46% ya Wanawake wa Zanzibar ni Wanene Kupita Kiasi, Tanzania Bara ni 36%

46% ya Wanawake wa Zanzibar ni Wanene Kupita Kiasi, Tanzania Bara ni 36%

Mkuu @safuher umeisikia hiii?
Mkuu habari za siku,na samahani sana kwa kuchelewa kureply hii mada.
Lakini inawezekana huo unene walionao watu ndiyo afya yao kwa heshima zao na uoni wao. With respect to them
UMeongea inshu ya msingi sana mkuu,tunaweza kusema kwamba wanene ni asilimis kadhaa kumbr hata hao wenyewe hawajioni kama ni tatizo ns unene wao.

Na katika maeneo ambayo wanawake wako bize na mapishi basi ni zanzibar,wanawake wanapika sana avyakula vya aina mbalimbali.

Hivyo na mimi naunga mkono mawazo yako kwamba asilimia kubwa ya wanawake wa kizanzibar hawaoni tati,o kuwa na unene kwa sababu hulka yao ni kupika hivyo hata kula watakuwa wanakula kwa uwingi pia.


Lakini pia ikikupendeza naomba uniambie kile unahisi, (au unajua) kibaiolojia wewe ni ipi 1. faida ya kuwa na kitambi mwilini?
Mkuu mimi nahisi faida ya kitambi ni stoo ya chakula cha ziada yaani mafuta,pale ambspo mwili utakosa chakula kwa muda mrefu basi mafuta ya kitambi yanaweza kutumika kuzalisha nishati ya mwili.

Kwa mantiki hiyo nadhani mtu mnene kama msechu na mtu mwembamba kama barnaba ukiwaweka na njaa kwa siku kadhaa mimi natarajia atakayeanza kufa ni barnaba kwa sababu ana akiba chache ya mafuta kuliko msechu.

Hivyo mimi nadhani hiyo inaweza kuwa faida endapo ikitokea hali hiyo ya njaa,mbali na hapo mkuu sijaona faida ya kiafya ya kuwa na kitambi kikubwa


Ipi faida ya kutunza maji na mafuta mwilini?
KAma nilivyotoa mfano wa msechu hapo juu ni kwamba mkuu utunzaji wowote ule bila shaka faida yake ni wakati wa mahitaji.

Hivyo mafuta na maji yakiwa yametunzwa mwilini kwa wingi na ikatokea siku mtu hana chakula wala maji basi yale yaliyohifadhiwa mwlini yatasaidia kumfanya asife mapema kwa njaa.

Lakini mbali ya faida hii nadhani jambo hili kutokea ni nadra sana kwamba mtu akae labda wiki 2 mpaka tatu hajapata maji wala chakula kwa mazingira yetu sio rahisi.

Hivyo hii hali ya dharura ambayo ni nadra kutokea isije ikatufanya tuhamasike kula saaana ili tutunze maji na mafuta ati kwa lengo la akiba pale inapotokea njaa😃.

Kwa sababu licha ya mafuta kutumika kama chanzo cha nishati pale penye uhaba lakini pia mafuta mengi mwilini huleta matatizo mbalimbai ya kiafya kama vile presha,shambulio la moyo n.k

Hivyo huwenda faida yake ikawa ni ndogo kiko madhara ya kuhifadhi mafuta hayo kwa muda mrefu huku tukisubiria matukio ya njaa na ukame.
 
Hivyo mafuta na maji yakiwa yametunzwa mwilini kwa wingi na ikatokea siku mtu hana chakula wala maji basi yale yaliyohifadhiwa mwlini yatasaidia kumfanya asife mapema kwa njaa.

Lakini mbali ya faida hii nadhani jambo hili kutokea ni nadra sana kwamba mtu akae labda wiki 2 mpaka tatu hajapata maji wala chakula kwa mazingira yetu sio rahisi.
Sahih. ✅

Na ulivyosema kuhusu kitambi pia ni sahihi kabisa.

Hiyo ndiyo faida ya kuwa na ziada mwilini.

Ni kwamba baiolojia ya miili yetu haijajihuisha(update) ili kuendana na dunia ya sasa bado ipo kizamani, primitive.

