Hawa jamaa wanakatisha tamaa vijana. Yaani wanatuma maombi ni vijana wengi mamia kwa mamia mwisho wa siku wana shortlist watu watano kwenda kwenye interview.
Imefikia kipindi taasisi na mashirika ya umma yatoe haki sawa kwa watanzania watanzania wote. Ita vijana wote wenye vigezo uwachuje sio una shortlist kwa ubaguzi.
Vijana wanavunjika moyo sana kwa kunyimwa hata fursa ya kuitwa tu kwenye usaili. Mamlaka zinazohusika na usaili wa utumishi wa mahakama tafadhari tafakarini hili.
Binafsi naumia sana napomuona kijana mwenzangu anahangaika kutafuta ajira na hata usaili tu ananyimwa.
Fanyeni kama wanavyofanya utumishi.