A better place to be with kenya, ama nchi gani? Nyinyi mlivyo na wivu, roho mbaya, mnafunga mipaka na kufubaza biashara, alafu unasema is a good place to invest. EA tungekuwa mbali zaidi ya hapo isipokuwa nyinyi ndo hurdle!
Yaani jamaa kaleta topic nzuri kwa roho safi kabisa lakini comment ya kwanza ni wewe mnafik alafu unatuita sisi ndo wenye roho mbaya, Kama ungekua na roho nzuri, topic kama hii ungechangia vizuri manake huyo
Yosef Festo katuunganisha sisi sote kama East Africa VS West Africa..
Alafu kukujibu hoja yako, siku zote nchi ambayo ina uchumi mdogo ndo inazulia nchi yenye uchumi mkubwa kwenda mbali zaidi, Hata ukiangalia nchi kama South Africa, inaangushwa na majirani, Kama majirani wake wangekua matajiri, kungekua na competition na pia nchi zengine zingekua na uwezo mkubwa wa kununua bidhaa za SA... SA ingekua ilifikisha 2 Trilllion dollars by now badala ya kukwama kwa $350Billion kwa karibu miaka 10 sasa.
Vile vile hapa EAC, kama Tanzania, Uganda wangekua na uchumi wa maana, kungekua na opportunity nyingi sana za kufanya biashara manake watu wangekua na uwezo wa kununua bidhaa kwahivyo makampuni yangekua yanajengwa kila mahali, pia kungekua na competition kali hakuna nchi ingetaka kuachwa nyuma... lakini vile hali ilivyo Kenya imekua ikiongoza kiuchumi kwa mda mrefu hadi tumejisahau tunakua wavivu na wazembe manake hakuna jirani yeyote anayetutishia kiuchumi sasa inakua hata sisi wenyewe hatujishughulishi manake tuko comfortable pale tulipo, lakini tungekua na kajirani flani ambako kamefanana na South Korea vile, tungejikaza tusiachwe nyuma angalau tuwafikie hali yao ya kiuchumi!
Leo hii kutokee maabara flani hapo Tanzania wagundue tiba ya corona, Kesho utasikia wakenya wakilalamikia serekali yao mitandaoni wakiuliza mbona Kenya haina maabara kama hio nayo ifanye uzinduzi wa maana, Hio haitakua eti tuna wivu na hio maabara ya Tanzania, ni katika ile hali ya competition, na ushindani wa kiuchumi,technolojia,sayansi kama huo ndo hufanya nchi zikaendelea kiharaka... Sio kama sasa ambapo majirani hamtutishii kwa lolote kwahivyo pia sisi hata hatujishughulishi.....