2022/2023 CAF interclub special thread

2022/2023 CAF interclub special thread

Update:

Mnao tarehe 9 mwezi huu wa nane, CAF wataendesha draw kwa ajili ya michezo ya hatua ya awali. Jumla ya wanachama 46 wamejitokeza kushiriki michuano ya kimataifa.

Hivyo kimahesabu ni kwamba kutakuwa na timu 58 zitakazoshiriki klabu bingwa kutoka mataifa 46 wanachama wa CAF. Yaani 46-12= 34
12x2= 24 hivyo jumla ya timu ni 34+24= 58

Kutokana na hesabu hiyo, ni timu sita pekee ndizo zilizopelea kufika timu 64 hivyo basi timu zote zitaanzia hatua ya awali isipokuwa timu sita bora tu kutoka kwenye 5 year CAF ranking ndio wataanzia hatua ya pili.

Hapa chini ni orodha ya vilabu na wanachama shiriki wa michuano ya kimataifa View attachment 2317575
Asantee...
 
Azam sijajua kwa nini ?
 
Team ni 68 au 64 mbona lugha gongana
 
Team ni 68 au 64 mbona lugha gongana
Soma uelewe usikimbilie ku comment tu mkuu. Kwanza hakuna nilipoandika timu 68 bali 58.

Ni hivi kawaida kunatakiwa kuwe na timu 64 ambazo zinatakiwa zicheze mechi za hatua ya awali ili timu 32 zibaki kucheza hatua inayofuata ambayo ni hatua ya pili na timu 32 zingine zitoke. Lakini kutokana na wachama 46 pekee kushiriki michuano ya klabu bingwa inamaana timu hazitoweza kufika 64 kwasababu katika wanachama 46 kuna wanachama 12 wanapaswa kutoa timu mbili klabu bingwa hivyo italeta timu 24 na wanachama 34 waliobaki wanatoa timu moja pekee Klabu bingwa hivyo jumla timu zinakuwa 58 pekee ndani ya msimu huu.
.
Kutoka timu 64 mpaka 58 kuna gap ya timu sita hivyo hizo timu sita ndizo zitakazocheza hatua ya pili ili kubalance timu ziwe 32 katika michezo ya hatua ya pili.

Umeelewa?
 
vip kuhusu Azam kuanzia hatua ya pili ni kigezo gani kimetumika mkuu?
 
swali la nyongeza mheshimiwa spika,
ikitokea nchi zote wanachama 56 zikapeleka timu kwenye cafcl, ina maana baki kufikia 64 ni timu 8,
je namba itabadilika kutoka wanachama 12 wanaoingiza timu mbili mbili na kuwa 8 au itakuaje?...
 
Kama
Uzi huu ni maalumu kwaajili ya kupeana update ya mashindano ya vilabu barani Africa ( Klabu bingwa na Shirikisho Africa)

Tanzania tukiwa tunawakilishwa na vilabu vinne ambsvyo ni Yanga, Simba, Azam na Geita gold ambapo Simba na Yanga watakuwa kwenye klabu bingwa wakati Azam na Geita Gold watakuwa kwenye shirikisho.

Utaratibu wote wa mashindano upo chini ya kamati ambao ndio yenye wajibu wa kusajili vilabu vitakavyoshiriki mashindano kwa msimu husika pamoja na kuwasajili wachezaji, kupanga ratiba ya mashindano na mwisho ni kujua mashirika wanachama watakaohusika na mashindano.

Kwasasa, mashirikisho wanachama wanatakiwa kuwasilisha timu zao ambazo zitashiriki mashindano ya vilabu msimu wa 2022/2023 na mwisho wa zoezi hili tarehe 31 mwezi wa 7.

Baada ya mashirika kutoa vilabu vyao vitakavyoshiriki kwenye klabu bingwa na shirikisho, CAF watapanga idadi ya timu itakazoanzia hatua ya awali na zitakazoanzia hatua ya pili. Ifahamike tu ya kwamba CAF ina wanachama 54 na katika mashindano kuna uwezekano wa baadhi ya wanachama wasishiriki mashindano kutokana na sababu zao mbali mbali ikiwemo ya kiuchumi, miundo mbinu, n.k hivyo kutokana na idadi ya wanachama wataokaoshiriki ndipo itakayoamua idadi ya timu za kuanzia raundi ya pili kwasababu inatakiwa zifike timu 32 itakazocheza raundi ya pili.