Zamaani hizo ilikuwa chakula ni cha taabu, hivyo mwanadamu akiuashiria mwili ki namna yoyote kwamba kuna shida/dhiki/hatari kwa mawazo yake. Mwili ulijiandaa kwa kuwa na akiba ya chakula na rasilimali nyingine. Maana chakula kilikuwa shida, cha kutafuta. Sasa huwezi kutafuta wakati simba wametapakaa. Au chochote.

Bahati mbaya hata hii leo mwili unaitikia vilevile. Hata tu mtu akiwaza deadline ya kazi! Au kubambwa na mchepuko. Yaani kila aina ya hofu mwili ukiaminishwa utaitikia kama enzi za mapangoni huko (primitively).

Tujiulize swali, je mwili utaweka tuu akiba ikiwa umejiaminisha kuwa chakula kipo bwerere? Na hakuna vita wala dhiki wala balaa lolote linalotarajiwa? (No impending doom/catastrophe)

Katika mifano yako, inawezekana Barnaba ako na hofu chache (ni ka musical genius kajamaa) kuliko Msechu labda. Kwa hiyo tukiwasoma mentality zao mmoja kajiachia na mwingine ametahayari (on edge) muda mwingi. Basi ndio maana maandalizi yao ya kukabili hatari (au kutokuwepo hatari) yanajipambanua katika miili yao.

Natamani wana JF tufanye kama utafiti, kuangalia falsafa za Barnaba VS falsafa za Msechu kupitia nyimbo zao tuone. Je itikadi na akili zao zimechangia kiasi gani hali zao kibaiolojia. Sema hapo tutakuwa tumefanya 'assumption' kwamba huwa wanaimba ya moyoni mwao maana kimjazacho mtu ndicho humtoka.

Nadharia ambayo tuipime hapa ni kwamba, bila hofu ya chochote: (Kukosa, kuachwa, kusemwa, kukamatwa, kukufa, kuugua) hakuna mwili utatunza wala kuhangaika kutafuta mbinu za kuongeza akiba ya rasilimali mwilini🤔. Stress/hofu ndiyo chanzo. Na mwili unajikusanyia ili kujilinda usipotezwe 'survival'


Hongera sana Mr. Umechelewa kujibu lakini umekuja kujibu kitu kimoja kamilifu sana 🙌. Ni matumaini yangu kuwa atakayeyaona majadiloano yetu, yakamuongezee vitu viwili vitatu katika vita yake.
 
Programu itategemea nini hasa ndio chanzo cha huo unene. Kulingana na utaalamu.
Ni sahihi mkuu ,ukijua chsnzo umetibu nusu ya tatizo.
Mr Safuher mimi naweka mbele hoja kuwa, tatizo zima la unene ni suala moja tu ULINZI BINAFSI basi.
NAm mkuu baada ya kusoma ufafanuzi wako kuhusu ulinzi binafsi narudi hapa kuchangia juu ya inshu nzima ya ulinzi mr Uhakika Bro .

Kuhusiana na suala la ulinzi binafsi hii nadharia imenishangaza na kunifurahisha japokuwa bado inanitia mashaka mengi lakini naona iko very interesting na kuna haja tuendelee kuijadili zaidi ili tufikie hatua fulani nzuri katika kuitambua.
Nadharia ambayo tuipime hapa ni kwamba, bila hofu ya chochote: (Kukosa, kuachwa, kusemwa, kukamatwa, kukufa, kuugua) hakuna mwili utatunza wala kuhangaika kutafuta mbinu za kuongeza akiba ya rasilimali mwilini🤔. Stress/hofu ndiyo chanzo. Na mwili unajikusanyia ili kujilinda usipotezwe 'survival'
Nimekuwa na falsafa yangu moja ambayo inasema kwamba "unene wowote unatokana na chakula"

Na huo unene ni yale mafuta ya ziada ambayo yamehifadhiwa mwilini.

Mimi huwa nafikiria kwamba mwili unahifadhi chakula sio kwa sababu ya ulinzi,bali mwili unahifadhi chakula kwa sababu tu kimezidi hivyo mwiki hauna namna nyingine zaidi ya kukihifadhi.

kwa mantiki hiyo chakula kilichozidi(mafuta ya mwili) ni sawa na maji ambayo yanamwagika baada ya ndoo kujaa.

