Hivi kweli unafikiri kuna kidume kwenye njaa? Utawezaje kuificha na mitandao hii iliyojaa? Kuna msanii aliimba "adui muombee njaa, atanyosha mikono juu hata kama alikuwa shujaa" njaa haifichiki kabisa.
Najua unaijua Tz, kwa Tz eneo hatari kama litakumbwa na njaa ni kanda ya ziwa tu, kwakuwa wanategemea mazao ya msimu na ya muda mfupi. Mazao ya nafaka, na tatizo kubwa zaidi ni familia kubwa, hawa jamaa wanajua kufyatua watoto sana. Bahati nzuri yao wana mifugo na ni ma had worker kwelikweli.
Taarifa, kwa sasa kanda ya ziwa ni msimu wa mavuno. Na mwaka huu wamevuna nafaka nyingi kupita misimu iliyopita. Mvua zinaendelea, hivyo wanapanda tena mle walikovuna. Kubwa zaidi, mwaka huu zao lao la kibiashara "pamba" litavunwa kwa kiwango kikubwa kiasi tunaanza kuhofu soko.
Hakuna njaa Tanzania, hao watafiti warudie tena. Mikoa mingine hata siiongelei, huwa njaa wanaisoma ktk vitabu vya historia. Lindi na Mtwara korosho imewapa kiburi mwaka huu.