2021 AFCON Special Thread

2021 AFCON Special Thread

Wewe ndio umekwenda mbali zaidi umeingiza hadi udini

Naziheshimu sana timu za uarabuni kwa nidhamu yao ya mpira
Lakini binafsi sizishabikii timu za kiarabu sio kwa sababu ya udini au uarabu wao
Kuna ile dhana kwamba waarabu wana figisu sana ukienda kucheza kwao enzi hizo
Simba na Yanga imekutana sana kadhia ya hawa jamaa
Na hii kwa kiasi kikubwa imesababisha Watz wengi hawazipendi timu za uarabuni kwa kuanini wanafigisu sana licha ya ubora wao

Lakini pia waarabu wana ile dhana kujiona kama wao sio waafrika, yaani hata kama ni waafrika lakini wao ni tofauti na waafrika wengine
Hili linasababisha waafrika wengi ambao sio waarabu kutokuzishabikia timu za kiarabu...... hali hii imejenga tabaka miongoni mwa Afrika na kunakua na ile dhana kwamba mashindano ya Afrika inakua ni kama Afrika vs waarabu
Ndio hiyo unakuta sio Mkongo au Mnaijeria anataka muarabu ashinde makombe ya afrika

Kama ukitembelea mabanda umiza ni rahisi sana kuona hiki nilicho eleza hapa
Point
 
Kwenye udini upo, kwenye ubaguzi upo.. waache watu washabikie timu wapendazo, na usilete ubaguzi wako hapa.
Kwa leo nakustahi, mtu alikuwa anataka timu yake ipite na ikawa imetolewa, nikasema labda ilikuwa inapita kwenda nyumbani, sasa hapa udini uko wapi? hebu fuatilia comments zangu na wadau wengine hapa pale timu tunazoshabikia zinapopata matokeo mabaya. Misimamo yako ya dini iko dhahiri, mapenzi yako kwa waarabu na dini yao ya jangwani humo yasikufanye kuquote kwenye vitu vya hovyo, siku nyingine nitakutolea uvivu.
 
Haliwezi kuwa tuta la hivyo. Yaani unamnawisha mtu makusudi.
Hii michezo Thierry Henry alikuwa anaipenda sana.
 
Back
Top Bottom