa anakundi kubwa la watu. Wakati Mpinzani wa ujio wa Lowasa yeye alitaka tathmini ifanyike kama Lowasa ni liability au asset?Huenda unadhani unajadili na mtoto au mgeni wa siasa na mtu asiyejua lolote. Kwa taarifa yako mafanikio ya cdm yaliletwa na kazi kubwa ya siasa iliyofanywa na cdm mara baada ya uchaguzi mkuu wa 2010. Kipindi cha toka 2010 mpaka 2015 cdm ndio chama cha siasa kilichofanya mikutano na kukutana na wananchi wengi kuliko chama chochote cha siasa ikiwemo ccm. Na hilo halina mjadala, wakati hayo yakifanyika hizo taka ngumu toka ccm chini ya Lowassa walikuwa wanazunguka kwenye nyumba za ibada kugawa pesa. Ingekuwa hao wanaccm walienda TLP au TADEA kisha wakapata viti hivyo hapo ungekuwa na hoja.
Usitake kupotosha kiwaziwazi jambo tunalolifahamu, wengi wa hao wanaccm walikuja cdm miezi miwili au mitatu kabla ya uchaguzi, na kilichowabeba ni kukubalika kwa cdm. Kwa hili la cdm kuokota hizo taka ngumu ilibidi Mbowe na kamati yake wakae pembeni kwa kuchukua vodafasta, matokeo yake zaidi ya 90% wamerudi walikota. Muda mrefu sana nimesema hata Mbowe kuendelea kuwa mwenyekiti wa cdm hivi sasa ni kosa kubwa la kiufundi, kwani hana jipya.
Hiyo 2020 mnayotishia nayo watu sio kwakuwa ccm iko imara au kwakuwa cdm ni mbovu, ila ni madaraka ya urais yanayotumika vibaya. Wote tumeshuhudia chaguzi zote toka awamu hii imeingia madarakani zikinajisiwa waziwazi, kukiwa na uhayani, ukatili na ukiukwaji mkubwa wa sheria za uchaguzi, na yote haya yanafanyika chini ya uratibu wa vyombo vya dola. Kile kilichowapa ushindi wa fedheha ccm kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa ndio jicho hicho kitawapa ushindi 2020 na sio kwa uwezo wa kisiasa. Hayo ya kwamba kuna maendeleo, au viongozi waliondoka cdm zitatumika tu kama sehemu ya kufichia ukweli, lakini ukweli hasa ni mamlaka zote za uchaguzi kuwa na hofu ya madaraka ya rais yanayotumika vibaya fullstop.
Pia ilikua ni Mabadiliko.. Lowasa ... Lowasa ... mabadiliko, Lowasa aliibeba CDM na sio CDM ilimbeba Lowasa.
Lowasa aliwabeba CDM kwa populality yake na uchumi wake.
Ningeona CDM wako serious kama wangewaadhibu wote waliowaingiza chaka kwenye hili.
Sent using Jamii Forums mobile app