Pre GE2025 2025 Je, Watanzania wanahitaji Rais wa aina gani?

Pre GE2025 2025 Je, Watanzania wanahitaji Rais wa aina gani?

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Mungu yupi unamaanisha
Mungu wa usawa na haki, Mungu wa uhuru na amani, Mungu muumbaji mbingu na ardhi na vyote viijazavyo dunia. Mungu wa upendo, rehema na neema.

Mungu ambae wanaCCM wanamuomba na kumlilia na hatimae huwajibu kwa kushinda chaguzi, kushika dola, kuunda serikali, kuongeza nchi na kuwatumikia waTanzania.

Na kwa Neema na Baraka za Mungu CCM itashinda kwa kishindo kikuu uchaguzi mkuu 2025, na mgombea urasi wake akiwa ni Dr Samia Suluhu Hassan 🐒
 
Kumekuwa na nadharia nyingi sana kuelekea 2025 ndani ya chama 5 tena, kitaifa katiba ibadilishwe kuwe na tume huru ya uchaguzi tupate mtu kutoka nje ya mfumo wa CCM.

Nimekuwa nikizungumza na watu tofauti nakupata nini wanakiwaza kuanzia mam ntilie mpaka mtu wa juu kabisa kimaisha.

Niukweli usiopingika yakuwa wakati chama na chawa wengine tunatumia all resources we have pamoja ushawishi kwa jamii kusema miaka mitano tena watanzania ndani ya mioyo wana mawazo yao binafsi na sio haya tunayaweka kwenye vichwa vyao.

Mbaya zaidi kwa sababu wa Tz ndio wataalamu waunafiki dunia wote wamekuwa sehem ya nyimbo mitano tena ila moyoni wanamawazo tofauti.

Naomba wale wote tunapenda uongozi wa mwanamke au tungetamani kuona hilo likitokea kupitia uzi huu basi msinipige mawe au kukasirika ila chukueni kimtazamo chanya kwa kuboresha pale panaitaji uboreshaji na sio vinginenvyo.

Awali ya yote jambo nimeligunduwa kwa watu wengi na ningeomba usije niambia toa uthibitisho naimani kama kuna team ya siri undeni mchunguze sio kwa uchawa kwa kutaka ukweli mtakuja niambia.

Nikuweli mchungu kwa namna yeyote ile watanzania bado hawajawa na mtazamo chanya kuongozwa na jinsia nyingine ukiacha ile waliizoea tangu uhuru. Watanzania wengi bado wanatamani kuona Me akiwa kiongozi wakitaifa.

Watanzania pamoja na yote yamefanyika chini ya serikali ya sita ila bado hawana raha na wanafanya unafiki aka kupata mkate wao wakila siku ila moyoni wapo mbali sana na hawaja ielewa serikali ya sita sera zake. Una 3R ila bado wanaona yale waliyasahau hili tu ni doa.

Chama kitaweka mgombea Me na kikawa na ushawishi mzuri vs chama kitaweka ke na kikawa na ushawishi zaidi ya chama upinzania chama chenye me kinaweza fanya vizuri zaidi kuliko chama chenye mamlaka. Maana yake ni nini? Bado kama Taifa tuna safari ndefu kumuweka ke ktk nafasi kubwa ya kitaifa.

Chama kinaweza kutumia nguvu na ushawishi mpitisha ke ila dalili zinaonyesha 👋 tena itakuwa mizito sana mizito sana mgombea anaweza omba dunia isimame ashuke ila haitowezekana na kutokana na hiyo misukosuko inaweza leta shida kwa chama.

Hali ilivyo sasa sivyo itakavyo kuwa pindi jina litakuja ke kwa sasa watanzania wanauvumilivu wakiamini taifa lilikuwa kwa msiba na 2025 kutakuwa na badiliko ktk watu wengi nilio zungumza nao wanaonyesha kuwa na subira ila sio kwamba wanataka 👋 hata wandani hakunaga wanafiki.

Gharama za kampeni chini ya ke zitakuwa kubwa sana na bado hata kwa goli la mkono kazi itakuwa nzito..
Tutakapo toka kwa uchaguzi badala ya kuongoza From day one ndani ya chama tawala yatazuka makundi mazito kwa uchaguz wa 2030 nadhani haya yatamvuruga mwenyekiti yataleta wizi na kila aina ya shida kwa taifa na chama waweza jouliza why na ndio maana tunasema haya..

Wapo wazee na wakongwe ndani ya chama walisha yaona haya tangu siku JPM alipo lala na hata sasa yanatimia na kuzidi timia ndio maana mstaafu mmoja akasema ukitaka Nchi itulie zungumza na wazee nje ya box ushauri wa wazee tulipata msiba 👋 nihatari kwa chama kule kitaluni mgawanyiko utakuwa mkubwa sana hatutoweza tuliza kama tulivyo tuliza kipindi kile. Kwanini wa Tz wanafiki machoni kama watu moyoni hawana utu.

