8th Sullivan Summit Arusha Tanzania

8th Sullivan Summit Arusha Tanzania

FMES,
Good question. Maana hivi sasa AY ana cheo kikubwa tu katika hiyo asasi. Na anajaribu kuiunganisha pamoja na kampuni yake ya GWI, which I think is wrong. Malengo ya Sullivan yalikuwa ni fair trade na kuhakikisha mashirika makubwa ya Kimarekani yanafuata sheria za Marekani hata katika nchi za nje kama iivyokuwa na Afrika kusini ambako kulikuwa hakuna vyama vya kutetea wafanyikazi wakati wa ubaguzi wa rangi. Hii ilisaidia sana kuwapa Waafrika fair treatment kwenye kampuni za Kimarekani na wakaanza kupandishwa vyeo na kupewa training. Baadaye kampuni za Makaburu nazo zikaona they have nothing to lose by giving fair treatment to the Africans. Ilisaidia kuleta mageuzi ndani ya Afrika kusini ambayo kwa vyovyote vile yangehitaji mtutu wa bunduki kuyafikia.
 
JF ni noma,
Sasa Mbona muungwana hatumii ubin wake wa pdh katika CV yake?au anona soo?
Rais wa Nne wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amri jeshi Mkuu Dr. Jakaya Kikwete..Je inaleta Maana?
Ay ni soo,Hata dili la utafiti wa Mafuta unaofanyika Lindi naye anahusika..
Kuna Jambo linakuja
 
Wanabodi,
Mtanisamehe maanake maswali yamekuwa mengi nashindwa hata kufuatilia ila nitakachosema ni kwamba yote mlozungumza yanazidi kupotosha umma.
nashindwa kuelewa kama anayetakiwa kulaumiwa ni JK ama AY kwa sababu kama JK ni fisadi na huyo fisadi mnamjengea ngome asikutane na AY fisadi mwingine hapa nashindwa kuelewa. na kifupi sijawahi kuona dunia ya leo mfanya biashara ambaye ataweza kuionea huruma Afrika kama sio sisi wenyewe na hasa tukipata kifua cha Sullivan.

Pili, Susuviri ameshindwa kabisa kutenganisha maelezo yangu kuhusu AY akiwa co founder wa GWI na kazi zake halafu kama mwenyekiti wa Sullivan foundation kiasi kwamba unataka tuamini kuwa AY ndiye mwamuzi wa dira ya Sullivan foundation na GWI yaani hawa ni kitu kimoja ama Sullivan imevumbuliwa na AY kama vile Foundation zakina Bill gates na Clinton.......Susuviri, unapokazania kuwa malengo ya AY ni fedha una maana gani haswa?... maanake madai kama haya naweza sema kuwa JK, kuwa rais kasukumwa na fedha kwanza, hali nachofahamu mimi JK ilikuwa ni ambition yake - ile ndoto ya kukalia kiti cha Urais. Zaidi ya hapo pia naweza sema sisi sote wafanyakazi tunasukumwa na fedha kufanya kazi na sio wajibu wetu kufanya kazi. Ubishi kama huu hauwezi kuwa na suluhu kwani hkuna kati yetu nyeweza kufanya kazi bure.
Pili, niliseme kuwa hiyo summit ya Arusha itaweza kutuletea fedha badala ya kuandaliwa nje ambako kila siku cost zake huwa ni kubwa zaidi. Yatakayofuatia baada ya mkutano huo siyafahamu ila nachojua kutakuwepo na deal nzuri zenye malengo mazuri maadam sisi tuwe na msimamo wetu ktk mikataba hii. ulichojaribu kubadilisha hapa ni kuchanganya mazuri ya wakati wa mkutano huo na yale yatakayofuata baada yaa.
Kisha labda hufahamu jinsi watu wanavyofanya kazi zao dunia hii ya mtandao...mjomba unaweza kumkuta Bill Gates ktk makampuni zaidi ya matano na uhusiano wake ukakupa taabu kuelewa. hadi hapa sijaona kitu kinachoweza kunipa hofu na hata hiyo GWI ikiwa hawa ni consultant firm tu, uamuzi wa mwisho unao wewe mwenyewe.
Jasusi,
.....
Mkandara, nadhani umepitiwa kidogo ndugu yangu nilijibu issue kuhusu Sullivan na GWI.
1. Nimeitofautisha vyema tu kwenye thread yangu iliyotangulia nikaeleza wazi kwamba BEFORE Sullivan ilikuwa namalengo mazuri, lakini sasa mambo yanakwenda tofauti kwa sababu AY kashika hatamu. Je unakubali hilo au la?

