2021 AFCON Special Thread

2021 AFCON Special Thread

Kuna wa2 wanakera sana, akiwachukia waarabu bac atataka wote wawachukie waarabu, akiona unashabikia timu yoyote ya waarabu/waislamu anatamani akupasue kichwa. Lakini kushabikia timu za mabeberu ni kawaida kwao. Huu ushenzi wa kubagua timu kisa rangi/waarabu cjui utaisha lini!

Wewe ndio umekwenda mbali zaidi umeingiza hadi udini

Naziheshimu sana timu za uarabuni kwa nidhamu yao ya mpira
Lakini binafsi sizishabikii timu za kiarabu sio kwa sababu ya udini au uarabu wao
Kuna ile dhana kwamba waarabu wana figisu sana ukienda kucheza kwao enzi hizo
Simba na Yanga imekutana sana kadhia ya hawa jamaa
Na hii kwa kiasi kikubwa imesababisha Watz wengi hawazipendi timu za uarabuni kwa kuanini wanafigisu sana licha ya ubora wao

Lakini pia waarabu wana ile dhana kujiona kama wao sio waafrika, yaani hata kama ni waafrika lakini wao ni tofauti na waafrika wengine
Hili linasababisha waafrika wengi ambao sio waarabu kutokuzishabikia timu za kiarabu...... hali hii imejenga tabaka miongoni mwa Afrika na kunakua na ile dhana kwamba mashindano ya Afrika inakua ni kama Afrika vs waarabu
Ndio hiyo unakuta sio Mkongo au Mnaijeria anataka muarabu ashinde makombe ya afrika

Kama ukitembelea mabanda umiza ni rahisi sana kuona hiki nilicho eleza hapa
 
Back
Top Bottom