70% ya wagonjwa wa ajali za barabarani waliopo MOI (Muhimbili) chanzo ni bodaboda

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2022
Posts
2,780
Reaction score
6,607
Asilimia 70 ya wagonjwa wanaofikishwa katika Taasisi ya Tiba ya Mifupa Muhimbili (MOI) wanatokana na ajali za barabarani, huku ajali zinazohusisha bodaboda zikiongoza kwa idadi.

Mkurugenzi Mtendaji wa MOI, Dkt Respicious Boniface ametoa takwimu hizo Jijini Dodoma amesema wengi wao wanakfikishwa hospitali wakiwa wameshavunjika mifupa mikubwa, wengine vichwa.

Taasisi yake pia imepokea majeruhi 11 wa ajali ya gari la Shule ya King David Mkoani Mtwara, kati yao watatu wapo katika uangalizi maalum.
 
Bodaboda ni janga jipya kama ilivyokuwa ukimwi miaka Ile ya tisini, serikali inaendelea kupoteza rasilimali kila siku Kwa uzembe wa kuwpa kichwa hawa bodaboda
 
Bodaboda lisingekua janga kama madereva wake wangekua na uelewa walau kuhusu sheria za barabara.
 
Juzi juzi nilikuwa kwenye The Kingdom of Rwanda nimekuta Boda boda wenye nidhamu ya hali ya juu na wenye kufuata sheria zote za Barabarani.

Hapa kwetu sijui ni laana gani inayotutafuna na kuangamiza kizazi hiki.
 
Probox/Succeed aka mchomoko zinapigwa marufuku maeneo mbalimbali kwa hoja dhaifu tu lakini bodaboda takwimu zake zinatisha lakini zinatazamwa kwa jicho la ajira kwa hiyo acha ziendelee kupeta.

Kuna hospital zina wodi zinaitwa Bodaboda!
 
Juzi juzi nilikuwa kwenye The Kingdom of Rwanda nimekuta Boda boda wenye nidhamu ya hali ya juu na wenye kufuata sheria zote za Barabarani.

Hapa kwetu sijui ni laana gani inayotutafuna na kuangamiza kizazi hiki.
Hata hapa bongo wapo bodaboda wanaojielewa. Inabidi umsome vizuri bodaboda ukiwa umepanda pikipiki yake kuanzia mavazi, harufu mpaka uendeshaji.
Mara nyingi sana nashuka kwenye bodaboda kabla sijafika niendako nikiona dreva ni mjinga.
 
Hata hawapimwi Afya kabla ya kupewa leseni ya Pikipiki.

Kuna mmoja huko Mtoni mtongani kamuua Mama wa watu kwasababu alikuwa na kifafa kikamshika akiwa akiwa kampakia Mama huyo

Hili Taifa linahitaji maombi maalum ya kumlaani Nyerere na kumuombea Kambona.
 
Unaharibu uzi makusudi.
 
Bodaboda lisingekua janga kama madereva wake wangekua na uelewa walau kuhusu sheria za barabara.
Sheria ni moja.

Baada ya hapo kuna hatua ya pili hadi kumi naa ishirini hivi kuhusu bodaboda.

Kuna suala la mavazi maalumu ya kinga ukiwa kwenye pikipiki, helment najua tunavaa japo hata nayo ni nusu wateja bado hawavai...... jaketi la pikipiki [sio la fashion] nazungumzia yale ya kina alpinestasr etc na viatu maalumu asee mi naona tuwekeze kwenye mavazi pia [motorcycle gear] itapunguza sana nahisi.

Mungu hana upendeleo na sheria ni msumeno.

Kwa uzi uleule mfano nipo natafuta viatu kama hii napata wapi mazee na shngapi?
Boot2.jpg
 
Attachments

  • Buti3.jpg
    Buti3.jpg
    26.5 KB · Views: 6
Presicely boda ni janga, Kuna kampeni ifanyike kuwaelemisha kundi hili.
 
K
Hata hapa bongo wapo bodaboda wanaojielewa. Inabidi umsome vizuri bodaboda ukiwa umepanda pikipiki yake kuanzia mavazi, harufu mpaka uendeshaji.
Mara nyingi sana nashuka kwenye bodaboda kabla sijafika niendako nikiona dreva ni mjinga.
Kuna siku utashukia Kuzimu
 
Sheria ni moja.

Baada ya hapo kuna hatua ya pili hadi kumi naa ishirini hivi kuhusu bodaboda.

Kuna suala la mavazi maalumu ya kinga ukiwa kwenye pikipiki, helment najua tunavaa japo hata nayo ni nusu wateja bado hawavai...... jaketi la pikipiki [sio la fashion] nazungumzia yale ya kina alpinestasr etc na viatu maalumu asee mi naona tuwekeze kwenye mavazi pia [motorcycle gear] itapunguza sana nahisi.

Mungu hana upendeleo na sheria ni msumeno.

Kwa uzi uleule mfano nipo natafuta viatu kama hii napata wapi mazee na shngapi?
View attachment 2307309
Haya madude nawaonaga wale wazungu(watalii) wanayavaa wakiwa wanaendesha pikipiki hapa kwetu.

Bodaboda wetu hawa hata peku fresh tuu .
 
Hawo boda watakua Salaama, endapo watumiaji wengine Barabara wataheshimu haki za wengine na kua wa vumilivu.
 
Back
Top Bottom