37 waenda jela Kilimanjaro baada ya kutiwa hatiani kwa makosa mbali mbali yakiwamo ya ulawiti,dawa za kulevya

37 waenda jela Kilimanjaro baada ya kutiwa hatiani kwa makosa mbali mbali yakiwamo ya ulawiti,dawa za kulevya

Ndagullachrles

JF-Expert Member
Joined
Jun 20, 2023
Posts
256
Reaction score
259
Watuhumiwa 37 wa makosa mbali mbali wamehukumiwa kwenda jela baada ya kupatikana na hatia mkoani Kilimanjaro .

Katika Mashauri hayo limo la mtuhumiwa kuhukumiwa adhabu ya kifungo cha maisha jela kutokana na makosa dhidi ya binadamu.

Taarfa iliyotolewa na jeshi la polisi mkoani kilimanjaro kupitia kamanda wake (SACP),Simon Maigwa inaeleza kuwa kati ya Kesi hizo zipo kesi sita za watuhumiwa wa ulawiti ambazo zilsikilizwa na kutolewa uamuzi ambako Jamhuri ilipata ushindi katika kesi hizo.

Watuhumiwa watatu katika kesi tatu walihukumiwa kifungo cha maisha jela kwa kosa la kulawiti katika Mahakama ya hakimu mkazi Moshi.

Mtuhumiwa mmoja alihukumiwa kifungo cha miaka 30 jela katika Mahakama ya Wilaya ya Same, huku watuhumiwa wengine wawili wakihukumiwa vifungo vya chini ya miaka 30 jela katika Mahakama ya hakimu mkazi Moshi.

Katika kesi moja ya kubaka, mtuhumiwa mmoja alihukumiwa kifungo cha miaka 30 jela katika Mahakama ya Wilaya ya Siha.

Katika kesi nyingine ya kuzini na maharimu (ndugu wa damu), mtuhumiwa mmoja alihukumiwa kifungo cha miaka 30 jela na Mahakama ya Wilaya ya Same.

Aidha, mtuhumiwa mmoja aliyekutwa na hatia ya kupatikana na silaha amehukumiwa kifungo cha miaka 20 jela na Mahakama ya Wilaya ya Moshi.

Taarifa hiyo imeeleza kuwa, katika kesi 11 za makosa ya maadili dhidi ya jamii, ikiwemo makosa ya kupatikana na dawa za kulevya na pombe haramu aina ya gongo, watuhumiwa waliopatikana na hatia na kuhukumiwa vifungo vya chini ya miaka sita jela, huku wengine wakitozwa faini kwa mujibu wa sheria.

Kadhalika, katika kesi nyingine 17 zilizohusu makosa mbalimbali ya jinai na usalama barabarani, watuhumiwa waliopatikana na hatia wamehukumiwa adhabu mbalimbali, ikiwemo vifungo vya chini ya miaka mitatu jela, huku wengine wakitozwa faini.

Wito kwa wananchi

Jeshi la Polisi Mkoa wa Kilimanjaro linaendelea kuwasihi wananchi wote kuwa na ushirikiano na Jeshi la Polisi kwa kutoa taarifa za uhalifu na wahalifu, pamoja na taarifa nyingine zinazoweza kusaidia kuzuia vitendo vya uhalifu katika jamii.

Soma Pia:
Wananchi wanakumbushwa kuwa taarifa hizo zinapaswa kutolewa kwa wakati kupitia vituo vya Polisi vilivyo karibu au kwa kutumia njia nyingine rasmi zinazopatikana, ili hatua stahiki za kisheria ziweze kuchukuliwa dhidi ya wahusika.

IMG-20260914-WA0277.jpg
 
Back
Top Bottom