Maji yakishajaa kwenye ndoo alafu ukaendelea kuyatia bila shaka kuna maji yatamwagika,yale maji yanayomwagika yanamwagika kwa sababu kuna ambayo yamezidi hivyo hakuna namna lazima mengine yamwagike tu,ndivyo nadhani ilivyo kwenye chakula na mwili.

Hivyo mimi nahisi haya mafuta ya ziada yanahifadhiwa sio kwa sababu ya kuitikia ile taarifa ya ulinzi wa mwili,bali nahisi yanahifadhiwa kwa sababu tu yamezidi mwilini na hivyo mwili hauna namna nyingine ya kufanya zaidi ya hiyo..

Hivyo mafuta ya ziada mwilini ni product ambayo haina budi kufanywa pale endapo chakula kimezidi mahitaji ya mwiili husika.

HIi naitilia nguvu kwa kurejea historia za wazee wetu wa nyuma ambao wengi walikuwa wakulima,haikuwa rahisi kukuta mtu ni mnene na mavitambi kwa sababu mwili utumia chakula bila ya kubakisha ziada kutokana na kushughulika na harakati za kilimo n.k


Sasa shida ya wakati huu wa kisasa ni kwamba tumerithi ulaji lakini hatukurithi harakati za maisha,tumekuwa na maisha ya kisasa huku ulaji wetu ukiwa ni wa kizamani.

HIvyo tunashindwa kuwa na miili ambayo haina akiba kwa sababu walaji wa zamani walikula na kufanya kazi za kushughulisha miili wakati huo walaji wa kisasa wanakula na kukaa maofisini tu.
 
Nimekuwa na falsafa yangu moja ambayo inasema kwamba "unene wowote unatokana na chakula"

Na huo unene ni yale mafuta ya ziada ambayo yamehifadhiwa mwilini.
Hii ni sahihi, ni kweli kabisa kwamba unene ni mafuta (na rasirimali nyinginezo, maji, protini, madini nk) ya ziada ambayo yamehifadhiwa mwilini. Ni chakula tulichokula.


huwa nafikiria kwamba mwili unahifadhi chakula sio kwa sababu ya ulinzi,bali mwili unahifadhi chakula kwa sababu tu kimezidi hivyo mwiki hauna namna nyingine zaidi ya kukihifadhi.

kwa mantiki hiyo chakula kilichozidi(mafuta ya mwili) ni sawa na maji ambayo yanamwagika baada ya ndoo kujaa.
Hapa sasa panahitaji umakini.

Modeli yako inaitwa ya kimakanika (mechanistic view), yaani inafanya kama vile mwili hauna akili na unajazwa vitu kulingana tu na mazingira uliyokumbana nayo.

Kwamba kama ni kalori zimewekwa nyingi kuliko zilizotumika basi mtu ananenepa.! Hapa ndipo tulipotofautiana.

Mimi maoni yangu ni kwamba mwili ni una akili yake kabisa(vitalistic view) unayo malengo na unayatimiza kulingana na bwana wake (wewe) upo mazingira yenye mahitaji gani.

Kwa hiyo kama ni ndoo (mwili) kwako ni inajazwa maji tu kulingana na mazingira kuleta maji mengi na ndio yanakuwa yamehifadhiwa katika ndoo mechanistically.

Basi kwangu ni kwamba ndoo (mwili) yenyewe unajiwekea mikakati mahsusi, kukusanya na kuhifadhi maji mengi zaidi kwa sababu tu imewasiliana na mazingira yakasema 'kutakuwa na ukame, shida, dhiki fulani' na ndoo inatambua kuwa. Kukiwa na jua kali ndoo zisizokuwa na maji hupasuka na kupotezwa mazima(sure death)🤔.
Hivyo mafuta ya ziada mwilini ni product ambayo haina budi kufanywa pale endapo chakula kimezidi mahitaji ya mwiili husika
Ukweli ni kwamba, kwa mtazamo wa mwili wakati huo, hauwazi kwamba nimezidisha kuhifadhi. La. Bali mwili huwaza kwamba hicho ndicho kiasi kifaacho kutunzwa mwilini kutokana na hali ilivyo (hatari). Kikipungua kidogo mwili huwekeza mikakati ya kukirudisha kama;
A. Mtu asikie njaa kali
B. Atake sukari na chumvi
C. Apunguze kuchoma mafuta
Ndio maana anayepunguza unene akifanikisha kidoogo, basi mwili utaitikia kumrudiahia hali yake iliyo 'salama zaidi'

