2022/2023 CAF interclub special thread

Asantee...
 
Azam sijajua kwa nini ?
 
Team ni 68 au 64 mbona lugha gongana
 
Team ni 68 au 64 mbona lugha gongana
Soma uelewe usikimbilie ku comment tu mkuu. Kwanza hakuna nilipoandika timu 68 bali 58.

Ni hivi kawaida kunatakiwa kuwe na timu 64 ambazo zinatakiwa zicheze mechi za hatua ya awali ili timu 32 zibaki kucheza hatua inayofuata ambayo ni hatua ya pili na timu 32 zingine zitoke. Lakini kutokana na wachama 46 pekee kushiriki michuano ya klabu bingwa inamaana timu hazitoweza kufika 64 kwasababu katika wanachama 46 kuna wanachama 12 wanapaswa kutoa timu mbili klabu bingwa hivyo italeta timu 24 na wanachama 34 waliobaki wanatoa timu moja pekee Klabu bingwa hivyo jumla timu zinakuwa 58 pekee ndani ya msimu huu.
.
Kutoka timu 64 mpaka 58 kuna gap ya timu sita hivyo hizo timu sita ndizo zitakazocheza hatua ya pili ili kubalance timu ziwe 32 katika michezo ya hatua ya pili.

Umeelewa?
 
vip kuhusu Azam kuanzia hatua ya pili ni kigezo gani kimetumika mkuu?
 
swali la nyongeza mheshimiwa spika,
ikitokea nchi zote wanachama 56 zikapeleka timu kwenye cafcl, ina maana baki kufikia 64 ni timu 8,
je namba itabadilika kutoka wanachama 12 wanaoingiza timu mbili mbili na kuwa 8 au itakuaje?...
 
Kama
kuna mtu bado hajaelewa mpaka hapa basi hata aje malaika kuelezea hataelewa kitu. Ahsante sana na usimba wangu nimeelewa vizuri

 
Hakika... Uko sahihi kabisa...

Sent from my TECNO LA7 using JamiiForums mobile app
 
vip kuhusu Azam kuanzia hatua ya pili ni kigezo gani kimetumika mkuu?
Ishu ya Azam kiukweli namimi imenichanganya sijui ni kigezo kipi kimetumika
 
swali la nyongeza mheshimiwa spika,
ikitokea nchi zote wanachama 56 zikapeleka timu kwenye cafcl, ina maana baki kufikia 64 ni timu 8,
je namba itabadilika kutoka wanachama 12 wanaoingiza timu mbili mbili na kuwa 8 au itakuaje?...
Swali lako linajibu ndani yake. Ikitokea wanachama 56 zimepeleka timu, ni lazima idadi ya wanachama watakaoingiza timu mbili mbili zitapungua ili kubalance zipatikane timu 64.
 
Ishu ya Azam kiukweli namimi imenichanganya sijui ni kigezo kipi kimetumika
nadhani formula ni ile ile, japo kuna kitu caf wamekosea.....

kwenye CAFCC kuna timu 50, ambapo huku timu huwa zinaenda a three round robin ku-qualify kwenda group stage,......

sasa, tuchukulie hizo timu 50 ndio zipo, na timu 13 ndio zinaanzia hatua inayofuata.... it means 50-13=37 (tayar hii namba haigawiki kwa mbili, ndio kosa lilipo)......

sasa, tuassume scenario mbili hapa,

scenario ya kwanza, tu-assume wamekosea idadi ya timu zitakazoanzia hatua inayofuata, labda ni 14........

so lets say ni 14,
kwaio 50-14=36,
round ya awali itakua 36/2=18.....

round ya kwanza 18+14=32, i.e 32/2=16,

QF round itakua 16 +16(zilizotolewa CL) =32/2 =16 group stage!

so katika timu zenye ranking ya juu upande wa CC ina maana Azam imo kati hzo 14 (13 kama walivyosema wao caf), hata hivyo Azam hana points labda kapewa kwa sababu ya ushiriki wao.......
 
Wewe umwmuona uyo tu daah ila watz sisi ni hatari kwa ustawi wa hii dunià asee
 
Kwa hali halisi nimayoina mwaka huu simba na yanga zinatoka mapema kabisa hata kwenye makundi hazisogei
 
Geita Gold ameingia kwenye shirikisho kwa kigezo kipi?
Mm nilifikiri Coastal Union ndio wenye nafasi ya pili Azam cup na kwa namna alivyopambana atacheza shirikisho barani Afrika.
kamuni hazimpi nafasi mshindi wa pili wa Azam FA Cup.Geita Gold Kawa wa nne Premier league ana sifa ya kuwakilisha
 
[emoji122][emoji122][emoji122]
 
Kwan caf si walishatoa list ya timu kutoka kwenue kila nchi na kwenye hiyo yaarifa walisema timu ambazo ziliandikwa kwa bold zitaanzia raundi ya pili au hiyo taarifa ilikuwa ya nan?
 
Na kama timu zinazoshiriki ni 58 kama mmoja wa wachangiaji alivyosema then timu 6 tu ndizo zitasubiria second round

Yaani kimahesabi itakuwa hivi
58 - 6 = 52

Hao 52 watatoana na kubaki 26

Hao 26 wataenda kuungana na wale 6 kukamilisha timu 32 kwa ajili ya second round
Ova
 
Update

Siku ya jumatano, majira ya saa saba mchana kwa muda wa Africa Mashariki raisi wa CAF Dr Patrice Motsepe atazindua mashindano ya Super league. Uzinduzi huo utafanyika jijini Arusha.

Pia leo siku ya jumanne ya tarehe 9 kutafanyika draw ya michezo ya hatua ya awali. Draw hiyo itafanyika saa kumi kwa majira ya Misri ambayo ni sawa na saa kumi na moja kwa majira ya Africa Mashariki. Hivyo leo ndio siku ya kujua nani kapangiwa na nani, aidha michezo ya kwanza katika hatua hii inatarajiwa kuchezwa tarehe 9 -11 mwezi wa tisa huku marudiano yakiwa tarehe 16-18 mwezi wa tisa.

Tusubiri tuone timu zetu za Tanzania zitapangiwa na timu zipi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…