Lunyungu
JF-Expert Member
- Aug 7, 2006
- 8,873
- 1,906
Mkutano wa Sullivan: Rais Kikwete apongeza Vodacom Tanzania
Na Mwandishi Wetu, Arusha
�
RAIS Jakaya Kikwete ameipongeza Kampuni ya Simu za Mkononi ya Vodacom Tanzania, kwa ushiriki wake mzuri katika mkutano wa Leon Sullivan unaomalizika leo jijini hapa.
�
''Ninawapongeza Vodacom Tanzania kwa ushiriki wao katika mkutano huu,'' alisema Rais Kikwete.
�
Alisema ushiriki wa sekta binafsi katika mkutano huo ni wenye manufaa na mchango mkubwa na kwamba, sekta hiyo ina nafasi kubwa kwenye ukuaji wa uchumi wa nchi.
�
Naye Hope Masters, Mtendaji Mkuu na Rais wa Taasisi ya Sullivan, aliipongeza Vodacom jinsi ilivyoshiriki na kwamba, ni mmoja wa wadau waliochangia mafanikio ya mkutano huo.
�
�Kwa namna ya pekee naipongeza Vodacom Tanzania kwa ushiriki wake wa karibu, ambao umeweza kufanikisha mkutano huu,� alisema Masters.
�
Vodacom Tanzania, ni mtandao rasmi wa mawasiliano katika mkutano huo ambao ulifunguliwa juzi usiku na Rais Kikwete. Pia, imetengeneza kituo maalum cha mawasiliano kinachotumiwa na Waandishi wa Habari kutoka sehemu mbalimbali za dunia wakiripoti matukio ya mkutano huo.
�
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania, Dietlof Mare alisema, Vodacom Tanzania inajisikia faraja kufanya biashara zake Tanzania, kutokana na sababu mbalimbali, zikiwemo amani, utulivu na ukuaji endelevu wa uchumi.
�
Mare alisema, mazingira hayo na sera nzuri za serikali, zimewezesha kampuni hiyo kuwekeza na hatimaye kukua mwaka hadi mwaka na kuwa mtandao unaoongoza.
� �
Alisema kwa kutambua Tanzania ni nchi inayoendelea na inayokabiliwa na changamoto katika ukuaji wa sekta mbalimbali, Vodacom Tanzania imekuwa ikiwekeza kuhakikisha maendeleo ya watu yanapatikana.
�
Alisema idadi ya wateja hai wa Vodacom Tanzania, wamekuwa wakiongezeka kila mwaka, hivi sasa Vodacom ina zaidi ya wateja �milioni nne, huku ikitoa ajira za moja kwa moja na zile ambazo sio za moja kwa moja kwa zaidi ya Watanzania 50,000.