4% ya mapato kwenda Zanzibar kama Hoja ya Muungano

Sio misaada ni bakaa ya pato la muungano, hapa kuna vitu tunachanganya. Soma bandiko moja huko juu kuna mtu alielezea vizuri ingawa mwishoni alimaliza kwa jazba
Funzadume kumbe lilipofungwa jukwaa la ngono ukahamia kwenye siasa? Ha ha haaaa, sawa pamoja na hiyo bakaa ya pato la shughuli za muungano lakini pia misaada inatakiwa igawiwe kwa 4% iende Zanzibar. Hapa tulikuwa tunawadhulumu kwa kuwa ni koloni letu!
 
Kuna tatizo kwa Rais Samia

Inaonekana kwa kauli zake ni kama alikuwa na ''chuki' fulani na sasa anataka kutekeleza hoja za Wazanzibar na si kero za pande zote za muungano. Hili litamkwamisha sana kwasababu Watanganyika watakapochachamaa itakuwa tabu

1. Kama anataka pesa za 4% na nyingine , Rais Samia pia aeleze Mchango wa Zanzibar ni upi katika muungano?

2. Rais pia aimbie SMZ igharamie wazanzibar pale Bungeni na Wizara na taasisi za muungano kwasababu wanapata mgao wao.

3. Rais aweke wazi kipi cha muungano kipi sicho ili Watananyika nao wawe na fursa zao bila kuingiliwa

Rais Samia atambue ni Rais wa JMT si Mwakilishi wa Wazanzibar na kwamba Zanzibar wana Rais, nani atawaongelea Watanganyika?

Nimefuatilia kauli za Rais Samia ni kama vile amekuja kutekeleza hoja za Wazanzibar, hili litamsumbua sana hasa Watanganyika watakaposema 'enough is enough'. Yeye si Rais wa Zanzibar ni Rais kutoka Zanzibar

Rais Samia ana fursa ya kurudi katika Rasimu ya Warioba ili mambo ya muungano yawe wazi na Zanzibar ipate inachotaka. Tutaendelea kuidai Tanganyika ili nasi tuwe na nafasi ya kuamua masuala yetu

Kuna tatizo na Rais ashauriwe kwa kauli zinazoelekea kule kule tulipotoka '' Ni zamu yetu''

JokaKuu Mag3
 
kwani Zanzibar ni NCHI?.
Zanzibar HAINA tofauti na morogoro au singida au dodoma n.k
fedha zinazoenda kwenye miradi ya maendeleo ya mikoa ziende pia Zanzibar.
Your extremly right

Moja: Zanzibar sio nchi

Mbili: Vigezo vinavyotumika kugawa fedha za maendeleo kwa mikoa ya Tanzania bara hivyo hivyo vitumike kwa Zanzibar, haiwezekani kaeneo kadogo zaidi ya mikoa ya Morogoro, Tabora, Pwani kapate asilimia 4 ya fungu lote
 
Utapewaje faida ya biashara kama hukuweka mtaji?

Zanzibar haikuchangia chochote kama mtaji hapo mwanzo na imeendelea kutochangia chochote kwenye hayo maeneo kwa nini wapate mgao wa faida?
 
yaani Zanzibar ni nguzo ya utalii Tz? wewe upo tz ya wapi? zanzibar ngi nguzo ya utalii kuliko ngorongoro, serengeti, mikumbi na mbuga zote hizi? akili yako umetupa wapi?
 
Utapewaje faida ya biashara kama hukuweka mtaji?

Zanzibar haikuchangia chochote kama mtaji hapo mwanzo na imeendelea kutochangia chochote kwenye hayo maeneo kwa nini wapate mgao wa faida?
kwahiyo wanadai kitu ambacho hawakuchangia mtaji?
 
Na kuilipa kila moja analipa deni la 96%:4%
Zanzibar haijawahi tenga fedha kulipia madeni ya mikopo...kama unabisha angalia hata bajeti ya serikali ya mapinduzi ya mwaka wa fedha 2021/2022 kama utaona

Mzigo wa mikopo ya Zanzibar hulipwa na jasho na damu za watanganyika kupitia serikali ya muungano
 
tuhesabiwe sasa, lini waliwahi kulipa mikopo, na kwanini, na kwanini tuwabebe? na hata baada ya kuwabeba wanatuzodoa?
 
Zanzibar Wana sehemu ndogo ya bahari ndugu. Kumbuka kwenda north wameshafungiwa na Kenya kurudi kisiwa mafia . Kutokana na zile sheria za kimataifa Zanzibar kamwe hawezi kuwa na eneo kubwa kutuzidi Tanganyika
Mafia mbali kote huko

Kabla hawajafika huko kuna visiwa vidogo vidogo vya Tanganyika vina wa block, mfano kisiwa cha Latham
 
Kodi yote inayokusanywa na TRA Zanzibar hubaki Zanzibar, hakuna senti inayovuka maji

Wakati huo huo wafanyakazi wa TRA Zanzibar ambao wote ni wazanzibar wanalipwa na TRA Taifa (ambayo mapato yake yanatokana na jasho la watanganyika)
Kama hujui waulize wenye kujua sio unaongeaongea tu ili uonekane na wewe umejibu.
 
Afadhali umeyasema haya maana watu hawasomi historia wala hawajui nini kimeendelea, lakini wanapiga kelele tu.
 
Wao kwa wao wanabagua balaa... Yaani Huko Kwao Bado ni mtihani je Muungano ukifa.... [emoji16][emoji16][emoji16]
Nyinyi wenyewe mbona munabaguana sana tu? Tena kwa makabila fulani fulani. Mukiwa kabila moja na bosi upendeleo nje nje. Tunayaona yanavyoendelea.
 
Uvunjike tu dadek,hakuna cha % hapa yaani..
 
Wazanzibar wana nongwa sana nilichogundua hizi KERO kila siku zinaongezeka tu.
 
Wana jeshi lipi???jeshi ni muungano polis ni muungano,mambo ya nje ni muungano..?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…