Dark City
JF-Expert Member
- Oct 18, 2008
- 16,253
- 11,626
hahaha Mbona wapo waliosema wameshalambwa vibao DC ngoja nimuombe Mods atuwekee hiyo Poll cjui ndo inaitwa hivyo..
One day nilibakia kidogo kulambwa kibao ila mzee akajishitukia akasema una bahati marehemu mama yangu kabla ya kuondoka duniani alinikanya nisijaribu kumpiga mwanamke atakayekuwa mke wangu nadhani aliona maono ,kwani baba yake alikuwa mpigaji mzuri wa mkewe
Nikaomba kimoyomoyo abarikiwe marehemu mama mkwe popote alipo.
Ila sasa sijajua angenichapa hicho kibao ni hatua gani ingefatia muda huo
Hongera sana FL1,
Hili suala linaumiza sana. Mimi nimekuwa na maisha haya ninayoishi kwa sababu ya yale niliyoaona wakati nikiwa mtoto. Nikikumbuka huwa nalia machozi. Sitaki kabisa watoto wangu wayaone hayo, labda kama nimekufa na libwana jingine ndo linafanya hayo.
Mama yangu amebondwa sana mbele yetu. Very sad and painful experience.
Mimi siwezi kumpiga mke wangu. Ila kunyoosha mkono na kurusha kibao ilishatokea mara moja. Na hali ya kutamani kutoa kichapo inatokea mara nyingi tu. Lakini siwezi kumpa hata neno mbele za watu,.. hata akiniudhi namna gani. Mke wangu anahitaji heshima sana, of which my mom never got. Nawashimu wanawake wote ila ukweli uko pale pale kwamba wana maneno yao ambayo ni zaidi ya sumu ya cobra!
Tujadili haya mambo lakini tuwe realisitic badala ya ku-present TV images.