41% ya wenye VVU jijini Dar wamepata mimba zisizotarajiwa

41% ya wenye VVU jijini Dar wamepata mimba zisizotarajiwa

Nyie ndio mnaoponza wenzenu, condom ina shida gani? Kwani haufiki unakoenda
Mie kwanza kibamia so condom inanipwaya niwe mkweli.
Pili, wanawake wenyewe wanakwambia raha ya tendo kumwagiwa shahawa...
Tatu sanyansi inasema condom upunguza utamu wa tendo kwa zaidi ya 30%. Sasa wataka ushahidi gani mwengine.
Wee unapenda condom? Kuwa mkweli
 
Mie kwanza kibamia so condom inanipwaya niwe mkweli.
Pili, wanawake wenyewe wanakwambia raha ya tendo kumwagiwa shahawa...
Tatu sanyansi inasema condom upunguza utamu wa tendo kwa zaidi ya 30%. Sasa wataka ushahidi gani mwengine.
Wee unapenda condom? Kuwa mkweli

[emoji15][emoji15] We kweli? Sasa itakuwaje na crush wako na zile ahadi zenu?

Kweli kiba100 km condom inagoma hakuna la kukusaidia endelea kuloweka
 
Binadamu bwana sasa hela zote hizo kwenye utafiti wa ngoma wakati ni jambo ambalo lipo wazi kuwa we fighting a lossing battle.
Watu wanapenda kavu kwa sababu ndivyo sex inavyotakiwa. U cant fight nature. Tukulane tuu jameni hamna namna kama kifa kupo tuu
Puuzie huu ujumbe..

Vaeni protection kabla ya kula vitu..telezeni kwa mliopimana.
 
View attachment 2659246
Taasisi ya Afya ya Ifakara imebaini kuwa asilimia 41 ya wanawake wanaoishi na virusi vya UKIMWI (VVU) Mkoa wa Dar es Salaam wamepata mimba zisizotarajiwa.

Hali hiyo imeelezwa kutokea kutokana na asilimia 60 ya wanawake wanaoishi na virusi hivyo, kutotumia njia za uzazi wa mpango.

Hayo yamebainishwa leo Juni 15, 2023 na Mtafiti kutoka Taasisi ya utafiti ya Ifakara Dk Francis Levira wakati akitoa wasilisho kuhusu utafiti huo uliofanyika katika miji ya Dodoma na Dar es Salaam mwaka 2021/22.

“Wakinamama ambao tuliwahoji, tuliwauliza kuwa mimba au uzazi wa mwisho kama ulikuwa umepangiliwa au haujapangiliwa na katika majibu tulipata Dodoma asilimia 29 na Dar es Salaam ilikuwa kubwa kwa asilimia 41, walipata mimba zisizotarajiwa”amesema Dk Levira.

Dk Levira amesema utafiti huo pia ulihusisha zaidi ya watu 15,000 ili kufahamu watu wangapi wanajua kama wana maambukizi na kutoa huduma ya upimaji.

Aidha Dk Levira amesema kati ya wanawake wenye virusi vya ukimwi ambao walifika kupata huduma kwenye vituo vya Afya ni asilimia 6 pekee ndio walikiri kupata huduma za uzazi wa mpango.

Akizungumzia kuhusu maambukizi kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto amesema utafiti umeabaini kati ya wanawake wenye virusi walioohojiwa ni asilimia 2 waliwaambukiza watoto wao virusi vya Ukimwi Mkoani Dodoma huku Dar es Salaam ikiwa kwa 8 asilimia.

Naye Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya ustawi na maendeleo ya jamii Fatma Taufiq amesema Serikali itumie tafiti hiyo kuboresha miundombinu ya vituo vya afya ili waathirika wanaofika vituo vya afya wapate na huduma za uzazi wa mpango.

Taufiq amesema huduma hiyo pia itasaidia kuwaeleza waathirika hao namna bora ya kuzuia watoto wao wasipatwe na virusi vya UKIMWI
Watu wanapiga ACAPELLA kama ulaya
 
Back
Top Bottom