2.Kuhusu fedha: Mimi ninachosema ni kuwa kama money is motivating you then say so openly, siyo kutuletea mizengewe kuhusu democracy na poverty eradication awards! Mimi ninachopinga ni kuchanganya those lofty goals wakati ukweli ni kwamba AY anafanya kazi ya kutumwa.
Je hilo limekuwa clear?

3. Malengo ya Sullivan - Umesema nimechanganya mazuri ya Sullivan Summit na yatakayofuata, sasa nitayatenganisha vipi? Hebu tufafanulie kwa point - malengo ya Sullivan summit ni nini? Si kuleta wawekezaji, kwani hao wawekezaji watakuja na kuondoka mara baada ya mkutano? If so tutafaidika nini - kuuza tourist art - afew makonde carvings and paintings? Kama wawekezaji wanakuja kuwekeza basi hiyo si ndiyo kitakacho FUATA baada ya mkutano? I think huwezi kuongelea mazuri ya mkutano bila kuongea kuhusu consequence na aftermath ya mkutano. Tafadhali nisaidie kutofautisha mwenzako, labda sijaelewa!

4. Sifahamu jinsi watu wanavyofanya kazi zao duniani. Hoho! This is funny! Laiti ungejua mambo ninayoyafahamu! But anyway, naomba niku-reassure, najua mambo yanavyofanya kazi lakini anachofanya AY na wenzake siyo sawa! Una uhakika issue hii ikipelekwa New York Times au Washington Post italala? No! Kwa nini? Kwa sababu GWI kama consultants are making a killing at the expense of Africans and that was the story in New York Times, hii ya Tanzania itakuwa even better! Just wait and see! Hiyo networking unayozungumzia is acceptable but not the way they do it. There's no reason sisi kuwatetemekea hiyo Old Boys Club inayotunyonya for centuries alafu sasa tunachobabikia eti kwa kuwa AY is Black!

Kuhusu Sullivan Summit - naomba unieleza Tanzania itafaidika vipi? Not in vague terms eti investment, NO! What type of investment? Why this summit is so important kiasi kwamba JK hakuwenda EU kutafuta huko mikataba ya ushirikiano na nchi za EU na kutufungulia masoko, bali kakimbilia award yake? I mean, tusiipe hiki kitu umuhimu mkubwa maana kama ingekuwa na manufaa hivyo how come NIgeria iliyo host for 2 occassions consecutively hawataki kuihost tena? Je wamefaidika na nini? Naomba uniletee facts, Mkandara, alafu tunaweza kuendelea, maana mimi nimeweka hapa facts nyingi!
 
Ok, naomba mi niendelee na kazi ya utafiti. Nimetayarisha diagram moja ambapo nimeonyesha jinsi AY, pamoja na his pals - Jeter na Masters wanavyotumia mtandao wao.
Wanachanganya masuala ya charity na foundation with activities za economic hitman!
Kama admin anaweza kutusaidia kubandika hii picha in the forum nitashukuru.
Baadaye kidogo nitaleta diagram nyingine itakayoonyesha ni jinsi gani hata board members wa Sullivan wana uhusiano na GWI na clients wao!
 

Attachments

  • ConnectingDots1.jpg
    ConnectingDots1.jpg
    145.3 KB · Views: 40
Hivi yule congresman Jefferson anayefanya dili na Afrika ambaye alibambwa na FBI hayuko na hawa jamaa?
 
Haya kuna diagram nyingine ambapo nimeongeza other institutions na also nimeona mtu mwingine ambaye amejitokeza naye ni Bill Clinton.
SAED ni mfuko ulioanzishwa na Clinton na akampa AY ulaji. Bill Clinton pia ni board member was Sullivan. Also Hillary Clinton amepata tuzo ya Sullivan.
Africa America Institute ilimpa recently JK zawadi about development na education. Some commentary nimesoma imesema AAI ni front organization ya CIA but it is not substantiated.
Jamani bado naendelea kujichimbia kwenye data. Any other useful information naomba nitumiwe hata kwenye PM.
 

Attachments

  • ConnectingDots2.jpg
    ConnectingDots2.jpg
    138.3 KB · Views: 29
Hivi yule congresman Jefferson anayefanya dili na Afrika ambaye alibambwa na FBI hayuko na hawa jamaa?

