4% ya mapato kwenda Zanzibar kama Hoja ya Muungano

je ni kweli pesa iliyochangiwa na znz ndo iliyojengea jengo lao la bot znz?
 
Kuna mtu kasema kuwa TRA wanakusanya mpaka Zenji??? [emoji15]
TRA ipo Zanzibar, na inakusanya mapato. Ila baada ya migongano mingi ya kera miaka kadhaa nyuma ikaamuliwa kuwa mapato yanayokusanywa na TRA yabaki Zanzibar, ila bado hayo mapato yanayokusanywa Zanzibar hayafikii hata 20% ya hiyo 4%
 
Walioweka hesabu kwa vigezo hivi walikuwa realistic? Ugawiwe hata kama huchangii inawezekana wapi? Gharama za Majeshi ya Muungano tu pamoja ya kuwa ni siri kuu, sidhani kama ZNZ inaweza kuzihimili wenyewe. Na mimi nimetoa tu eneo moja kama mfano.
Kwa kumuongezea mwambie mishahara yote ya watumishi wa SMZ inaliowa na Tanganyika
 
TRA ipo Zanzibar, na inakusanya mapato. Ila baada ya migongano mingi ya kera miaka kadhaa nyuma ikaamuliwa kuwa mapato yanayokusanywa na TRA yabaki Zanzibar, ila bado hayo mapato yanayokusanywa Zanzibar hayafikii hata 20% ya hiyo 4%
Basi hao TRA wamelegea, kwamba TRA mapato ya Znz yanabaki znz ili yafanyeje? [emoji23]
 
Zanzibar wana bodivyao inayo kusanya mapato, inaitwa ZRB.sema sasa niwaoigaji kichizi, wanakusanya pesa wanatoa mifukoni mwao.
 
Zanzibar wana bidi yao inayokusanya mapato
 
TRA ipo Zanzibar, na inakusanya mapato. Ila baada ya migongano mingi ya kera miaka kadhaa nyuma ikaamuliwa kuwa mapato yanayokusanywa na TRA yabaki Zanzibar, ila bado hayo mapato yanayokusanywa Zanzibar hayafikii hata 20% ya hiyo 4%

Wafanye kuanzisha yao tu ZRA ishu imesolve tayari
 
Wanao ngangania huu muungano ni watanganyika siyo wa zanzibar na kila rais wa ccm asema yuko tayari kulinda mungano hata damu imwagike lkn mungano uwepo mashekhe wa uamsho wamo ndani kwa kutaka mamlaka kamili ya zanzibar
Watanganyika Hatuwezi kung'ang'ania muungano kwasababu hautunufaishi.
 
Unajua kirefu cha KMKM?
 
Zanzibar ni Mali ya watu weusi huyo sultan alikuja na kuiona Zanzibar ingalipo . Oman ndio Mali ya sultan. Sultan ni muarabu na wazanzibar asilia ni watu weusi . Katika awamu wa Samia Zanzibar itapaa kimaendeleo kwasababu ya 4% ya Jasho la watanganyika masikini wa Hukwo Rukwa. Muungano ni huu ilikuepo faida Kwa Zanzibar ili kuzuia sultan asirudi Zanzibar baada ya mapinduzi ya afro Shiraz's party. Ila kuhakika hauna faida yeyote Ile .
 
Tutalipa 4% kwa misingi gani?
Kwani Muungano tunaulipia mahari?
 
Point zako nimezipenda kinamna ila ungenikosha kama ungeliuliza kwa muangalio wako huo huo, jee deni la tanzania kwa nchi za nje linawahusu vipi zanzibar, ilhali matumizi yote ya mikopo hiyo hufanywa tanzania bara? Zanzibar hupata mikopo yao kutoka nje ya nchi kivyao sasa kwa nini wahusishwe na malipo ya madeni ya Tanzania?
 
Mkuu umefika Zanzibar? umeona wabara waliokuepo Zanzibar? 80% ya wafanykazi wa mahoteli ni wabara. sasa hiyo hoja ya kuwa wazanzibar bara wapo wengi haina mashiko, mana hata Zanzibar wabara wapo wengi
Wabara wanabaguliwa sana na wa zenji. Sababu ya wafanyakazi wengi kutoka bara ni kwa sababu wazenji ni wavivu hawataki kufanya kazi.
 
Zanzibar ipo ZRB inayokusanya mapato, lakini inakusanya mapato kwa mambo amabyo sio ya muungano tu.

Kwa maana TRA pia wako na idara hiyo ya mapato katika vitu visivyo vya muungano au???
Mambo haya nadhani ZRB Inasimamia:
Mapato ya Serikali za mitaa, usafiri na barabara Ingawa kuna TANROADS. Pia Kilimo, mifugo pamoja na Uvuvi. Lakini Ishu ya Magereza na biashara baina ya wazalishaji wa chini na kati.

Lakini swali la Msingi:
Je TRA Inatenganisha hivi vitu kwa upande wa Tanganyika au ndo sandakalawe Amina??? [emoji16][emoji16][emoji15]
 
Wabara wanabaguliwa sana na wa zenji. Sababu ya wafanyakazi wengi kutoka bara ni kwa sababu wazenji ni wavivu hawataki kufanya kazi.

Walinikata jina langu Kisa tu Mimi ni Msukuma na Nina shahada ya Awali ya Teknolojia wanewapitisha Astashahada ya Teknolojia wakina Kombo na Hamdani [emoji2959]
 
Wabara wanabaguliwa sana na wa zenji. Sababu ya wafanyakazi wengi kutoka bara ni kwa sababu wazenji ni wavivu hawataki kufanya kazi.

Kama wanabaguliwa sana kama unavyosema wangekwenda na wakaendelea kuishi?

Na tukisema wabara ni mambumbumbu hawawezi kufanya Biashara ndiomana wapemba wakawa wamejaa huko nami nitakua nimekosea?
 
Walinikata jina langu Kisa tu Mimi ni Msukuma na Nina shahada ya Awali ya Teknolojia wanewapitisha Astashahada ya Teknolojia wakina Kombo na Hamdani [emoji2959]

Mkuu ulikatwa wapi?

Favorism ni kitu ambayo ipo kila sehemu, hayo ni mambo ya kawaida tu kwenye Dunia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…