Pre GE2025 2025 tunahitaji mdahalo wa wagombea Urais kama ilivyofanyika kwa TLS. Unawaweka wagombea kwa uhalisia wao, hakuna longolongo

Pre GE2025 2025 tunahitaji mdahalo wa wagombea Urais kama ilivyofanyika kwa TLS. Unawaweka wagombea kwa uhalisia wao, hakuna longolongo

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Wakuu,

Mwakani wagombea Urais wanatakiwa kufanyiwa mdahalo kama huu ulioendesha leo na Star Tv.

Kupitia mdahalo huo unaona kabisa huyu anafaa huyu amejaa pumba, na wengine wapo kwaajili ya kujaza nafasi tu.

Hii itasaidia wananchi kufanya maamuzi sahihi na kutodanganyika na doti za kanga au kofia za vyama.

Au nasema uongo chawa na nyuki wa mama?
Ccm kama kawaida yao watakimbia
 
..Kikeke na Odemba hawana ujasiri wa kuuliza viongozi wa Ccm maswali magumu. Wanafurukuta huku kwa wapinzani tu.
Umewahi kushuhudia Odemba akihoji Viongozi w Serkali kama Msemaji mkuu wa serkali,Gambo,Makamu wa Rais wa Zanzibar na wengine wa Serkali kama mawaziri na wakuu wa Mikoa na wilaya nitajie Interview Odema aliyoshindwa kuuliza Maswali
 
..umeona interview aliyofanyiwa Rais Ruto na wale waandishi wa watatu?

..Tangu kuumbwa kwa Tanganyika umewahi kuona waandishi wa Kitanganyika walio informed, na wanaojiamini namna ile?
 
Wakuu,

Mwakani wagombea Urais wanatakiwa kufanyiwa mdahalo kama huu ulioendesha leo na Star Tv.

Kupitia mdahalo huo unaona kabisa huyu anafaa huyu amejaa pumba, na wengine wapo kwaajili ya kujaza nafasi tu.

Hii itasaidia wananchi kufanya maamuzi sahihi na kutodanganyika na doti za kanga au kofia za vyama.

Au nasema uongo chawa na nyuki wa mama?
ccm walipompata BW Mkapa mwenye uwezo binafsi waliutaka mdahalo. Baada ya hapo wamekuwa wakwepaji!
 
Kwa nini ccm huwa hawataki midahalo?
Huwa wanaangalia na uwezo wa mgombea wao, wakiona ni kilaza hiyo midahalo huwa hawataki hata kuisikia...lakini mgombea akiwa vizuri wanakubali, mfano enzi za Mkapa walikubali midahalo
 
Au nasema uongo chawa na nyuki wa mama?

Ni kweli, mdahalo tena iwe ina round kama 3 hivi ili sije tukadhani tumeuziwa mbuzi ndani ya gunia kumbe siyo.

Kongole kwa StarTv Medani Kuu chini ya chief Odemba kwa kuendesha modeli ya mdahalo mzuri kama wa jana wa wagombea urais TLS .
 
Ufanyike tu, hata Samia akikimbia, wengine wafanye, Raia watajua Rais kakimbia mdahalo
 
Hali ni mbaya, mchakato kuelekea uchaguzi wa 2024 na 2025 una hujumiwa kwa makusudi kwa faida ya chama tawala.

Kama vile kamati ya uchaguzi ya TLS ilivyofanya njama za kumuengua Boniface Mwabukusi, bila watu kupaza sauti na kwenda mahakamani leo asingekuwepo ktk mchakato wa kugombea TLS

Je midahalo ya kupima uwezo wa Tume Huru Ya Uchaguzi inafaa ifanyike sasa ili kupima utayari wa Tume kuweza kusimamia mchakato mzima. Bila hivyo midahalo ya wagombea wa nafasi mbali mbali itakuwa haina maana kidemokrasia

Mfano :
27 Julai 2024
ZItto Kabwe: Tume Huru Haikujiandaa Kuandikisha Wapiga Kura

View: https://m.youtube.com/watch?v=W4ZY4Gp5CSk

Mkoa wa Kigoma wananchi walijitokeza kwenda kujiandikisha lakini kadi zimekwisha hivyo wananchi wengi wamekosa haki ya kujiandikisha. Hii ni hujuma dhidi ya mchakato mzima wa uchaguzi umeanza amesema Zitto Kabwe....
 
..umeona interview aliyofanyiwa Rais Ruto na wale waandishi wa watatu?

..Tangu kuumbwa kwa Tanganyika umewahi kuona waandishi wa Kitanganyika walio informed, na wanaojiamini namna ile?
Tatizo unafananisha Nchi Yenye katiba Nzuri na nchi ambayo bado katiba yake inahitaji Marekebisho
 
Midahalo ni mbwembwe na kuiga demokrasia za magharibi.

JPM hakutaka mdahalo na hakuwa na staha ya kuweza kuushiriki lakini kwa miaka 5 aliyoiongoza TZ kafanya mengi sana. SSH aliyerithi nafasi yake anafanya kazi kubwa sana huko mikoani na hahitaji midahalo.

Watu wa mijini haswa wa humu mitandaoni wanaona midahalo ina faida lakini huko vijijini unakopelekwa umeme kila kukicha hawana kabisa uhitaji wa kuiona midahalo.

Lissu anaweza sana kujenga hoja, lakini sidhani kuwa ufanisi wake wa kazi unaweza kupimwa kwa kingereza chake na majivuno ya kuongea mbele ya kipaza sauti.
 
Nashauri kusiwepo na midahalo Kwa wagombea! Kwa sababu nchi itapata aibu Kwa wagombea hao. La pili, Kwa sasa hatuna wenye uwezo wa kuuliza maswali yenye tija Kwa wagombea, hatuna!
 
Wakuu,

Mwakani wagombea Urais wanatakiwa kufanyiwa mdahalo kama huu ulioendesha leo na Star Tv.

Kupitia mdahalo huo unaona kabisa huyu anafaa huyu amejaa pumba, na wengine wapo kwaajili ya kujaza nafasi tu.

Hii itasaidia wananchi kufanya maamuzi sahihi na kutodanganyika na doti za kanga au kofia za vyama.

Au nasema uongo chawa na nyuki wa mama?
Chama chetu huwa kiaweka mpira kwapani
 
Back
Top Bottom