5G vs Starlink

Tanzania hakuna 5G kuna jina tu la 5G kwenye mitandao ya simu wakidai ni 5G of which haina criteria za kuitwa 5G, wanatumia jina la 5G kufanya biashara tu, of which sio 5G

e.g 5G ya hapa Tz nyingi speeds zake maximum ni 250MBs upload & download, hapo ndio speed iko juu na haiko stable..!! So 5G unayosemea ujue kabisa hakuna hapa
 
This is never true...smartphones haziko designed kupokea signals direct from the satellite. Lazma kuwe na satellite dish na rauter.
 
"Starlink haitokuwa mtandao wa kila mtu" sahihi kabisa. Watakao enjoy nahisi ni wabunge maana najua kwa ulimbukeni wao zitafungwa bunge Zima.
 
Starlink itawanufaisha wa vijijini TU tatizo tunafata mkumbo. Vijijini Kwa vile minara haijafika sana wao wanahuitaji mkubwa wa starling ila sisi wa mijini hatuna shida mbona?
Acha ufara basi
 
Kuhusu bei za bando serikali pia inachangia. Kiufupi Hilo ni swala mtambuka sio watoa huduma wanajiamulia. Hata starlink watapandisha huduma TU usizani hizo figures hapo juu za bei za mabando Yao zitabaki hivyohivyo. Zitapanda mtaanza Tena kutoa milio.
 
Nani kakudanganya, ujue unaweka umuhimu ambao haupo, hivi game online wangapi wanacheza? Video call usidanganye watu, 100ms unaongea video call vizuri sana, webrtc ambayo ipo kwenye browser iliyotengenezwa kwa ajili ya live chat inatumia hadi ping ya 100ms vizuri sana ...
Hata zoom protocol walikuwa wanatumia ni webrtc kwenye app yao ya browser, na ilifanya vizuri sana, na kufika hadi ping ya 500ms..

Ndio maana nakuambia labda anayetumia UDP ndiye atakwama , tena UDP inakwama hata kwenye 30ms, UDP protoc doesnt care kwamba packets zimefika zote au la, lakini kuna protocol za kisasa ambazo zinahakikisha packets zote zinafika, na kama hazijafika inatoa taarifa zinatumwa tena...

Hapo ni suala la protocol inayotumika...

Live video call nani kakudanganya? 100ms kwa live video inatosha vizuri sana... Whatsapp hawatumii udp kwenye video call...

Hata internet decoders sasa hivi hazitumii UDP, acha kujidanganya... uDP sio reliable hata kwa latency nzuri... Itakuwa nzuri labda kwa local network...



Na mwisho tambua latency haiepukiki, nguvu ya kifaa inachangia latency, unapo record lets say instagram live video, tambua kifaa kita process video, au ku convert, then video itatumwa kwemda kwenye cloud, itakuwa processed, halafu itatumwa kwenye kifaa kingine, napo itakuwa processed tena, hapo tayari kuna delay imeongezeka...

Acha kuongopea watu mkuu... Hata whatsapp wanasema 100ms ni fair kabisa kwa live video call, acheni siasa kisa kulinda biashara zenu...
 
Unaweza uka funga Fiber nyumbani na ofisini kwa bei ndogo kushinda Starlink moja.
Starlink hata weekend nikiwa beach niatumia we na fiber yako utawaambia waipeleke hadi beach?

Halafu 10mbps sio speed ndogo kwa upload, hio 10mbps ndio kampuni nyingi wanatoa kama download speed kwa home internet ... Hata hivyo upload speed inafika hadi 25mbps..

Fiber tupa kule..
 
5G zetu ni za mchongo, nchi nyingine unapata 700Mbps, starlink haisogei hapo.
Starlink anapokomesha ni uwezo wa ku move nayo, ukiingia na starlink yako kwenye treni kuelekea Morogoro unaperuzi mwanzo mwisho... Ukipanda meli unaperuzi tu, hata ukiwa porini ni ku surf tu... Kwa speed ya 50Mbps hadi 250Mbps, 250Mbps inatosha sana, hata 4G zenu hazifiki hapo...
 
Starlink ni option nzuri kwa mazingira ambayo hakuna 5G au Fiber.

Naona watu wanaoendesha hotel mbugani huko, au kwenye projects huko vijijini.... Mradi kama wa Bomba la Mafuta itawafaa hii.
 
Kabla ya kuongelea 5G kwanza angalia takeimu za watumiaji wa Internet kwenye bara la Afrika ni asilimia 37 pekee kati watu zaidi ya bilioni 1.3. Unafikiri share ya watanzania wanaotumia Internet ni wat wangapi?

4G yenyewe kwa bara la Afrika imeenea kwa asilimia 64 pekee. Hapa nchini 4G utaikuta kwenye majiji na baadhi ya miji michache, ukitoka kilomita 20 tu unakutana na 3G kushuka chini.
 
Kama unataka data za watumiaji Internet chukua Tcra, data zote za Nje hazina maana kwetu sababu hawajui mifumo yetu. Mfano sisi tunashare ip adress, ip moja mnatumia watu zaidi hata ya 100 kawaida watu wote hao kuwa counted kama mtu mmoja.

According to Tcra watu milioni 39 wanatumia Mobile data, labourforce ya Tanzania ni watu Milioni 31 (miaka 15 hadi 64). So ni asilimia kubwa tu tupo covered.

Halafu tumia tu akili ya kuzaliwa je ni kweli Africa kila watu watatu mmoja tu ndo anatumia internet? Mtaani kwenu watu wenye whatsapp ni wachache kuliko ambao hawana?
 
Data uchwara. Kila robo ya mwaka TCRA Huwa wanatoa takwimu kuhusu ufanisi na udhaifu wa MNOs wetu download pdf uone takwimu tulivyopiga hatua
 
Chief kwenye masuala ya teknolojia naheshimu sana michango yako kwa sababu binafsi sina ufahamu wa kutosha.
Kwa sababu nafuatilia sana masuala ya teknolojia nilikutana na huo utafiti uliofanywa na reputable institution hivyo sina sababu ya kukubeza wala kuubeza huo utafiti uliofanyika kwa kuwa kila utafiti unatumia methodology ambazo zinaweza kutofautiana kati ya taasisi na taasisi.
Otherwise I'm always interested to learn badala ya kubishana.
 
Data uchwara. Kila robo ya mwaka TCRA Huwa wanatoa takwimu kuhusu ufanisi na udhaifu wa MNOs wetu download pdf uone takwimu tulivyopiga hatua
Sina utaalam wa masuala ya teknolojia ingawa napenda kufuatilia kwa kuwa teknolojia inakuwa siku hadi siku.
Kuuita utafiti wa mtaalam kuwa finding zake ni uchwara ni kuukosea utaalam wa aliyefanya huo utafiti. Tujifunze tu kutambua findings za wengine hata kama findings zako unaziona ndio sahihi kuliko za mwenzako.
Hata hivyo subject matter ilikuwa uwepo wa 5G. Watumiaji wa WhatsApp hata 2G unatumia bila shida. Kabla ya kutaka kuboshana unatakiwa kuelewa data na subject matter kabla kuhukumu uchwara wa data zinazotokana na findings za utafiti.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…