Pre GE2025 2025 ni ushindi wa kishindo kwa Rais Samia

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Hivi kwa akili zako, hizo hizo zinazokutosha, ushindi wa kishindo unapatilanaje bila tume huru!
 
Kwahiyo kusiwe na uchaguzi kabisaa kama imeshajulikana atashinda kwa kishindo, Duh! nimejaribu kufikiria mara 100 sijaelewa kabisa.
 
Kwanza, Mungu yupo upande wako kwa kazi nzuri unazo wanyanyia waja wake.

Pili, watanzania wote wenye mapenzi mema wanakuunga mkono umewaonyesha njia.

Tatu, wanawake ni jeshi kubwa wameamua na kuridhia uwe Esther/Hadija wao kwa kizazi hiki, uwakomboe kwenye makucha ya mfumo dume uliotaka kuota mizizi nchini.

Nne, Dola iko mikononi mwake kila aliye madarakani ni kwa ridhaa yake na dola ina imani na yeye labda aamue kuachia dola kwa hiari yake mwenyewe.

Tano, Ccm ni chama kubwa, chama kongwe linalo kubalika Tanzania, Afrika na duniani lenye mbinu zaidi ya 1000 yeye ni m/kiti wake je? Kipi kitashindikana?

Sita, Hakuna upinzani Tanzanian bali kuna watoa taarifa wasio na ushawishi na wasio na agenda zaidi ya ubwabwa na kulia kupigwa risasi za mablankoo, tena wao wenyewe ili kuichafua serikali.

Kwa kweli ninauona ushindi mnono kwa huyu mama yetu mpendwa hakuna wa kumzuia kuingia ikulu 2025.
Wale manabii wa uongo na mapastor feki wanaoendelea kujitabiria viunabii vyao uchwara kwamba Ccm itagawanyika tuwapuuze.

Nb. Maandiko yanasema ombeni nanyi mtapewa, bisheni nanyi mtafunguliwa.

Nami ninakuomba mama unikimbuke kwenye ufalme wako ujao.

Nitakusaidia kufanya kazi za watanzania kwa uzalendo hekima, utu na weledi.

Kwa Africa, hasa Africa mashariki uwez kuwa Rais then ukakosa kushinda mhula mwingine never haiwezekani

So hata kama mama Samia angefanya Maisha kuwa magumu sanaaaaaa still 2025 angeshinda

Hata bila kampen atashinda tena Kwa 95%
 
Kwa hiyo hakuna haja ya wananchi kupiga kura?
Wananchi kupiga kura ni haki yao kumchagua wanayemtaka na ndio maana hata vyama pinzani vinapoweka wagombea wao huwa wanakubaliwa na dola na kuachwa wagombea hivyo sanduku la kura ndio hutoa majibu kati ya wagombea wote waliokubaliwa na dola ni yupi ambaye wananchi wamemchagua
 
Kwani tume huru ni ile mnayoitaka nyingi chadema tu? Nchi ina vyama zaidi ya kumi na kitu vyama vingine havihitaji tume huru isipokuwa nyinyi chadema au mnataka iitwe tume huru ya chadema ya taifa ya uchaguzi? Yaani Mbowe awe mwenyekiti, kisu awe mkurugenzi na heche, mnyika, Pambalu na msigwa wawe wajumbe ?
 
Uchaguzi ni lazima kushinda kwa kishindo ni kwa kufanya tathmini ya mambo muhimu aliyoyafanya watanzania na kulinganisha na watoa taarifa ambao hawana agenda ya kuwavutia wananchi
 
Wananchi kupiga kura ni haki yao kumchagua wanayemtaka na ndio maana hata vyama pinzani vinapoweka wagombea wao huwa wanakubaliwa na dola na kuachwa wagombea hivyo sanduku la kura ndio hutoa majibu kati ya wagombea wote waliokubaliwa na dola ni yupi ambaye wananchi wamemchagua
Hii sasa ni porojo kwa sababu mwanzo umesema hakuna anayeshinda bila dola kukubali..
nchi hii hauwezi kushinda bila kukubaliwa na dola
Kwa maana hii wananchi wanapoteza muda kwenda kupiga kura, na upotevu wa pesa za walipa kodi maskini kugharamia mchakato wa uchaguzi
 
Kwanza, Mungu yupo upande wako kwa kazi nzuri unazo wanyanyia waja wake.

Pili, watanzania wote wenye mapenzi mema wanakuunga mkono umewaonyesha njia.

Tatu, wanawake ni jeshi kubwa wameamua na kuridhia uwe Esther/Hadija wao kwa kizazi hiki, uwakomboe kwenye makucha ya mfumo dume uliotaka kuota mizizi nchini.

Nne, Dola iko mikononi mwake kila aliye madarakani ni kwa ridhaa yake na dola ina imani na yeye labda aamue kuachia dola kwa hiari yake mwenyewe.

Tano, Ccm ni chama kubwa, chama kongwe linalo kubalika Tanzania, Afrika na duniani lenye mbinu zaidi ya 1000 yeye ni m/kiti wake je? Kipi kitashindikana?

Sita, Hakuna upinzani Tanzanian bali kuna watoa taarifa wasio na ushawishi na wasio na agenda zaidi ya ubwabwa na kulia kupigwa risasi za mablankoo, tena wao wenyewe ili kuichafua serikali.

Kwa kweli ninauona ushindi mnono kwa huyu mama yetu mpendwa hakuna wa kumzuia kuingia ikulu 2025.
Wale manabii wa uongo na mapastor feki wanaoendelea kujitabiria viunabii vyao uchwara kwamba Ccm itagawanyika tuwapuuze.

Nb. Maandiko yanasema ombeni nanyi mtapewa, bisheni nanyi mtafunguliwa.

Nami ninakuomba mama unikimbuke kwenye ufalme wako ujao.

Nitakusaidia kufanya kazi za watanzania kwa uzalendo hekima, utu na weledi.
Unaitwa Fukua ,kikwetu Fukua ni panya naona unaelekea kwenye upanya Hv sasa naamini majina ya watu huonesha jinsi walivyo.
 
Back
Top Bottom