24Hrs Season 4:Nimeshindwa kuielewa baadhi ya episode msaada tafadhari..

24Hrs Season 4:Nimeshindwa kuielewa baadhi ya episode msaada tafadhari..

David Palmer na jack bauer wana historia ndefu tangu season 1, jack aliokoaga maisha ya palmer, kimsingi ni zaidi ya marafiki. Baada ya rais wa season 4 kudunguliwa akiwa kwenye airforce 1 na gaidi Habib Marwan na kushindwa kuendelea na majukumu yake, mzee wa maboko Charles Logan aliekua vice president akaapishwa kua rais. Ila Logan na Jack hawana historia nzuri sana na mahusiano yao kwa ujumla hayako poa. Kuna sehemu kuna jamaa mmoja aliekua associated na terrorists alikua anashkiliwa ctu, na baada ya jamaa wa ctu kushindwa kupata info toka kwa jamaa, jack akaenda kinyume na direct order ya logan, akamtorture jamaa mpaka akapata alichokua anakitaka. Logan ndo alipotoa arrest warrant ya bauer, wakati huo jack akiwa kwenye operation ya kumkamata marwan pale club. Baada ya watu wa logan kuonekana na walinzi wa marwan na jamaa kufanikiwa kutoroka mahusiano ya logan na jack yakazidi kuingia dosari, na logan ikaonekana kama hana uzoefu wa kuhandle crisis za kigaidi, ndipo mike novic chief of staffs aliposhauri aletwe david palmer kusimamia show coz ana uzoefu na mikikimikiki ya magaidi toka seasons za nyuma

Umeelezea vizuri sana.
 
Unanikumbusha season yangu ya mwisho kuifatilia Lost...niliacha pale kisiwa kilipopoteaga...halafu kuna movie nyingine director anatakiwa awe anapimwa mkojo kila scene...mfano Dead of Thieves...mbwembwe nyingi action ya moja tu tena ni risasi zinalia weweee...
 
Da'Vinci kusema kweli 24 niliziangalia nazani 2012 au 2014 nilishazisahau!!... ngoja nirudie kuicheki hiyo episode nitarudi!..
Lakin Habib Maruan ndio aliyekuwa anawapa tabu zaidi naona
 
Back
Top Bottom