Kama una full name yake utanirahisishia kazi yangu. Also alitimuliwa mwaka gani from congress.
Thanks for the info!
 
Mkandara,

Mkapa alikuwa mgumu kutoa ovyo bila kula kisawasawa. Sasa Muungwana ni sawa na wale wagawaji ambao ukimsifia ana meno mazuri tayari anafungulia boma!
 
Kama una full name yake utanirahisishia kazi yangu. Also alitimuliwa mwaka gani from congress.
Thanks for the info!
Bado yupo kwenye Congress na alikuwa ni mnene katika mambo ya African Affairs. Alibambwa na laki moja kwenye friji kwenye sting operation ya FBI. Ni wa Louisiana kama sikosei na kafanya biashara sana Nigeria!
 
Kishoka,
Congressman Jefferson was a lone ranger. Yeye alishirikiana zaidi na VP wa Nigeria, Atiku something.
 

Nimejaribu kufanya utafiti wa haraka lakini sijaona link ya AY na Jefferson, hata hivyo bado ndo kwaaanza naanza. However Atiku na Obasanjo ni paka na mbwa! So ukiwa kwenye kambi moja huwezi kuwa kambi nyingine.
Lakini wenzetu wa Nigeria wako makini, maana wanaandika kila kitu bila kuogopa! Ngoja nirudi nikajichimbie tena!
 
Nimejaribu kufanya utafiti wa haraka lakini sijaona link ya AY na Jefferson, hata hivyo bado ndo kwaaanza naanza. However Atiku na Obasanjo ni paka na mbwa! So ukiwa kwenye kambi moja huwezi kuwa kambi nyingine.
Lakini wenzetu wa Nigeria wako makini, maana wanaandika kila kitu bila kuogopa! Ngoja nirudi nikajichimbie tena!

Nami sijaona link ya Congressman huyu na TZ. Ila nilichoona kwa haraka haraka ni kuwa huyu Bw. alitumia nafasi yake katika Congress kujitafutia deals na tenda Africa haswa Botswana na Nigeria.
 
Duh! hapa ndipo napochoka na Wabongo..
Damn, ndio maana Wakenya wamechukua mlima Kiimanjaro, sisi tumebaki kulaumu tuuu hata kama hatufahamu nini malengo ama minutes za mkutano mzima. Yaani huu mkutano tu umeyazua yote haya na kama hayupo Bush ama kiongozi mweupe anayejulikana basi hili ni deal la walaji!...wakati tumesha liwa sana na wa South, Waarabu wakaingia Wagiriki na Wataliani, waingereza na mwisho Wa - Canada wotenao wanatumaliza bado tu wasiwasi wetu mkubwa ni mtu mweusi mwenzake..Ni tabia ambayo imefanya Watanzania tuogopane hata huko nchi za nje hatuna ushirikiano kabisa zaidi ya upishi wa majungu...
Ukitazama saana hii ni tamaduni yetu Wabongo kuwa ni bora apate mtu wa nje (hasa mzungu ama mweupe) lakini sio rafiki ama ndugu yako!..Na atakayepata ni zake binafsi hazina ubia na mtu.
Kutokana na hali kama hii kamwe hatuwezi kuendelea kwani huu sio ujanja hata kidogo ila ni kuwa insecure na maradhi yanayotokana na inferiority complex. Mara nyingi ni vigumu kwetu ku question utajiri, elimu ama uwezo wa Mhindi, mzungu ama mwarabu lakini inapofikia kuwa ni mmatumbi mwenzetu.... Loooh! hata kamati za ufundi zitatembelewa...

Mkandara kwa hiyo ni bora kuibiwa na Mmarekani mweusi (au muungwana) kuliko kuibiwa na mzungu, right?

Is that the implication of your post?
 
Mkandara,

Sasa hivi hapendwi mtu! Awe Mmanga, Mbulushi, Mchina, Mthailnd, Mzungu au Mnugu!

Tatizo si nia ya AY au Sullivan ambao wote ni lobbyist walioko ule mtaa maarufu pale DC K Street. Tatizo ni what does Tanzania get or benefit out of this?

Ukiangalia picha ya Karamagi, Mahiga, Young (board Member wa Barrick) na huyo mtasha (is is Sinclair?) ambayo ilipigwa mwaka jana, halafu February ya 2007 Karamagi anaingia mkataba wa miaka 50 ambao mnufaikaji wa 99% ni Barrick na si Tanzania, then you have to be suspicious of everything that is happening at current state of Tanzania.

