50/50 inayotafutwa haina msingi zaidi ya kufahamiana na kujuana

50/50 inayotafutwa haina msingi zaidi ya kufahamiana na kujuana

50/50 yaweza kuwa jambo jema sana ili kuonesha usawa na sie tufanane na dunia.

Nadhani akina mama safari hii wamepata mtetezi wa kweli mwenye mamlaka makubwa ya uteuzi. Either mwenda zake alijaribu kuwa maingizo mapya mawili kwenye mifumo ambao huko nyuma nafasi hizo zilikuwa za wanaume.
VP Samia S. Hassan 2015-2021 (Ambae kwa sasa ndie C in C)
Commissioner Gen. wa Uhamiaji Dr. Anna Makakala.

Nataka kuamini hao wawili niliowataja walifika pale kwa meritocracy na ika-happen pia kuwa ni wanawake.

USA ambao wamepata uhuru na wana idadi kubwa ya wanawake waliosoma ila mpaka sasa ni nchi ya 70 kwa kiwango cha uwakilishi wa akina mama bungeni.


Tunawatakia kila la heri akina mama ambao baadhi yao ni mama zetu, shangazi zetu, dada zetu, wake zetu, wanetu kwenye majukumu ya kuteuliwa na mamlaka kutumikia Watanzania.

Rai yangu kwa mamlaka ya uteuzi ni namna gani akina mama kama ambavyo wanaume au vijana wanatakiwa kuteuliwa washike nafasi by merits na sio kubebwa.
Na kwa muktadha wa sasa asiwe mtu kwa sababu ya CV (educational achievement) ila mtu mwenye uwezo wa ku-push the bounds na kufanya mambo yatokee.

Tanzania inapakana na Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi, Congo, Zambia, Malawi na Mozambique; Baharini tuna nchi kama Comoro, Madagascar, Seychelles na Mauritius.
Tuna muono gani kulifikia hilo soko kwa mahitaji ya msingi kama chai, kahawa, korosho, cocoa, nyama, samaki, maziwa, nguo za kuvaa au vitambaa?

Tumezungukwa na nchi zenye watu wengi sana, nadhani wateule wa Mhe. Rais waje na akili zenye kuleta suluhisho linalowezekana, ni namna gani tukiamua kuuza hata biscuits nchini Comoro toka Tanzania zifike kwa haraka kwa bei nafuu kuliko Dubai?

Juzi nimenunua cornflakes, kuchungulia nikaona made in Libya; yaani linchi looote hili yet tuna import cornflakes?

It high time akina mama, wanaume, vijana wa kike kwa kiume ambao mtateuliwa na mamlaka za uteuzi mje na solutions zenye kuzalisha ajira, kuongeza exports, kuongeza tax base, kupunguza imports.

Kila la kheri tena Mama Samia Suhuhu Hassan Rais wa JMT kwenye kulijenga Taifa na kutekeleza kwa vitendo 50/50.


Wewe ndo mwanaume haswaa! I appreciate you
 
Wapo mbioni kupitisha sheria ya kuwaruhusu kuoa wanaume kwa lazima yaan tuwe km India pia wawe wasemaji wakuu wa familia zao hapo ndipo anguko litawajia na watamuacha mama ktk mataa,mwanamke abaki kuwa mama na mwanaume abaki kuwa baba
Sorry hiyo sheria kwa kukadiria inapitishwa lini? Ije mapema jamani! Tuoe😊😉
 
Ni zamu yao, kama wana vigezo hakuna tatizo.
Kule Bungeni miaka yote bado kuna akina mama wanashindana kutikisa makalio. Hiyo tu inatosha kusema 50/50 ni uzembe wa mawazo kwa mkuu wa nchi tunayetegemea ahimize ufahamu kwa akina mama. Yeye mwenyewe anajua ameupataje urais, leo tunaambiwa kwa vigelegele kwamba atateua wafike idadi. Huko Z'bar alikolelewa na kukulia anaweza akapeleka wazo hilo au anatuharibia Tanganyika yetu?

50/50 tunaipenda ifike, lakini ipitie njia njema ili iwe ya kudumu na iwe ndani ya jamii siyo ianzie ikulu kuja kwa wananchi. Hiyo ni kutuletea marafiki zake wa kike ktk utawala.
 
Msiumie Sana nchi yetu Tanzania ni nzuri Sana.Mwaka 2025 itakuwepo shangwe ambayo haijawi kutokea tangu Uhuru wetu.Mtampata kiongozi ambae ndo ataleta MAENDELEO ya kweli.Hawa wapo tu kuandaa njia ili kiongozi wa kweli aje.Yapo na yatatokea aminini ndugu zangu.
 
Wanapigania 50/50 chakushangaza bado wenyewe kwa wenyewe utakuta wanasemana. Si mnajua wanawake walivyo. Hii 50/50 ina harufu ya kubaguliwa kwa wanaume.
 
Mimi nadhani tutafute suluhisho la hizi nafasi za teuzi badala yake ziwe proffesional opportunities, zitangazwe watu aaply na wafanyiwe interview kulingana na vigezo husika
 
Back
Top Bottom