Ni kama tu ambavyo mtu mwenye homa, anavyoswma 'nasikia baridi' na anatetemeka ili kupandisha joto hata likipungua kidoogo tu katika hilo joto kali ambalo tayari analo mwilini (homa). Ni kwa sababu kiwango chake (thermostat) ameiseti juu kwa makusudi kabisa ya mahitaji ya mwili kwa mazingira hayo.
tumerithi ulaji lakini hatukurithi harakati za maisha,tumekuwa na maisha ya kisasa huku ulaji wetu ukiwa ni wa kizamani.

HIvyo tunashindwa kuwa na miili ambayo haina akiba kwa sababu walaji wa zamani walikula na kufanya kazi za kushughulisha miili wakati huo walaji wa kisasa wanakula na kukaa maofisini tu
Umeangazia, ulaji na ukaaji tu.

Je umegusia ufikiri?

Hofu walizopambana nazo, na shida walizopambana nazo.

Maana leo mtu wa ofisini akisema nina kazi kubwa mbele kesho (stress ya mafaili mengi). Na ndivyo hivyo mkulima atasema nina kazi kubwa mbele kesho (stress ya kufyeka eneo jipya na visiki) hawa wote miili yao iliwaamini na kuwaandalia akiba ya nishati. Lakini mmoja ataitumia kweli, mwingine misuli yake haitahusika saana.

Ni kweli tuna mkanganyiko katika mtindo wa maisha

Dawa ni nini?
Dawa ni mtu awe mkweli, kama kazi ni nyepesi, aseme kazi ni nyepesi asiupe mwili taarifa tofauti. Kama hakuna hatari aseme hakuna hatari asiupe mwili taarifa tofauti. Maana ukishaupa mwili taarifa ki stress, mwitikio wake ni kujaza rasilimali mwilini (kuhifadhi)
 
Modeli yako inaitwa ya kimakanika (mechanistic view),
Ahaha nakupata vizuri kaka mkubwa.
Modeli yako inaitwa ya kimakanika (mechanistic view), yaani inafanya kama vile mwili hauna akili
Hapa mkuu NItaonesha huko mbele namna ambavyo hata dhana yako inafanya kana kwamba mwili hauna akili pia
Kwamba kama ni kalori zimewekwa nyingi kuliko zilizotumika basi mtu ananenepa
Haswaa ndio falsafa ambayo nimekuwa nikiisimamia.
Mimi maoni yangu ni kwamba mwili ni una akili yake kabisa(vitalistic view)
Kabisa kaka hata mimi nakubaliana na wewe kwamba mwili una akili yake,lakini tunatofautiana namna ambavyo mwili hutumia akili hiyo.

Mimi naona mwili katumia AKILI kwa kufanya kitendo cha kuhifadhi chakula cha ziada ambacho hakina matumizi kwa wakati huo.

Wakati huo wewe unaona kwamba bwana mwili hajatumia akili,hapo tunatofautiana 😃.

Ili kutengeneza msingj mzuri kwetu mimi nauliza swali lifuatalo 👇👇👇

ni vitendo vyenye sifa gani mwili akivifanya ndipo unaona kwamba ametumia akili ?
Na ni vitendo vyenye sifa gani mwili akivifanya ndipo unaona HAJATUMIA akili ?


kwa mtazamo wa mwili wakati huo, hauwazi kwamba nimezidisha kuhifadhi.
kama bwana mwili hawazi uhalisia wa kwamba chakula kimezidi basi nadhani hii dhana yako pia inafanya kana kwamba mwili hauna akili kwa sababu kama mwili ungekuwa na akili ungeliwaza uhalisia ambao ni kuzidi kwa chakula.
Bali mwili huwaza kwamba hicho ndicho kiasi kifaacho kutunzwa mwilini kutokana na hali ilivyo (hatari)
Kama mwili unawaza hivi nadhani pia kwamba tunaudefine mwili kwamba hauna akili.

