Fab,
Usitumie kisingizio cha mama yako kuachika kuwa sababu ni kukeketwa. Wakati baba yako anamuoa mama yako bila shaka alijua kwamba mama kapigwa kiwembe lakini bado tu aliendelea nae hadi ukazaliwa. Kama kuna dada zako nao wana matatizo kwenye ndoa zao bado nasema usisingizie ukeketaji, inawezekana wao wenyewe ndo wameshindwa kuzitunza ndoa zao, na bila shaka hao waume zao walipoanzana nao hadi kufikia kuwaoa walijua kwamba wamepigwa viwembe. Halafu kitu kingine manka, mimi nimekaa moshi miaka 7, ninawafahamu vizuri sana wachaga, kwahiyo huwezi kunidanganya kuhusu sababu za wanawake wa huko kuachika, there are number of issues!!
Ni dhahri kwamba kwa mtu kama mimi kuja hapa kutetea hii mila wengi wetu hawawezi kunielewa, lakini hao wasionielewa ni kwakuwa wanaangalia upande mmoja tu pasipo kutaka kujua na upande wa pili. Ukeketaji hauwezi kumalizika kwa siku moja, ni suala la muda mrefu kidogo. Kwahiyo kinachofanyika ni kuendelea kutoa elimu kadri inavyowezekana, na hiyo imesaidia kuboresha mazingira ya zoezi lenyewe na baadhi ya wasichana kuona hakuna sababu ya kutokeketwa na at the same time wanaume nao kufahamu kwamba hata mwanamke asiyekeketwa bado anafaa na anaweza kuwa mke bora. Kwa maana kwamba inahitajika muda ili wazee wetu wa mila kuona na kutafakari njia mbadala kwa hawa dada zetu kuweza kupatiwa mafunzo haya ya kuwavusha rika, toka utoto na kuingia ujana pasipo kupitia ukeketaji. Kwa kuwa wazee bado wanaamini kwamba ni muhimu kila msichana akapitia huo mtihani na kwa kuzingatia elimu na ushirikiano na wataalamu wa afya ndio sababu ukeketaji wa sasahivi ni kama kiashiria tu, kwakuwa wanakata ile kitu kidogo sana kiasi ambacho haina athari yoyote kwa msichana. Bahati mbaya hii kitu watu wengi tunaijakidili kiushabi zaidi pasipo kujua undani wake na ukweli wake.
Mwisho, Fab bado nakusubiri unithibitishie kwamba hawa wanawake hawafiki kileleni!!:teeth: