Smt016
JF-Expert Member
- Jan 11, 2016
- 3,012
- 4,300
Uzi huu ni maalumu kwaajili ya kupeana update ya mashindano ya vilabu barani Africa ( Klabu bingwa na Shirikisho Africa)
Tanzania tukiwa tunawakilishwa na vilabu vinne ambsvyo ni Yanga, Simba, Azam na Geita gold ambapo Simba na Yanga watakuwa kwenye klabu bingwa wakati Azam na Geita Gold watakuwa kwenye shirikisho.
Utaratibu wote wa mashindano upo chini ya kamati ambao ndio yenye wajibu wa kusajili vilabu vitakavyoshiriki mashindano kwa msimu husika pamoja na kuwasajili wachezaji, kupanga ratiba ya mashindano na mwisho ni kujua mashirika wanachama watakaohusika na mashindano.
Kwasasa, mashirikisho wanachama wanatakiwa kuwasilisha timu zao ambazo zitashiriki mashindano ya vilabu msimu wa 2022/2023 na mwisho wa zoezi hili tarehe 31 mwezi wa 7.
Baada ya mashirika kutoa vilabu vyao vitakavyoshiriki kwenye klabu bingwa na shirikisho, CAF watapanga idadi ya timu itakazoanzia hatua ya awali na zitakazoanzia hatua ya pili. Ifahamike tu ya kwamba CAF ina wanachama 54 na katika mashindano kuna uwezekano wa baadhi ya wanachama wasishiriki mashindano kutokana na sababu zao mbali mbali ikiwemo ya kiuchumi, miundo mbinu, n.k hivyo kutokana na idadi ya wanachama wataokaoshiriki ndipo itakayoamua idadi ya timu za kuanzia raundi ya pili kwasababu inatakiwa zifike timu 32 itakazocheza raundi ya pili.
Hapo chini ni ratiba ya mashindano ya CAF ngazi ya vilabu kwa msimu wa 2022/2023