Kwa nini mwili uwaze jambo ambalo ni kinyume na uhslisia ? Hiyo inaweza kuwa ni ishara ya kwamba hii nadharia yako mkuu nayo inaufanya mwili kana kwamba hauna akili.
Je umegusia ufikiri?
Naam sijagusia kwa sababu fulani huwenda tukaiona huko mbele mkuu.
Maana leo mtu wa ofisini akisema nina kazi kubwa mbele kesho (stress ya mafaili mengi). Na ndivyo hivyo mkulima atasema nina kazi kubwa mbele kesho (stress ya kufyeka eneo jipya na visiki) hawa wote miili yao iliwaamini na kuwaandalia akiba ya nishati. Lakini mmoja ataitumia kweli, mwingine misuli yake haitahusika saana.
Kama mwili anaandaa nishati sawa baina ya mtu anayefanya kazi za misuli sana na mtu anayefanya kazi za ofisi sana basi nadhani hiyo pia ni uthibitisho wa kwamba mwili hauna akili.

Kwa sababu mwili angekuwa na akili angeweza kutofautisha baina ya mtu wa ofisi ambaye hatumii sana misuli na mtu mkulima ambaye anatumia sana misuli.

Ndio maana nikasema kwamba hata hii nadharia yako mkuu inaichukulia kwamba mwili hauna akili.

Kuondoa utata huu ndipo niksuliza swali hili "

ni vitendo vyenye sifa gani mwili akivifanya ndipo tunahesabu kwamba mwili ametumia akili ?


Na ni vitendo vyenye sifa gani mwili akivifanya ndipo tunahesabu kwamba mwili HAUJATUMIA akili ?

 
wapeleleze yote, na yale mengine kama bado yapo au yalishasambaratishwa kitambo. nadhani tamaduni zinawagarimu, mwanamke hafanyi kasi, toka asubuhi amefungiwa na bwanake asije akatoka nje wagalatia wakamwona wakamtongoza, hadi sokoni mwanaume ndio anaenda, kwanini asinenepe kama fukusi? kazi yake ni kula tu na kumsubiria jamaa arudi kwenye mihangaiko aje ampe unyumba, na aina za vyakula wanavyokula vina wanga mwingi mno, mara machapati, mikate, nyama imejaa mafuta, kalimati, maandazi,kababu,kabibi, urojo fujo tupu.
 
Mimi naona mwili katumia AKILI kwa kufanya kitendo cha kuhifadhi chakula cha ziada ambacho hakina matumizi kwa wakati huo.

Wakati huo wewe unaona kwamba bwana mwili hajatumia akili,hapo tunatofautiana 😃.
😆😂 ahsante kupoint out, yas ukichukulia kuwa mwili unakuwa umetumia akili kusema 'chakula kimezidi, hakitatumika chote sasa ivi wacha nifanye mchakato nikihifadhi hapa na pale. Oooookay, sawa ni akili.

Basi nafurahi kwa sababu wote kumbe tupo kwenye ile vitalistic view. MWILI UNA AKILI 🤝.

kama bwana mwili hawazi uhalisia wa kwamba chakula kimezidi basi nadhani hii dhana yako pia inafanya kana kwamba mwili hauna akili kwa sababu kama mwili ungekuwa na akili ungeliwaza uhalisia ambao ni kuzidi kwa chakula
Kuna kuzidi kwa aina, hapana nnamaanisha kwa hatua mbili na zote ni kweli;
1. Chakula kimezidi kwenye mlo
2. Chakula kimezidi kwenye mwili, kwenye hifadhi.

Wewe umekazia zaidi suala la mwili kutambua na kuchakata namba moja kuliko hiyo namba mbili.

Maana kama mwili ungetambua kuwa chakula kimeshazidi katika hatua zote mbili basi ungezuia kukitafuta, kukisharabu na kukitunza. Badala yake mtu akajisaidie chooni. Ndiyo. Mwili unao uwezo wa kuchagua usharabu sana au usharabu kiasi tu chakula unachokula.

