42. Wananchi 268 wahudumiwa kliniki ya ardhi Chemba, hati 181 zasajiliwa

42. Wananchi 268 wahudumiwa kliniki ya ardhi Chemba, hati 181 zasajiliwa

Wizara ya Ardhi

Govt Institution
Joined
May 14, 2024
Posts
306
Reaction score
165
IMG_7540.png


CHEMBA

Wananchi 268 wamehudumiwa katika Kliniki ya Ardhi Wilaya ya Chemba mkoani Dodoma ndani ya siku tano tangu kuanza kwa huduma hizo Oktoba 5, 2026, huku hati miliki za ardhi 181 zikiwa zimesajiliwa na nyingine 92 zimechukuliwa na wahusika.

Akizungumza kuhusu mafanikio ya kliniki hiyo, Oktoba 10, 2026 Kamishna wa Ardhi Msaidizi Mkoa wa Dodoma, Bi. Happiness Mtutwa, amesema kliniki hiyo itaendelea kutolewa ili kuwafikia wananchi wengi zaidi na kurahisisha upatikanaji huduma za ardhi, hususan usajili wa hati miliki.

Amesema, lengo la kliniki hiyo ni kuhakikisha wananchi wengi zaidi wanapata hati miliki za ardhi zao, akiwashukuru kwa kujitokeza kwa wingi na kuendelea kutumia fursa hiyo kupata huduma karibu na maeneo yao.

“Lengo letu ni kutoa hati nyingi kadri inavyowezekana hapa Wilaya ya Chemba. Nashukuru wananchi wamejitokeza kwa wingi” amesema Bi. Mtutwa.

Aidha, amesema amewaelekeza wataalamu wa ardhi kuwasiliana kwa njia ya simu na wananchi walioanza mchakato wa kupata hati miliki lakini hawajakamilisha hatua zinazohitajika, ili waweze kukamilisha miamala yao kwa wakati.

Mbali na hayo, Bi. Mtutwa amewasisitiza watumishi wa sekta ya ardhi katika Halmashauri ya Wilaya ya Chemba kutoa huduma bora kwa wananchi, kutatua changamoto zinazowasilishwa kwa wakati na kuhakikisha kuwa utendaji wao hauleti migogoro mipya ya ardhi.

Ameendelea kuwahimiza wananchi wa Wilaya ya Chemba kujitokeza kwa wingi kupata huduma za ardhi na kutumia mfumo wa kielektroniki wa e-Ardhi, unaowawezesha kupata huduma mbalimbali za ardhi kwa urahisi na kwa wakati, ikiwemo huduma zinazohusiana na upatikanaji wa hati miliki za ardhi.
 
Back
Top Bottom