Hapo chini ni ratiba ya mashindano ya CAF ngazi ya vilabu kwa msimu wa 2022/2023

View attachment 2294183
kuna mtu bado hajaelewa mpaka hapa basi hata aje malaika kuelezea hataelewa kitu. Ahsante sana na usimba wangu nimeelewa vizuri
Mkuu kuna kitu kunaitwa association ranking (5 year ranking) halafu kuna club ranking (5 year ranking)

Association ranking ni mjumuisho wa alama zinazokusanywa na vilabu katika mashindano ya kimataifa ya champions league na confederation
kwenye association husika mfano Misri ina alama 183ambazo zimekuanywa kwa mjumusho wa timu zake zote zilizokusanywa ndani misimu mtano.

Association ranking ndio inayoamua nchi zibazoingiza timu nne kwenye michuano ya kimataifa kwasababu association 12 bora ndizo zitakazopata hiyo nafasi

Kuhusu club ranking
Ni point inayojikusanyia club kwa misimu mitano katika mashindano ya kimataifa.

Hakuna faida ya moja kwa moja kwa kuwa kwenye top 10 au top 12 bali kuna vipaumbele endapo ikitokea condition fulani mfano upungufu wa timu za kushiriki klabu bingwa.

Lakini ikitokea wanachama wote wa CAF wataleta timu zao hakutakuwa na faida kwa kuwa timu yenye nafasi ya juu kwenye rank, zaidi tu utasaidia association yako kupanda chat ili kuiwwzesha i maintain nafasi ya kuingiza timu mbili

Piga hesabu tu mfano memberr 50 wanashiriki katika klabu bingwa kati ya 54 maanake kutakuwa na jumla ya timu 62 hivyo imebakia timu mbili tu kufika 64 kama zinavyotakiwa kwenye hatua ya awali ambazo ni timu 64. Hivyo hapo ni timu mbili tu zitaanzia hatua ya pili. Ila ikitokea wanachama wameleta timu zinazofika 64 basi hakutakuwa na timu yoyote itakuanzia hatua ya pili bali timu zote 64 zitaanzia hatua ya awali kabisa

Update:

Mnao tarehe 9 mwezi huu wa nane, CAF wataendesha draw kwa ajili ya michezo ya hatua ya awali. Jumla ya wanachama 46 wamejitokeza kushiriki michuano ya kimataifa.

Hivyo kimahesabu ni kwamba kutakuwa na timu 58 zitakazoshiriki klabu bingwa kutoka mataifa 46 wanachama wa CAF. Yaani 46-12= 34
12x2= 24 hivyo jumla ya timu ni 34+24= 58

Kutokana na hesabu hiyo, ni timu sita pekee ndizo zilizopelea kufika timu 64 hivyo basi timu zote zitaanzia hatua ya awali isipokuwa timu sita bora tu kutoka kwenye 5 year CAF ranking ndio wataanzia hatua ya pili.

Hapa chini ni orodha ya vilabu na wanachama shiriki wa michuano ya kimataifa View attachment 2317575
 
Mkuu uko ndotoni au ? Geita gold anaenda shirikisho kwa kigezo Cha Costal union kupoteza kombe mbele ya Yanga (ASFc) ambapo Geita pia alikua nafasi ya nne upande was ligi kuu ........Sasa hapo endapo costal union angechukua kombe angeenda moja kwa moja shirikisho Alf Geita angebaki
Hakika... Uko sahihi kabisa...

Sent from my TECNO LA7 using JamiiForums mobile app
 
vip kuhusu Azam kuanzia hatua ya pili ni kigezo gani kimetumika mkuu?
Ishu ya Azam kiukweli namimi imenichanganya sijui ni kigezo kipi kimetumika
 
swali la nyongeza mheshimiwa spika,
ikitokea nchi zote wanachama 56 zikapeleka timu kwenye cafcl, ina maana baki kufikia 64 ni timu 8,
je namba itabadilika kutoka wanachama 12 wanaoingiza timu mbili mbili na kuwa 8 au itakuaje?...
Swali lako linajibu ndani yake. Ikitokea wanachama 56 zimepeleka timu, ni lazima idadi ya wanachama watakaoingiza timu mbili mbili zitapungua ili kubalance zipatikane timu 64.
 
