2022/2023 CAF interclub special thread

2022/2023 CAF interclub special thread

Smt016

JF-Expert Member
Joined
Jan 11, 2016
Posts
3,012
Reaction score
4,300
Uzi huu ni maalumu kwaajili ya kupeana update ya mashindano ya vilabu barani Africa ( Klabu bingwa na Shirikisho Africa)

Tanzania tukiwa tunawakilishwa na vilabu vinne ambsvyo ni Yanga, Simba, Azam na Geita gold ambapo Simba na Yanga watakuwa kwenye klabu bingwa wakati Azam na Geita Gold watakuwa kwenye shirikisho.

Utaratibu wote wa mashindano upo chini ya kamati ambao ndio yenye wajibu wa kusajili vilabu vitakavyoshiriki mashindano kwa msimu husika pamoja na kuwasajili wachezaji, kupanga ratiba ya mashindano na mwisho ni kujua mashirika wanachama watakaohusika na mashindano.

Kwasasa, mashirikisho wanachama wanatakiwa kuwasilisha timu zao ambazo zitashiriki mashindano ya vilabu msimu wa 2022/2023 na mwisho wa zoezi hili tarehe 31 mwezi wa 7.

Baada ya mashirika kutoa vilabu vyao vitakavyoshiriki kwenye klabu bingwa na shirikisho, CAF watapanga idadi ya timu itakazoanzia hatua ya awali na zitakazoanzia hatua ya pili. Ifahamike tu ya kwamba CAF ina wanachama 54 na katika mashindano kuna uwezekano wa baadhi ya wanachama wasishiriki mashindano kutokana na sababu zao mbali mbali ikiwemo ya kiuchumi, miundo mbinu, n.k hivyo kutokana na idadi ya wanachama wataokaoshiriki ndipo itakayoamua idadi ya timu za kuanzia raundi ya pili kwasababu inatakiwa zifike timu 32 itakazocheza raundi ya pili.

Hapo chini ni ratiba ya mashindano ya CAF ngazi ya vilabu kwa msimu wa 2022/2023

IMG_20220717_145750.jpg
 
Geita Gold ameingia kwenye shirikisho kwa kigezo kipi?
Mm nilifikiri Coastal Union ndio wenye nafasi ya pili Azam cup na kwa namna alivyopambana atacheza shirikisho barani Afrika.
Walibadili sheria muda tu, ni kwamba mshindi wa kombe la shirikisho la Azam pekee ndiye mwenye tiketi ya kuingia ya kucheza kombe la shirikisho Africa. Zaidi ya hapo anachukuliwa walioshika nafasi ya tatu na ya nne kwenye msimamo wa ligi kuu
 
Hii sheria iliwekwa kipindi Yanga au Simba alikuwa hana uhakika wa nafasi ya 4?
 
Hapo awali TFF hawakuweka utaratibu unaoeleweka wa kumpata mwakilishi wa kombe la shirikisho Africa. Msimu wa mwaka 2018/2019 kombe la Azam lilibebwa na Azam na Lipuli wakawa washindi wa pili, lakini cha ajabu Lipuli akaachwa kuwakilisha mashindano ya CAF confederation na badala yake wakampa KMC kwavile kashika nafasi ya nne kwenye msimamo wa ligi kuu hivyo ikawa runners-up wa kombe la Azam hana nafasi kwenye CAF confederation cup.

Msimu wa 2019-2020
Simba anachukua kombe la Azam dhidi ya Namungo, lakini cha ajabu hapo TFF wameona runners-up ndiye anayepaswa kuwakilisha nchi kwenye kombe la CAF confederation cup hivyo Yanga ambao walikuwa wa pili kwenye msimamo wakashindwa kuwakilisha nchi kwenye michuano ya CAF confederation cup. Kulikuwa na malalamiko kadhaa juu ya kutokuwepo na utaratibu maalumu bali TFF kujiamulia tu wanachojisikia ndipo ikaja kwa utaratibu huu wa mshndi pekee wa kombe la Azam ndiye atakayepaswa kuwakilisha nchi zaidi ya hapo pambana kwenye ligi ushike nafasi za juu
 
Sawa nimeelewa japo sikubariani na utaratibu uliowekwa
 
Uzi huu ni maalumu kwaajili ya kupeana update ya mashindano ya vilabu barani Africa ( Klabu bingwa na Shirikisho Africa)

Tanzania tukiwa tunawakilishwa na vilabu vinne ambsvyo ni Yanga, Simba, Azam na Geita gold ambapo Simba na Yanga watakuwa kwenye klabu bingwa wakati Azam na Geita Gold watakuwa kwenye shirikisho.

