2026 hapa bongo patakuwa na wachezaji wanalipwa milioni 50 kila mwezi

Mtemi Eno

Member
Joined
Jul 10, 2023
Posts
37
Reaction score
148
Makampuni mengi kwa sasa idara ya masoko hawabezi fact kwamba hizi timu zina wafuasi wengi kuzidi vyama vya siasa na huunganisha watu pamoja hata kwenye tofauti za kidini ama siasa.

Makampuni tunayaona kwa sasa yanataka ukaribu kwa namna yoyote na hizi timu, si ya hapa kwetu tu bali hata nje wamejua kwamba hizi timu zina impact kubwa kwenye soko la Tanzania.

Mambo yanazidi kuwa makubwa, timu zinapata pesa za endorsements, kufikia 2026/2027 si ajabu timu zikawa zinaingiza bilioni 10 pekee masuala ya endorsements na sponsorships pekee.

Kwa misuli hii ya pesa tutegemee 2026/27 wachezaji wakulipwa milioni 50 wataletwa hapa bongo.
 
Nakubaliana na wewe muhimu waendelee kujibeand zaidi na zaidi kwa sasa kilichobaki ni kumpata mdhamini mkuu wa ligi atakaeweka pesa nzuri haiwezekani pesa za bonus ziwe nyingi kuliko pesa za mshindi wa kwanza zinazotoka kwa mdhamini mkuu.

Pili CCM ndio wanatuchelewesha kwenye maendeleo ya soka viwanja hawataki kuviendeleza wamevikumbatia tu ingependeza virudishwe serikalini bajeti itengwe vifanyiwe ukarabati hapo ndipo tutafurahia soka.
 
Kabisa upo sahihi huo ndio ukweli,wachezaji wa nje huko wanabeba mpunga mrefu wanasepa wachezaji wa ndani awathaminiwi sana kwenye malipo.
 
Makampuni mengi kwa sasa idara ya masoko hawabezi fact kwamba hizi timu zina wafuasi wengi kuzidi vyama vya siasa na huunganisha watu pamoja hata kwenye tofauti za kidini ama siasa.

Makampuni tunayaona kwa sasa yanataka ukaribu kwa namna yoyote na hizi timu, si ya hapa kwetu tu bali hata nje wamejua kwamba hizi timu zina impact kubwa kwenye soko la Tanzania.

Mambo yanazidi kuwa makubwa, timu zinapata pesa za endorsements, kufikia 2026/2027 si ajabu timu zikawa zinaingiza bilioni 10 pekee masuala ya endorsements na sponsorships pekee.

Kwa misuli hii ya pesa tutegemee 2026/27 wachezaji wakulipwa milioni 50 wataletwa hapa bongo.
Uto nao wajaribu kukibrand Basi siyo kujifungia Hilo mji mwema tu.
 
Back
Top Bottom