46% ya Wanawake wa Zanzibar ni Wanene Kupita Kiasi, Tanzania Bara ni 36%

46% ya Wanawake wa Zanzibar ni Wanene Kupita Kiasi, Tanzania Bara ni 36%

mkuu naomba na mimi nikuulize swali kidogo kutokana na huu mjadala wetu.

Kuna sehemu ulisema hivi 👇👇👇👇

SWali langu liko hivi..

Je mkuu wewe unakubaliana na suala la kwamba unene uliopitiliza unaweza kusababisha magonjwa sugu kama vile stroke,pressure ama kisukari ?
Ndiyo, unene uliopitiliza unaweza kusababisha magonjwa sugu kama pressure na stroke........ na kisukari pia kinahisianishwa saana na unene uliopitiliza uliodumu.
 
Shinyanga,geita,tabora uko wanawake wakishaolewa wanageuzwa TREKTA

Tofauti na dar na Pemba, wanawake wanaolewa na kugeuzwa MAUA
 
Ndiyo, unene uliopitiliza unaweza kusababisha magonjwa sugu kama pressure na stroke........ na kisukari pia kinahisianishwa saana na unene uliopitiliza uliodumu.
Sawa sawa mkuu.

Swali la nyongeza kidogo mkuu..

Unadhani ni kwa nini bwana mwili anaacha mpaka unene unakuwa mkubwa na kusababisha magonjwa hayo wakati bwana mwili huyo anao uwezo kabisa wa kuepuka unene huo kutokana na akili aliyokuwa nayo bwana mwili huyu ?

Unadhani ni sababu gani inasababisha mwili mpaka anashindwa kucontrol uzito ambao baadae unaenda kusababisha magonjwa hatarishi ?
 
Unene wa Zanzibar unatokaba na kuzaa sana sio kula ,chunguza hilo unene anaopata mwanamke baada ya kuzaa .
Mwanamke akizaa anapumzika majukumu mengine,anabaki kulea uku akifakamia misosi non-stop.

Angalia wanawake wa kisukuma,
Wakizaa wanapungua maana kibarua Kiko pale pale[emoji4]
 
Kuzaa + kula sana = Unene

Azae halafu apige pasi ndefu unene atausikia tu.
Aangalue vizur single mother wanaozalia maghetoni, afu maisha Ni magumu. Matiti Kama ndala, wamekonda na kuchakaa Kama mbwa koko[emoji29]
 
wapeleleze yote, na yale mengine kama bado yapo au yalishasambaratishwa kitambo. nadhani tamaduni zinawagarimu, mwanamke hafanyi kasi, toka asubuhi amefungiwa na bwanake asije akatoka nje wagalatia wakamwona wakamtongoza, hadi sokoni mwanaume ndio anaenda, kwanini asinenepe kama fukusi? kazi yake ni kula tu na kumsubiria jamaa arudi kwenye mihangaiko aje ampe unyumba, na aina za vyakula wanavyokula vina wanga mwingi mno, mara machapati, mikate, nyama imejaa mafuta, kalimati, maandazi,kababu,kabibi, urojo fujo tupu.
Sahii kabisa,
Wanaume wa Kipemba wananishangaza Kwenda sokoni
 
Halafu sijui ni shetani au ni nini, juzi tu nmewaza kwa sauti nikajisemea "nipunguze kidogo kula" cha ajabu hiyo jana nmeamka na apetite ya hatari asubuhi nmekula chapati tatu... Shetani ana nguvu kuliko breakdown
Lakini ukigonga chapati 3 asubuhi hiyo si ni moja kwa moja mpaka dinner jioni?
 
Halafu sijui ni shetani au ni nini, juzi tu nmewaza kwa sauti nikajisemea "nipunguze kidogo kula" cha ajabu hiyo jana nmeamka na apetite ya hatari asubuhi nmekula chapati tatu... Shetani ana nguvu kuliko breakdown
Wee achana nao hao watafiti bwana...kuna raha ya kulisogeza tumbo ndio uione mbususu
 
Sawa sawa mkuu.

Swali la nyongeza kidogo mkuu..

Unadhani ni kwa nini bwana mwili anaacha mpaka unene unakuwa mkubwa na kusababisha magonjwa hayo wakati bwana mwili huyo anao uwezo kabisa wa kuepuka unene huo kutokana na akili aliyokuwa nayo bwana mwili huyu ?

Unadhani ni sababu gani inasababisha mwili mpaka anashindwa kucontrol uzito ambao baadae unaenda kusababisha magonjwa hatarishi ?
Jibu ni: sababu za KIUSALAMA. Usalama wa uhai kwa kuhofia usipotezwe mazima.'For survival'

Kama mwili utahakikishiwa kwa kuambiwa kwamba ni salama, hakuna hatari wala shida wala vita ijayo. Ni amani na salama. Basi kamwe hautakusanya akiba hizo za kupitiliza.

Lakini kama mwili utaambiwa ni hatari itakuja hivi punde, muda wowote kuanzia sasa. Basi itakusanya na kuhifadhi kwa ajili ya matumizi ya muda mfupi. Na hili wala sio hasara kamili. Maana shida ikija kweli chakula kitatumika na hali itarudi kawaida. 'Acute stress'

Tatizo sasa, stress za siku hizi ni za uongo. Hofu ni za uongo. Shida na vita hata hazipo lakini bado mtu anajiaminisha kuwa kuna shida. Hakuna njaa lakini bado anatumia maneno yanayoashiria kuna njaa kali. Na anafanya hivyo kwa muendelezo wa muda mrefu. 'Chronic stress'

Mifumo ya mwili, inabaki katika hali ya hatari kwa muda mreefu, inajibebesha mzigo mkubwa (ni dharula). Na inafanya michakato mingi kwa hali ambayo ilipaswa kuwa ya muda mfupi lakini inaendelezwa na wakati kimfumo sio endelevu 'unsustainable'. Na ndio matokeo yake kukongoroka afya.

Mwili umedanganywa na akili. Akili imeupa picha ya hatari na dhiki kuu wakati sio kweli. Hebu watu waichukulie email ya bosi kama email sio kama li kitu la kutisha tena la kufisha ati 'D E A D L I N E' aani ukivuka tu unakufa😧
Na kukosa mikaratasi ya hela mfukoni kusisomeke kama hivi punde ' N I T A K U F A N J A A'
Mwili ukiondolewa hizo hofu na ukahakikishiwa usalama wake, hautaona haja ya kuhifadhi dharula kubwa kupitiliza. Huu ndio msingi wa nadharia.

TLDR: Mwili unahifadhi chakula kwa dharula na kwa sababu za kiusalama. Ilitusaidia enzi tukiishi mapangoni, ingetusaidia hata leo. Tatizo tu ni uongo tunaouaminisha mwili kwamba kuna shida na kumbe kiuhalisia hakuna shida.
 
Halafu sijui ni shetani au ni nini, juzi tu nmewaza kwa sauti nikajisemea "nipunguze kidogo kula" cha ajabu hiyo jana nmeamka na apetite ya hatari asubuhi nmekula chapati tatu... Shetani ana nguvu kuliko breakdown
Shetani hana shida na mwili wa binadamu, ana shida na roho.
 
Back
Top Bottom