Kasungura ana jeshi lake la kula na kukwapua bila huruma (IPTL, TDC, DAWASCO) na Muungwana ni Mtwana wa Sinclair, Barrick, Tudor kupitia Karamagi.

Kama Pundit alivyosema awali, Muungwana si lazima awe na meno makali kama Kasungurabali yeye ni facilitator mkubwa kwa cheo chake (ama kwa kujua au bila kujua).

Sasa ukisoma maneno ya Cynthia Mckinney, itabidi ujiulize, Bulyanhulu walizikwa watu wakati Muungwana alikuwa waziri wa madini. Sinclair altamka hadharani 2004 kuwa Rais ajaye wa TZ ni rafiki yake wa Takriban miaka 17 (Sutton ilishaingia Tanzania at that time na waziri wa madini aliyeshughulikia Sutton ni Muungwana), Karamagi kasaini mkataba 2007 halafu 2008 Kongamano laja kutaliii Arusha na watakaa kwenye hoteli yao Mount Meru, jee ni faida gani Mtanzania anapata? is this the win win situation?

Jee Kamati ya Bomani wanaweza kufanya kazi yao kwa makini kuhusu mambo ya madini ikiwa principle mkuu wa yote haya anapewa sifa na Board Members wa Barrick?

On the other hand, kama wao (Sullivan, GoodWorks) ni lobbyist, na mshikaji Richard anafanya kazi nao, ni vipi walituachia tukazama mkenge na RDC, Buzwagi au hili skendo la ATC?

Rev.

Just from the conflict of interest issues hapo ilibidi muungwana aji-distance na kina Sullivan/AY/Barrick.

It is one thing to promote investment and quite another to be publicly "in bed" with them.Sasa hata hizi circus like efforts za ku-overhaul sekta ya madini zitaweza kuzaa matunda kweli? Kina Bomani wanapata message gani kuhusu Barrick wanapomuona muungwana ana-dance nao kama hivi, objectivity katika kupitia masuala ya Barrick itakuwepo kweli?

I have identified central points in the exchange involving Mkandara.

Mkandara is pointing out the "Social Darwinism" factor, that in the current investment worldstage, mafisadi and economic hitmen are to be expected and we should not blame them as it is their jobs.If at all it is true that AY and his network are corrupt (which is questionable to him) then we should blame our leaders for exposing us to them.I agree with some of this but also want to go further and point out that mafisadi wapigwe vita popote.Tumeshamsema muungwana sana, na sasa inaonekana kama muungwana na AY wanaunganisha teams.Kwa hiyo kwa sababu AY kaingia kwenye anga zetu naye ni fair game kumchambua na kumsimamisha.

The point about AY being better than wazungu, if that is what was meant, is total hogwash.Kwanza tukae tukijua AY ni figurehead ya network ya watu kibao wa "old boy network" kina Bush, Clinton, Sinclair,Mulroney, Kashogi etc.Kwa hiyo hii theory ya mtu mweusi ni shallow.Halafu pia hata kama angekuwa kweli anatoka the new black panther movement, ufisadi against Tanzania ni ufisadi tu, hata kama ni wa Che Nkapa na Yona, kwa hiyo tutaupiga vita.

Huwezi kuwa against double standard ya watanzania kuwa scrutinize sana weusi (which is not even the case) halafu ukaleta double standard nyingine ya kum-favor AY kwa sababu yeye ni mweusi (strictly speaking he is not even representing black people's interests)
 
Kila nchi ya Africa yenye utajiri wa maliasili na hasa madini, imekuwa haina amani.Kumekuwapo na vita ya wenyewe kwa wenyewe; angalia DRC (Zaire), Angola, Afrika Kusini,nk. Katika nchi zote hizi viongozi wake wawe weusi au wazungu walisifiwa sana na Marekani si kwa uongozi wao mzuri bali kwa kuwa waliruhusu maliasili hizo kuchotwa na wamerekani kwa maslahi binafsi. Kumbuka marehemu Mobutu; kila wakati marekani ilimsifia sana, kumbe ni janja ya kuwafunika wazaire wasione wizi uliokuwa ukifanyika.
Sasa Tanzania tunafaywa vivyo hivyo. Rais anaitwa na kusifiwa ili nasi huku nyumbani tubweteke kuwa anafanya vizuri! Si mmesikia kuna kampuni moja ya kimarekani inataka kuja kujiingiza kwenye masuala ya dhahabu Tanzania? Si mnajua kuwa huyo bwana Young ni shareholder wa Barrick?. Tunasubiri nini sasa?
Kamati ya madini ilete mapendekezo kuwa hakuna kuruhusu shughuli yoyote mpya inayohusu madini yetu hadi (1)sheria irekebishwe,(2)Watanzania turidhike kuwa shughuli za madini zilizopo hivi sasa zina manufaa na si ghiliba (3) Tuwe na wazalendo wetu wenyewe wenye uwezo na utaalamu wa kusimamia shughuli za madini (4)Watanzania tudhaminiwe mikopo na serikali ili tuweze kuchimba madini sisi wenyewe. Tuanze kidogokidogo hatimae tutakuwa magiant kama wao; 'kila mtoto huanza kwa kutambaa'
 
