Uvumilivu usiokuwa na ukomo ni wehu! Kati ya weakness zenu zinazokera ni kutoa taarifa za uongo kwa mteja na pia kutotoa mrejesho kwa wakati.
Mtu nmetuma maombi yangu,mmeshajua niko eneo gani na mnajua kwa eneo husika miundo mbinu yenu haiwezeshi huduma kupatikana haraka eneo ilo,mpeni taarifa mteja na zisiwe tu taarifa bali taarifa sahihi na za kweli. Mwambieni bhana hapo ulipo kukufikia ni baada ya miezi mitatu.
Ntakupa mfano,last saturday nlikwenda Mlimani City duka la Ttcl,nkamkuta mzee mmoja pale,nkaongea nae akatoa majibu ambayo unaona kabisa huu ni uongo tu. Nkatoka nkaenda duka la Halotel,wakanipa namba ya Technician wao niwasiliane nae,nikampigia simu akanielekeza kwamba kwa urahisi ntumie current location ya eneo unalotaka hiyo huduma. Jioni yake of the same day akanipigia,akanieleza kwamba kwa mtambo wao mahala ulipo na mm nnapotaka huduma ni mbali na hivyo haiwezi kuwa haraka mimi kupata huduma husika. Unaona kabisa level of professionalism,Ttcl sasa😂😂. Jibu la yule jamaa halikuwa zuri kwangu lakini nlifurahi jinsi nlivyopata mrejesho upesi na nlilidhika kabisa