Fact/Kijiukweli: Mjamzito husharabu kalsiamu zaidi ya mwanamke ambaye hana kakichanga kanakotengeneza mifupa ndani yake🤔. Akili mwili ya kujua ninahitaji kalsiamu zaidi, nitaitafuta zaidi na nitaisharabu zaidi.

Hivyo basi, kama bado unakusanya, maana yake kwa akili yake (ya kuambiwa na mwenye nao) bado inaonekana chakula hakitoshi kukabili vita/dhiki ijayo
Kama mwili anaandaa nishati sawa baina ya mtu anayefanya kazi za misuli sana na mtu anayefanya kazi za ofisi sana basi nadhani hiyo pia ni uthibitisho wa kwamba mwili hauna akili.
Mwili akili yake ni kama ya mtoto zaidi, hauna mantiki sana (kama conscious thought). Hautumii hesabu vizuri. Ni uwanda wa subconscious na unaathiriwa saana na kiwango cha msisitizo binafsi wa mtu.

Mtu akijisemea kuwa kazi ni kuuuuuuuubwa mbele yake, na akajaza mahisia mengii basi mwili humjaza nguvu kulingana na alivyouambia.

Una akili mwili, lakini kwa kitojua hesabu na mantiki, kuna uwezekano ukaandaa nishati kubwa kuliko kiuhalisia inayohitajika. Tena wa ofisini anao uwezo wa kumzidi wa shambani, akiwekeza mawazo visivyo.

Maono: ukichukua takwimu kijuujuu, mameneja wengi ndio hiwa wanene kuliko wanaowasimamia: basi ni kwa sababu meneja anajiona ana mzigo mkuuuuuuubwa wa kazi kuliko mfanyakazi wake. Japo woote, kimsingi wanachofanya ni kuandika andika makaratasi tu. Waweke wote wana maisha karibu sawa kama gari na nyumba.
ni vitendo vyenye sifa gani mwili akivifanya ndipo tunahesabu kwamba mwili ametumia akili ?


Na ni vitendo vyenye sifa gani mwili akivifanya ndipo tunahesabu kwamba mwili HAUJATUMIA akili ?
Ndugu, tumekubaliana kwamba mwili una akili, maoni yako na maoni yangu yoote yameelekeza ni akili.

Nilikuweka kundi la pili (la mamechanistic pipo) kimakosa.

Haiya bro jibu hiki;
Ni kwa nini mwili uendelee kushinikiza, kutafuta, kula na kusharabu chakula hata kama mtu tayari ako na uzidifu wa 'rasilimali' alizohifadhi mwilini?

Nakazia, kwa nini usizuie tena hamu ya chakula? Na mtu akijilazimisha kula ni kwa nini usiache asilimia kubwa iende na haja kubwa?
 
Ndugu, tumekubaliana kwamba mwili una akili, maoni yako na maoni yangu yoote yameelekeza ni akili.

Nilikuweka kundi la pili (la mamechanistic pipo) kimakosa.
😃Naam tupo pamoja mkuu na umenijibu na nimetosheka na majibu yako,umenitendea haki haswa mkuu katika kujibu kwako.
Ni kwa nini mwili uendelee kushinikiza, kutafuta, kula na kusharabu chakula hata kama mtu tayari ako na uzidifu wa 'rasilimali' alizohifadhi mwilini?
Daah mkuu hili swali lako ni gumu na liko very technical😃😃

JAwabu langu : mimi naona kwamba kuna wakati miili yetu inahisi njaa sio kwa sababu hakuna chakula mwilini hapana,bali tunahisi njaa kwa sababu hakuna chakula tumboni(stomach).

Kuhisi njaa ni ishara ya mwili na ni wito kutujulisha kwamba jamani eeee humu tumboni hakuna kitu,hivyo mtu akiitikia wito huo kwa kula maana yake njaa itaondoka.

ILa kama mtu hatoitikia wito huo amwili atasema poaa kama hamtaki kuleta chskula tumboni mimi naenda kumega mafuta yaliyopo kwenye mapaja ama tumbo kwa ajili ya kuzalisha nishati ya mwili,na hapo ndipo mwili husnza kuchoma mafuta.