Mimi naomba kuunga mkono aliyoyaandika JASUSI na KAMAKABUZI!
Sisi watanzania ni lazima tuweke upole wetu pembeni. Na maneno kuhusu eti hawa mabepari kutuibia is 'fair play' siwezi kukubali especially in this context, Just to show you all what tyoe of people we are dealing with, hebu cheki 'besti' wake AY - Masters alivyowaibia waNIgeria kwa kutumia rais wao - hapa Bongo ni AY kwa kumtumia Muungwana. Lakini cheki wenzetu waNigeria walivyokuwa makini!
Nigerians abroad are questioning the appointment of a non-African born and controversial confidant of President Olusegun Obasanjo, Mr. Carlton Masters as ECOWAS Special Envoy for African Diasporan Relations.A statement released in Washington D.C earlier in the week by Masters' Goodworks International-which he co-founded with Andrew Young, a former US Diplomat to the UN announced that ECOWAS has named Masters to the position, the first of such an appointment by the regional organisation.
Masters, whose marriage was reportedly sponsored by President Obasanjo and held in Abuja, is known as the main international arrowhead of the controversial launching of the Obasanjo presidential library, an issue that continues to generate ripples raising ethical questions.One of such questions is whether a sitting president ought to embark on such private venture fundraising which some allege include a subtle arms-twisting of holders/managers of state resources, private persons and companies-both local and international. Masters' role is central in the international effort to get multinationals to donate to the Obasanjo presidential library, and he has owned up to this publicly.
Besides the Goodworks International, is known to be a registered lobbyist for Nigerian government here in the US, and Young has publicly attested to the fact that President Obasanjo is the main reason why Goodworks International has not gone belly-up.
Hapa Mkandara, sijui utasemaje? Unaona ni vitu gani ambavyo hawa watu wanafanya? Maana Masters na AY na Jeter wote ni Sullivan na walipeleka summit kwanza kwa same pretext like sasa hivi Bongo (from Abuja to Arusha! au siyo?)
na ndivyo walivyopenya into Nigeria na hivi ndivyo watakavyopenya Bongo!
 
Naomba kuendelea kuonyesha jinsi AY na marafiki zake walivyoitumia Sullivan kujitajirisha kupitia Goodworks Int.

As in the days of military dictatorship, the federal government of Nigeria is still actively in the business of retaining foreign lobbyists in the United States paying them hefty sums of money even though Nigerian embassies are abroad are often cash-strapped and financially insolvent, Empowered Newswire reports.

Leading the pack among the lobbyists the federal government continue to retain in the US, is Ambassador Andrew Young's GoodWorks International, which is said to have made millions from Nigeria as a lobbyist since President Olusegun Obasanjo's first term in office. GoodWorks has been retained since 2001 and continues to be retained by the government to date.
In one instance in 2004, the Obasanjo administration paid the firm where Andrew Young is Chairman about half a million dollars to talk to Nigerians abroad to do business in Nigeria. At the same period, the firm was retained by Nigeria to counter proposed sanctions against Nigeria because of the asylum offered to former Liberian president Charles Taylor.

Na Sullivan Summit ilifanyika Nigeria mara 2 mwaka 2003 na 2006

The Summit is presently involved in discussions to launch a major HIV/AIDS education and containment program that will benefit millions of children over the next five years. The announcement of this initiative took place at the Sullivan Summit VI in July 2003. It was also at this last Summit that Reverend Sullivan announced the Global Sullivan Principles. The Global Sullivan Principles are an update of the apartheid-busting principles that were applied to South Africa and were devised to ensure fair hiring and business practices by international corporations throughout the world.

