2025 watafanya waliyoyafanya mwaka huu wa 2020, kisha watesema uchaguzi umwikisha tufanye maridhiano

2025 watafanya waliyoyafanya mwaka huu wa 2020, kisha watesema uchaguzi umwikisha tufanye maridhiano

Salary Slip

Platinum Member
Joined
Apr 3, 2012
Posts
52,828
Reaction score
165,667
Hiki kinachoitwa maridhiano kati ya CCM na ACT, ni geresha tu, na hapa CCM wana-buy time lengo likiwa ni kujipanga kwa 2025.

Binafs naona haya ni maridhiano baina ya wanasiasa juu ya namna gani watagawana keki ya taifa na si maridhiano kwa faida ya Wazanzibar unless wanatuambia wamekubaliana nini juu ya madai ya msingi ya Wazanzibar,madai ambayo yakitekelezwa,basi yaliyotokea mwaka huu na katika miaka iliyopita, hayatajirudia tena.

Nachokiona hapa ni viongozi wa ACT kuwageuka wananchi wao huku wakijua 2025 hakuna kitachobadilika bali yatajirudia ya mwaka huu kama ilivyokuwa katika miaka iliyopita.

Pia,natarajia Maalim Seif ndani ya hii miaka mitano kutangaza kutogombea tena urais wa Zanzibar, na hivyo kipindi hiki ni cha yeye kutengeneza mafao manono ya kutaafu akiwa kama Makama wa Raisi.

Kinachofuata ni kumwandaa Maalim Seif mwingine kwa ajilii ya 2025 ambae nae atajifanya ana misimamo kama Maalim Seif ila mwisho wa siku atakuja kufanya alichofanya Maalim Seif na viongozi wenzake wa ACT mwaka huu wa 2020.

Kwahiyo, 2025 mtarajie yale yaliyojiri mwaka huu huko Zanzibari kujirudia ambapo CCM wataitinisha mchezo kwa kuleta hoja ya maridhiano na ACT, na kama ACT itaendelea kuwa na nguvu Zanzibar, wataafika maridhiano hayo- business as usual.

ACT kwa sasa ni pacha wa CUF huku CCM akiwa ndio mzazi wa hawa identical twins.
 
Katiba ya Zanzibar inataka uwepo wa serikali ya umoja wa kitaifa.
Hata hivyo, chama kushiriki katika serikali haina maana ya kuacha itikadi yake au msimamo wake.
Ushiriki huo waweza kutumia kama jukwaa la kuendeleza mapambano kwa ufanisi zaidi.
 
Ni kweli, Katiba ya Zanzibar inataka SUK.
Lakini Katiba vilevile inasema Mamlaka huwekwa na Wananchi.
Jee, katika hili kauli/chagua la wananchi limeheshimiwa?

Nadhani SUK inayozungumzwa na Katiba ni Ile ambayo mshindi ameshinda kwa HAKI na aliepata kura zaidi ya 10% nae ameipata kwa HAKI.
Hapo sasa vyama hivyo viwili vinakaa na kutimiza takwa hilo la Katiba la SUK.

Takwa la msingi hapa ni uchaguzi wa huru na haki na chaguo la Wananchi kuheshimiwa.

Ni vizuri kuitii Katiba yetu kwa ukamilifu wake na sio kuchukua baadhi tu katika yale tuyapendayo.

Kwa uelewa wangu mdogo nadhani hivyo ndivyo itakiwavyo - vinginevyo tuelimishane- yawezekana sisi wengine uelewa wetu ni mdogo.
Shukran.
 
Upinzani umeshindwa kuongozi kwa sababu ya kutanguliza matumbo yao makubwa mbele.

Wanasiasa siyo wa kuamini tena milele.

Kama CCM watasimamia haki waendelee tu hao hao. Wapinzani walishaonyesha rangi zao hatuwaamini tena, Period!!
 
Katiba ya Zanzibar inataka uwepo wa serikali ya umoja wa kitaifa.
Hata hivyo, chama kushiriki katika serikali haina maana ya kuacha itikadi yake au msimamo wake.
Ushiriki huo waweza kutumia kama jukwaa la kuendeleza mapambano kwa ufanisi zaidi.

Ukishaingia serikalini unaambiwa utumikie wananchi, na sio mapambano.
 
Upinzani umeshindwa kuongozi kwa sababu ya kutanguliza matumbo yao makubwa mbele.

Wanasiasa siyo wa kuamini tena milele.

Kama CCM watasimamia haki waendelee tu hao hao. Wapinzani walishaonyesha rangi zao hatuwaamini tena, Period!!

Unajicontradict, unasema wanasiasa sio wa kuwaamini, lakini unataka ccm waendelee tu, hao ccm sio wanasiasa?
 
Salary Slip unachosema ni kweli kabisa, kwani hakuna maridhiano yoyote yanayofikiwa bila kuwepo na 'Muswada wa maridhiano' kilichofanyika hapa ni punda afe mzigo ufike.
 
Ccm imegundua shida ya wapinzani ni vyeo na Sio kubadilisha Maisha ya wananchi kisera.Ndo maana wanawaibia kura zao, Kisha wakilalama wanawaambia wafanye maridhiano na wapewe vyeo.matokeo yake wananchi wanakonda, viongozi wananenepa.
 
Unajicontradict, unasema wanasiasa sio wa kuwaamini, lakini unataka ccm waendelee tu, hao ccm sio wanasiasa?

Afadhali hawa ambao wanaongoza tumeshawajua, kuliko hawa wanatuambia andamananeni then kesho unamkuta kwa mfalme anakula vinono,

Kutumiwa kama toilet paper kama daraja la mtu kwenda juu siyo!

Sikatai wapo wenye nia halisi ya ndani kabisa ya kukomboa Tanzaniai.e Tundu Lissu, ila ni wachache sana kiasi kwamba unafiki wa wengi umewaharibia.
 
Maridhiano kila bada ya uchaguzi; mshindwa ni yule yule na mlalamikaji ni yule yule! Kile walichoridhiana kiwekwe hadharani ili mwisho tupime kama hicho walichoridhiana kimetekeleawa au la!
 
Back
Top Bottom