36 wajitokeza kuuza figo Hospitali ya Taifa Muhimbili

36 wajitokeza kuuza figo Hospitali ya Taifa Muhimbili

Kwani hakuna utaratibu wa kusaini kusaidia wenye shida na viungo pindi unapofariki wanatoa wanachohitaji?

Kwa kweli unakuta mtu anauza kwa mfano halafu baada ya miaka miwili anaishiwa hela
Anachanganyikiwa anaenda tena kuuliza kama wananunua na Kende auze
Huyo ni mjinga.
 
Hospitali ya Taifa Muhimbili imetoa ripoti ya takwimu zinazoonesha kupokea maombi ya wananchi 36 walioomba utaratibu wa kuuza figo zao ili kukabiliana na ugumu wa maisha.

Takwimu hiyo imetolewa jana wakati wa maadhimisho ya siku ya kukabiliana na ugonjwa wa Figo duniani.

Awali, Ofisa Ustawi wa Jamii kutoka kitengo cha figo Muhimbili, Halid Mahenga alinukuliwa hivi karibuni akisema kuwa kati ya Januari hadi Februari, watu sita walikwenda hospitalini hapo wakiulizia utaratibu wa kuuza figo zao.

Aidha, Mahenga katika taarifa yake kwa umma, alisema kati ya mwaka 2019 na 2020 idara yake ilipokea maombi ya watu watatu waliohitaji kupewa utaratibu wa kuuza figo zao, huku mwaka 2021 wakipokea watu wengine 27 ambao baadhi yao wamedai chanzo kuwa ni ugumu wa maisha.

Hata hivyo, ameeleza kuwa wakati serikali ikiendelea kufanyia kazi maandalizi ya sheria ya upandikizaji wa viungo, hospitali hiyo kwa sasa inaendelea kuzingatia misingi yote ya maadili kitaaluma katika upandikizaji wa figo.

“Ni muhimu watu wakatambua kwamba ni makosa kisheria, mgonjwa akihitaji upandikizaji hospitali itazingatia kanuni zinazohitajika kwa mtu anayetakiwa kuchangia figo kwa mgonjwa mwenye uhusiano wa damu” Alisema Mahenga

Hospitali ya Muhimbili tayari imepandikiza figo kwa wagonjwa 68 tangu kuanza kwa huduma hiyo nchini mwaka 2017, huku wagonjwa 110 hadi 120 wakipewa huduma ya usafishaji figo kila siku hospitalini hapo
View attachment 2146838
Chanzo. https://www.tanzaniaweb.com/TanzaniaHomePage/health/Muhimbili-Watu-36-walijitokeza-kutoa-figo-601085
Hii inawezekana ikawa ni fursa ya kibiashara.
 
Haya mambo unaweza kudhani ni utani ila kama watu wanafikia hali hiyo ni hatari sana. Wanaweza wakaibuka watu wakatumia fursa hiyo wakawa wanazinunua illegally na yakawa majanga. Mmemsikia binti wa Uganda aliyeenda Uarabuni kufanya kazi za ndani karudishwa hana figo na haongei wala kutembea.
 
Katika moja ya vitu alivyofanya Jakaya ni kuandaa mazingira,misingi na kuboresha upatikanaji wa huduma za afya na matibabu ambazo tulikuwa zinapatika nchi za Asia na Ulaya hapo Hospitali ya Muhimbili. Tutakukumbuka Sana Mzee wetu.
Umeamua kusifia kwenye hakuna
Sasa huo si ndio wajibu wa serikali? Hapo ni sawa na kumsifia ng'ombe kula majani
 
Tumefikia huku aisee..shida hizi mhh
 
Mimi siyo figo moja tu, niko tayari kuziuza zote 2 nilizonazo. Haya maisha yanazingua sana.

Kama nitakosa connection ya kwenda Ukraine ndani ya wiki ijayo, kituo kitakachofuata ni hapo Muhimbili.
Ungeuza na moyo kabisa mkuu.

Ili upige mshindo wa nguvu,

Utanuwe maisha.
 
Katika moja ya vitu alivyofanya Jakaya ni kuandaa mazingira,misingi na kuboresha upatikanaji wa huduma za afya na matibabu ambazo tulikuwa zinapatika nchi za Asia na Ulaya hapo Hospitali ya Muhimbili. Tutakukumbuka Sana Mzee wetu.
Ongezea na hospital ya kisasa kabisa ya magonjwa ya MOYO (JKHI)
 
Umeamua kusifia kwenye hakuna
Sasa huo si ndio wajibu wa serikali? Hapo ni sawa na kumsifia ng'ombe kula majani
Ulitaka nimsifie nani? Mbowe au marehemu? Kusifia ni sehemu ya motisha kwa waliopo madarakani lakini pia ni faraja kwa waliostaafu. Wangapi wamepita hawakufanya?
 
Ni kwl mkuu ,

Lakini sio ya kuuza kiungo chako cha mwili..
Tumechagua kujiajiri kwa kuuza viungo vyetu. Kule kwenye Government, NGOs na agencies nyinginezo hatupi ajira. Mitaji ya kujiajiri hatuna. Watoto wao ambao wana access ya mitaji (eg. the Mwinyi family) wala hawajiajiri zaidi ya kupata ulaji mnono kule Zenji na Bara.TUTAIPATA MITAJI KWA KUUZA FIGO.
 
Back
Top Bottom