Na ndio maana wakati wa mfungo kama huu wetu wa kiisilamu kuna wakati utahisi njaa kali sana lakini baada ya muda hauhisi tena njaa,kwa nini ?
K
wa sababu wakati umefunga ile njaa unayoihisi ni kwa sababu mwili unakupa ishara kwamba tumboni hakuna chakula.

Sasa unapoendelea kukaa na njsa bila kula maana yake mwili atasema aah poa si umekataa kuleta chakula tumboni basi mimi namega mafuta ya mwili,na hapo ndipo mtu anaanza kuhisi njaa inapunguaa zaidi kwa sababu mwili ametafuta mbadala wa chakula.


Hivyo basi hata mtu kibonge mwenye akiba ya kutosha atahisi njaa kwa sababu chakula cha tumboni ndio ambacho mwili hukitumia kwa kuupa mwili ngumu.

So hata kama mtu awe mnene kiasi gani mwili hatoangalia kwamba jamaa ana mafuta ya akiba kiasi gani bali mwili ataangalia jee tumboni ipo chakula ama hakipo ? ,kama hakipo ndipo ataita kwa mfumo wa kuhisi njaa.
Nakazia, kwa nini usizuie tena hamu ya chakula? Na mtu akijilazimisha kula ni kwa nini usiache asilimia kubwa iende na haja kubwa?
😃😃 swali jingine gumu na very technical.

Jawabu langu : mimi nadhani kwamba akili ya mwili ndio imeishia hapo yaani kuhifadhi chakula cha ziada badala ya kukigeuza kiwe haja mtu ajisaidie na asiwe na mafuta ya ziada mwilini.

Nadhani Hoja yako haswa katika swali hili mkuu ni kwamba "kama kuhifadhi chakula ch ziada cha mwili ni vibaya kwani mwili hauna akili ya kutafuta mbadala mwingine wa kuondoa ziada ya chakula hicho badala yake itafute mbadala huu wa Kuhifadhi chakula ambacho baadae kitakuja kuleta shida ya obesity na magonjwa mengine ?
jawabu langu linarudi palepale kwamba akili ya mwili ndiyo imeishia hapo na kama ulivyosema kule juu kwamba 👇👇
Mwili akili yake ni kama ya mtoto zaidi, hauna mantiki sana
NA ukasema pia kwamba 👇👇👇
Hautumii hesabu vizuri.
Hivyo huwenda hapa katika jambo hili la kubadilisha akiba iwe haja basi huwenda ni katika mambo ambayo mwili haukutumia hesabu vizuri ?

Au huwenda jambo hili la kubadilisha akiba kuwa haja limeshindikana kufanywa na mwili kwa sababu ile uliyoisema kwamba akili ya mwili ni kama ya mtoto ?

hivyo basi ukiendelea kula chakula mwili utakusikikiza wewe kwamba huyu jamaa maadamu anakula chakula basi anakihitaji hivyo acha tukihifadhi na kingine tukitoe kama haja kubwa.

Lakini ukikaa na njaa muda mrefu huwenda mwili anasema kwamba jamaa hahitajii chakula huyu hivyo hata hiki cha akiba tukiondoe mwilini.

Sijui kama nimekujibu mkuu ?

Na kama sijakujibu naomba urejee tena kuuliza ili tuende sambamba katika mjadala wetu huu.
 
Perfecto!

Mwenye masikio (macho) na asikie (ajisomee) madini hayo 🤝
mkuu naomba na mimi nikuulize swali kidogo kutokana na huu mjadala wetu.

Kuna sehemu ulisema hivi 👇👇👇👇
, kama bado unakusanya, maana yake kwa akili yake (ya kuambiwa na mwenye nao) bado inaonekana chakula hakitoshi kukabili vita/dhiki ijayo
SWali langu liko hivi..

Je mkuu wewe unakubaliana na suala la kwamba unene uliopitiliza unaweza kusababisha magonjwa sugu kama vile stroke,pressure ama kisukari ?
 
Back
Top Bottom