2024 usimfanyie mwanamke financial favour yoyote

2024 usimfanyie mwanamke financial favour yoyote

Haya sasa tushamaliza miezi 9 ya mwaka 2024, ma-simp wote nipeni mrejesho wanawake wote mliowaohonga wamewanufaisha nini kimaendeleo.
 
Pia hakukuona tu uko vizuri financially bali.pia aliona namna gani umemshobokea sana
Half american Bush Dokta Kelsea saa ingine hata mtu unakuwa hujamshobokea, kuna mdada mmoja mgeni alikuja ofisini kwetu kikazi, akaongea nasi, boss wetu akatusihi tubadilishane nae namba, so alichukua namba yangu, alichat na mm akiniuliza vitu vya kazi nikawa namjibu ipasavyo, tukaagana, nikafuta namba yake

Ikapita wiki 2 kimya, mara napigiwa simu mara kwa mara, mara sms nikiwa nashangaa nani huyu, akajitambulisha flani, nikakausha, mara simu mara sms mwishowe akaniomba laki 1, nikamwambia sitaki na siwezi kumpa hela.

Nlishangaa sana alivoniomba iyo hela, shida sio yeye kuniomba hela, Yani shida ni kwamba mm ni stranger kabisa kwake, sijamtongoza, sikuwa na mpango wa kumtongoza, sikumshobokea, kwanini aniombe hela,

It's insane, ni sawa mtu ujitokee uende ofisi za watu, ukamuombe hela mtu yoyote utaemkuta pale, ambae humjui, how is that possible 🫢🫢, nshawahi pitia nyakati ngumu kiuchumi ila sijawahi omba hela kwa stranger, huwa nawaomba ndugu na rafiki, sijui lakini, mpaka sasa najiuliza kama yule mdada alikuwa na akili timamu au hayajanikuta bado.
 
Back
Top Bottom