Summit VI in Abuja, Nigeria, attracted unprecedented high-level political attention and the largest sum donations since the Summit movement began. Summit VI was attended by President George W. Bush (the first presidential visit to Africa), Secretary of State Colin Powell, and National Security Adviser Dr. Condoleezza Rice. ......
In one of its most defining moments of 2006, the Foundation convened Sullivan Summit VII (SSVII) in Abuja, Nigeria, July 17-20, 2006, where it engaged over 2000 business leaders, academics, ten Heads of State, 45 official delegations from Africa, the U.S. and Europe, and other NGO representatives.

Sasa hapa mimi naona hamna haja ya kukataa kitu. Hawa watu ni hatari, hiyo summit is just a front for them kujinufaisha. SPonsor mojawapo wa summit kwa mfano ni Coca cola, sasa hiyo kampuni iko tayari hapa itawekeza tena? Sponsor mwingine Shell , Exxon na Chevron. Haya tuone... lakini mimi ningefurahi ningejua how much retainer fees is Tanzania paying GWI for organizing the SUmmit, and how much organization fees do we pay to Sullivan foundation to have the summit here?
 
Naomba wenzetu mlioko Marekani msishangae kama mliattend hiyo Sullivan dinner na kama mlijiandikisha - kwamba mtatafutwa na GoodWorks International eti kukutana na rais wenu. And AY will pocket his retainer fees. Kumbe Mungwana angetaka angeonana nanyi bila AY but what does he know?
Mwafrika wa kike, labda ungewasiliana na Ay na GWI wao wangeweza kukusaidia uonane na rais wako😀
 
Yanibidi kutua kalamu yangu na kuyaacha yote kama yalivyo isipokuwa wakati utazungumza zaidi kwani hakuna haja ya kuendelea kulumbana kama wafungwa gerezani au mabaharia wa nchi kavu....
Nina imani kubwa na Sullivan foundation,na kwamba AY ni mwenyekiti tu wa foundation iyo kama alivyo Freeman na Chadema.
Nina imani kubwa na Waamerica weusi kuliko Wazungu kama nilivyo na imani na Chadema kuliko CCM, Hata kama kuna watu wanamwekea mashaka Freeman Mbowe.

Na ikiwa kuna mtu ataweza kuniuliza leo hii, Chadema watatuletea nini? itakuwa vigumu kwangu kufahamu kwani sina utume isipokuwa nitakacho uliza ni kwamba CCM imetuletea nini?...sasa kuna faida gani kubaki na CCM ambayo imeshakuwa maradhi yanayokuondoa afya yako kiuchumi kila siku! - hii nikiwataja hao wazungu, wahindi, mafisadi wa ndani na EU ambao walituletea Richmond, IPTL, Barrick, Citywater,na mengineyo mengi tu.
Nina imani Chadema wasingeyafanya haya hata kidogo kwa sababu nafasi kama hizi hupatikana mara moja.....Na wao wanajua haya hata kama mvuto wa fedha ni mkubwa zaidi. Sullivan foundation ni wabora kuliko IMF ama EU!

Mwisho, we need investors lakini safari hii watakuwa chini ya chombo cha mtu mweusi badala ya IMF, chombo ambacho nina imani nacho na kwamba mwenyekiti AY sii mwamuzi wa mwisho wa Sullivan foundation wala hapangi malengo, hachagui wawekeshaji wala hawezi kutuamlia sisi tutakachotaka na hiyo GWI yake. With all said, bado nina imani naye kuwa ni kiongozi mzuri isipokuwa hapendwi na wengi na pengine ana nuksi kama Salim A. Salim, simply because he served whiteman's office. Sina chuki na wazungu hata kidogo ila nachosema ni kwamba inapofikia biashara, mzungu humtazama mzungu, mhindi humtazama mhindi na Mchina humtazama Mchina kama mshirika. Mtu mweusi ni budi amtazame mtu mweusi na alopewa ajenge imani ya kuwa katunukiwa yeye kwa udugu huo. We have to start from somewhere na hii Summit nadhani ni mahala bora pa kuanzia.

Nimemaliza, tusubiri wakti! - By the way Muungwana atakuwa tena Marekani hivi karibuni kuhudhuriia huo mfuko wenu wa Millenium. Kesha ingia UK kuomba pia fedha za EU.. wale waliotuletea mapanki Mwanza, fedha hazionekani wala maendeleo.
 
Back
Top Bottom