Utaratibu wote wa mashindano upo chini ya kamati ambao ndio yenye wajibu wa kusajili vilabu vitakavyoshiriki mashindano kwa msimu husika pamoja na kuwasajili wachezaji, kupanga ratiba ya mashindano na mwisho ni kujua mashirika wanachama watakaohusika na mashindano.

Kwasasa, mashirikisho wanachama wanatakiwa kuwasilisha timu zao ambazo zitashiriki mashindano ya vilabu msimu wa 2022/2023 na mwisho wa zoezi hili tarehe 31 mwezi wa 7.

Baada ya mashirika kutoa vilabu vyao vitakavyoshiriki kwenye klabu bingwa na shirikisho, CAF watapanga idadi ya timu itakazoanzia hatua ya awali na zitakazoanzia hatua ya pili. Ifahamike tu ya kwamba CAF ina wanachama 54 na katika mashindano kuna uwezekano wa baadhi ya wanachama wasishiriki mashindano kutokana na sababu zao mbali mbali ikiwemo ya kiuchumi, miundo mbinu, n.k hivyo kutokana na idadi ya wanachama wataokaoshiriki ndipo itakayoamua idadi ya timu za kuanzia raundi ya pili kwasababu inatakiwa zifike timu 32 itakazocheza raundi ya pili.

Hapo chini ni ratiba ya mashindano ya CAF ngazi ya vilabu kwa msimu wa 2022/2023

View attachment 2294183
Timu kumi zinaanzia raundi ya pili, ikiwemo Simba
 
Hakuna guarantee ya timu 10 kuanzia hatua ya pili bali inategemea na idadi ya wanachama watakaoshiriki michuano.

Timu zinatakiwa ziwe jumla ya 64 ili zikicheza mechi za hatua ya awali zitoke 32 na zibakie 32 ambazo ndio zitacheza hatua inayofuata (hatua ya pili) na kisha zibaki timu 16 zitakazounda unda makundi manne.

Mfano msimu uliopita kulikuwa na wanachama 42 tu walioshiriki michuano katika jumla ya wanachama 54. Ukichukua idadi ya 42 ukitoa mashirikisho 12 zinazoingiza timu mbili mbili unabakiwa na wachama 30 walioingiza timu moja moja, hivyo imefanya kuwe na jumla ya timu 54 zilizoshiriki michuano ya klabu bingwa. Katika 54 ili timu zifike 64 kuna gap ya timu kumi hivyo hizo timu kumi ndio zilizoanzia hatua ya pili. Huku timu 44 zikianzia hatua ya awali ili kuweza kubalance timu zifike 32 zitakazocheza hatua ya pili.
64-54= 10
54 -10 = 44
44/2= 22
22+10=32
 
Umeelezea kitaalamu sana, sidhani kama mashabiki wa Mbumbufu S.C wanaelewa hili
 
njaakalihatari , Scars, OKW BOBAN SUNZU tumalizie maombi ya mwisho
 
Nimethibitisha pasi na kuacha shaka kwamba unayajua haya mambo. Hongera sana.

Nina swali dogo, ni ipi status ya Zanzibar kwenye mashindano ya CAF ?
Wanapata benefits zote za ngazi ya vilabu lakini hawazipati kwa ngazi ya timu za taifa. Why
 
Timu kumi zinaanzia raundi ya pili, ikiwemo Simba
Mimi ni shabiki wa Simba, lakini huwa napenda watu wawe wanaelewa zaidi kuliko kukariri. Hakuna idadi kamili ya timu bora kuanzia raundi wa pili ya CAF CL. Hizo timu kumi zilikuwani kwa msimu uliopita, kila msimu idadi hupungua au huongezeka kulingana na idadi ya timu zote zilizothibitisha kushiriki. Kwa hiyo licha ya Simba kuwemo katika 10 bora ya washiriki wa CAF CL, inawezekana kabisa kwa msimu huu zikachukuliwa timu 7 au hata 12. Lengo la wapanga ratiba ni kwamba timuzichujane katika raundi ya awali lakini kwa namna yoyote round ya kwanza zibaki timu 32, ili makundi ziwepo timu 16. Sasa kwa kuwa idadi ya nchi na timu zinazothibitisha hubadilika mwaka hadi mwaka, hata timu zinazoanzia raundi ya awali idadi yake hubadilika. Kwa hiyonusishangae msimu huu Simba yumo katika 10 bora za washiriki lakini akaanzia raundi ya awali
 
Rasta maombi ya nini?
Mkuu mmesahau, maombi yalianza kwa Etoil du Sahel, yakaja kwa Orlando pirates na sasa inabidi kumalizia kwa wanachama washirika wa CAF wasilete timu nyingi ili timu ya Simba ianzie hatua ya pili
 
Simba kushiriki hatua ya pili ni uhakika mzee, wanaonzia hatua ya awali washajulikana
 
Back
Top Bottom