85% ya Wezi / Matapeli wa Mitandaoni ( Tuma kwa Namba hii ) wanatokea / wako Ifakara Mkoani Morogoro

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Joined
Jul 13, 2013
Posts
60,660
Reaction score
121,325
"Huwa wanakaa katika Nyumba Moja huku Wake zao wakiwa busy kuwapelekea Vyakula. Na baadhi yao ni Wasomi wakubwa sana tu hadi wana Doctorates ( PhD ) zao"

Nukuu hii nimeitoa EFM Radio Asubuhi hii baada ya kumsikia Bwana Innocent Mungi Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano Wizara ya Habari na Teknolojia akitiririka na kuserereka zake kama Mtaalam na Mngwena ( Mjuzi ) wa Mambo haya TEHAMA ( ICT ) katika Kipindi cha Joto la Asubuhi.

Wana Ifakara Morogoro Shikamooni.
 
Mji wa ifakara matepeli niwengi mpk Wazee wenyenyewe wanajiitawanaeenda lupigakodi
 
Ukute kuna wapopo huko wanashirikiana na wazawa,,,hawa jamaa siku hizi wanajifunza sana kiswahili
 
Kama wanajulikana hadi na nyumba wanayokaa kwa nini TCRA, polisi na wahusika wengine wasifanye ambush ili kuwakamata na kuwafikisha mbele ya sheria?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…