Ishu ya Azam kiukweli namimi imenichanganya sijui ni kigezo kipi kimetumika
nadhani formula ni ile ile, japo kuna kitu caf wamekosea.....

kwenye CAFCC kuna timu 50, ambapo huku timu huwa zinaenda a three round robin ku-qualify kwenda group stage,......

sasa, tuchukulie hizo timu 50 ndio zipo, na timu 13 ndio zinaanzia hatua inayofuata.... it means 50-13=37 (tayar hii namba haigawiki kwa mbili, ndio kosa lilipo)......

sasa, tuassume scenario mbili hapa,

scenario ya kwanza, tu-assume wamekosea idadi ya timu zitakazoanzia hatua inayofuata, labda ni 14........

so lets say ni 14,
kwaio 50-14=36,
round ya awali itakua 36/2=18.....

round ya kwanza 18+14=32, i.e 32/2=16,

QF round itakua 16 +16(zilizotolewa CL) =32/2 =16 group stage!

so katika timu zenye ranking ya juu upande wa CC ina maana Azam imo kati hzo 14 (13 kama walivyosema wao caf), hata hivyo Azam hana points labda kapewa kwa sababu ya ushiriki wao.......
 
uzi makini sana huu.

haya mambo kuna mpaka viongozi na wasemaji wa timu kubwa hawayajui,kuna mmoja amesema kwa kinywa kipana kabisa timu yake itaanzia hatua inayofuata kwasababu ni bingwa wa ligi ya NBC alafu Simba itaanzia hatua ya awali.
mimi mpaka niliona aibu[emoji23][emoji23][emoji125][emoji125][emoji125]
Wewe umwmuona uyo tu daah ila watz sisi ni hatari kwa ustawi wa hii dunià asee
 
Kwa hali halisi nimayoina mwaka huu simba na yanga zinatoka mapema kabisa hata kwenye makundi hazisogei
 
Geita Gold ameingia kwenye shirikisho kwa kigezo kipi?
Mm nilifikiri Coastal Union ndio wenye nafasi ya pili Azam cup na kwa namna alivyopambana atacheza shirikisho barani Afrika.
kamuni hazimpi nafasi mshindi wa pili wa Azam FA Cup.Geita Gold Kawa wa nne Premier league ana sifa ya kuwakilisha
 
Mimi ni shabiki wa Simba, lakini huwa napenda watu wawe wanaelewa zaidi kuliko kukariri. Hakuna idadi kamili ya timu bora kuanzia raundi wa pili ya CAF CL. Hizo timu kumi zilikuwani kwa msimu uliopita, kila msimu idadi hupungua au huongezeka kulingana na idadi ya timu zote zilizothibitisha kushiriki. Kwa hiyo licha ya Simba kuwemo katika 10 bora ya washiriki wa CAF CL, inawezekana kabisa kwa msimu huu zikachukuliwa timu 7 au hata 12. Lengo la wapanga ratiba ni kwamba timuzichujane katika raundi ya awali lakini kwa namna yoyote round ya kwanza zibaki timu 32, ili makundi ziwepo timu 16. Sasa kwa kuwa idadi ya nchi na timu zinazothibitisha hubadilika mwaka hadi mwaka, hata timu zinazoanzia raundi ya awali idadi yake hubadilika. Kwa hiyonusishangae msimu huu Simba yumo katika 10 bora za washiriki lakini akaanzia raundi ya awali
[emoji122][emoji122][emoji122]
 
Kwan caf si walishatoa list ya timu kutoka kwenue kila nchi na kwenye hiyo yaarifa walisema timu ambazo ziliandikwa kwa bold zitaanzia raundi ya pili au hiyo taarifa ilikuwa ya nan?
 
Na kama timu zinazoshiriki ni 58 kama mmoja wa wachangiaji alivyosema then timu 6 tu ndizo zitasubiria second round

Yaani kimahesabi itakuwa hivi
58 - 6 = 52

Hao 52 watatoana na kubaki 26

Hao 26 wataenda kuungana na wale 6 kukamilisha timu 32 kwa ajili ya second round
Ova
 
Update

Siku ya jumatano, majira ya saa saba mchana kwa muda wa Africa Mashariki raisi wa CAF Dr Patrice Motsepe atazindua mashindano ya Super league. Uzinduzi huo utafanyika jijini Arusha.

Pia leo siku ya jumanne ya tarehe 9 kutafanyika draw ya michezo ya hatua ya awali. Draw hiyo itafanyika saa kumi kwa majira ya Misri ambayo ni sawa na saa kumi na moja kwa majira ya Africa Mashariki. Hivyo leo ndio siku ya kujua nani kapangiwa na nani, aidha michezo ya kwanza katika hatua hii inatarajiwa kuchezwa tarehe 9 -11 mwezi wa tisa huku marudiano yakiwa tarehe 16-18 mwezi wa tisa.

Tusubiri tuone timu zetu za Tanzania zitapangiwa na timu zipi
 
Back
Top Bottom