80% ya wazee wetu walishindwa kujitafuta na kujipata

Ukweli ndio huu.pia kuna muhubiri mmoja alisema ukweli ni kwamba inatakiwa mzazi uweke akiba kwa ajili ya watoto wako. Maana biblia inasema mtoto anarithi nyumba na mali kutoka kwa baba yake...how come mtoto ndio anaanza kumjengea mzazi nyumba? Means kuna mahali mzazi hakutimiza wajibu wake.
 
Na wewe Jenga wanao waje warithi, acha kulalamikia!
 
Pumbavu kabisa wewe kichwa kikubwa akili huna,mzazi wako anawezaje kuwa mzigo kwako?usipo muhudumia mama alie kunya na baba alie kukojoa utamuhudumia nani?mama mkwe sio[emoji24][emoji24][emoji24]
 
Kumbuka na wewe utazeeka. Wewe endelea kusimanga wazee na kuwaita mizigo, kwenye kutafuta kuna kupata na kukosa huwezi jua walipitia changamoto zipi katika utafutaji wao.
Kweli kabisa nadhani huyu kijana ni mshenzi tu kuwakosea adabu wazazi ni laana kaisha laniwa tayali
 
Vilabu vya pombe na mijanajike ya vilabuni wangemwachia nani?
 
Wazee wengi licha ya kuzembea ujanani bado wanacheza bao badala ya kufuga hata njiwa.
Wazee wengi wa zamani walikuwa waadilifu makazini.

Kizazi cha sasa 80% sio waadilifu na wapigaji,,
Tusiwalaumu wazee wetu kwa kushindwa kufika malengo.

Kila mtu ana ndoto zake ktk maisha,,,kufanikiwa wewe sio ufikirie walioshindwa ni wazembe au wajinga.
 
Uongo
 
Acha Kulalamika Saidia Wazazi Wako Upate Baraka
 
Kumbuka na wewe utazeeka. Wewe endelea kusimanga wazee na kuwaita mizigo, kwenye kutafuta kuna kupata na kukosa huwezi jua walipitia changamoto zipi katika utafutaji wao.
Uko Sahihi,Kweli Kuna Wazee walipambana lkn hawakufanikiwa hao wapo,lkn kuna Wale ambao walichezea muda wao Yaani hawakufanya chochote Kazi kushindana kumiliki mademu,kushindana Kunywa bia Nyingi,kujua wanamuziki mbalimbali nyakati zao,kucheza kamali,nk.Kiufupi hawakujua kuwa Kila Jambo lina Wakati wake,na Wakati ni ukuta.Waulize uone,baadhi yao huwa wanakili kuwa walichezea fursa.

Sent from my V1901A using JamiiForums mobile app
 
Upo sahihi,Mfano Watumishi hawakuwa na mikopo ya benki enzi hizo.Ila tukubali Kuna Wazee waliwahi kupata fursa nzuri tu lkn walizichezea.

Sent from my V1901A using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…