Siasa za dunia hazipo upande wa ke kungekuwa na nafuu kubwa kama USA ke angechukua nchi ila kwa sasa ni giza nene sana.

Haya ni mawazo ya watu pasipo weka majina na sio lazima kuyaamini unaweza soma nakuacha hapa kwa wakati mwafaka. Japo sio mbaya wazee wavishikio wakafanya check list kuthibitisha maelezo yangu.
Watanzania sio wanafki kama usemavyo na ili uamini hilo dora ijitenge na siasa ifanye majukumu yake ya kisheria na kikanuni kuwe na uwanja sawa wa kisiasa ndio utajuwa kama Watanzania sio wanafki kama usemavyo
 
Mungu wa usawa na haki, Mungu wa uhuru na amani, Mungu muumbaji mbingu na ardhi na vyote viijazavyo dunia. Mungu wa upendo, rehema na neema.

Mungu ambae wanaCCM wanamuomba na kumlilia na hatimae huwajibu kwa kushinda chaguzi, kushika dola, kuunda serikali, kuongeza nchi na kuwatumikia waTanzania.

Na kwa Neema na Baraka za Mungu CCM itashinda kwa kishindo kikuu uchaguzi mkuu 2025, na mgombea urasi wake akiwa ni Dr Samia Suluhu Hassan 🐒
Duh, ndo huyo wa haki na amani?
Anaetoa baraka za wanaCCM kuua na kuchinja kweupe, alieumba dhahabu, almas, tanzanite, na ardhi safi lakin akawanyima ufahamu wa kuvuna na kuzitumia kwa manufaa ya watanzania bali wachache kujinufaisha?

Mungu aliebariki roho mbaya za kikatili kwa watu wa CCM , akawapa ujasiri wa kuona maskin wa taifa lao kama vikaragosi, unamzungumzia Mungu yupi wew, au mungu aliewapa ujasiri watu waibe na kupora mali za maskini na kuzipeleka kwa wazee wa masinagogi kutoa harambee, ni yupi mungu wamzungumzia ...

Taifa linaangamia kwa kulea upumbavu.
 
Duh, ndo huyo wa haki na amani?
Anaetoa baraka za wanaCCM kuua na kuchinja kweupe, alieumba dhahabu, almas, tanzanite, na ardhi safi lakin akawanyima ufahamu wa kuvuna na kuzitumia kwa manufaa ya watanzania bali wachache kujinufaisha?

Mungu aliebariki roho mbaya za kikatili kwa watu wa CCM , akawapa ujasiri wa kuona maskin wa taifa lao kama vikaragosi, unamzungumzia Mungu yupi wew, au mungu aliewapa ujasiri watu waibe na kupora mali za maskini na kuzipeleka kwa wazee wa masinagogi kutoa harambee, ni yupi mungu wamzungumzia ...

Taifa linaangamia kwa kulea upumbavu.
Gentleman,
chuki binafsi, dhana na Imani potofu ilojaa moyoni mwako ni mali yako binafsi, hakuna wa kuhangaika au kubabaika nayo.

Kama Taifa,
chini ya serikali sikivu ya CCM, tutaendelea kuilinda Amani ya waTanzania wato kwa nguvu zote na kwa gharama yoyote ile.

Ukimendea wake za watu na kutolewa mangeu huna haja ya kusingizia utekaji, acha tamaa na vitu vya watu 🐒
 
Maisha yanakatisha tamaa kwa kweli.

Hakuna mtu ambaye hapendi kuongozwa na mwanamke endapo uongozi wake utakuwa mzuri na Wala hakuna mtz anayeweza hofu Hilo coz kwanza Ni sifa kubwa.

Watanzania wanachukizwa zaidi na kiongozi ambaye kwanza anawanyima watu uhuru wa mawazo yao tofauti ambayo kimsingi ndio chachu na kianzilishi Cha maendeleo ya nchi kwa ujumla. Imefika hatua mbaya Sana kwa Sasa kiukweli , mtanzania amebanwa kila angle ya mawazo mbaya zaidi kwa kuwa wajinga ndio asilimia kubwa nchini basi namba hiyo hutumiwa kuwa nyenzo yakulazimisha wachache Hawa wenye Nia ya dhati kutumbukia kwenye mchezo wao.
Nafkiri kiongozi makini Ni Kama mpira wa miguu uwanjani. Mchezaji mzuri anaonekana mapema tu, Wala haihitaji matangazo meeengi. Na kufosi kukubalika. Hali Ni Tata. Yaani viongozi wa Leo sio tu kwamba wananchi hawapendi hasha! Bali hata maisha hayapendi. Nivile tu haijakaribia hali ya usyria.
 
Rais Mwanaume mwenye hofu ya Mungu na anayekerwa na rushwa na ufisadi kutoka moyoni.
 
Back
Top Bottom