Christopher Cyrilo
Member
- Oct 5, 2015
- 90
- 482
OPERESHENI ENTEBE/OPERESHENI THUNDERBOLT
Tukio moja la dharura ambalo lilitokea mnamo juni 27 1976, wakati Yitzhak Hofi akiwa ndio kwanza amepokea kijiti cha ukurugenzi wa MOSSAD, ilikuwa ni dharura iliyohitaji suluhu kwa ustadi mkubwa, pamoja na bahati. Vijana mchanganyiko wenye asili ya kiarabu na wengine kijerumani waliteka ndege ya shirika la ndege la ufaransa, Air France Airbus 300. Ndege ilianzia Tel Aviv hadi Athens – Ugiriki, ambapo watekaji waliingia wakijifanya abiria wa kawaida kwa ajii ya safari ya kuelekea Paris, Ufaransa. Kwa kuwa safari ilianzia Tel Aviv, abiria wengi kati ya 248 waliokuwamo walikuwa waisrael.
Watekaji walijitambulisha kama mawakala wa ukombozi wa Palestina,(PLO) kisha wakatoa amri kwa rubani kurusha ndege hadi Entebe, Uganda ambapo dikteta jeuri na katili Idd Amin Dada alikuwa akitawala, naye alikubaliana na kitendo hicho na kuwapokea na kuwahifadhi watekaji. Masharti ya watekaji yalikuwa kuachiwa huru kwa wafungwa 40 wa kipalestina waliofungwa katika jela za Israel, pamoja na wafungwa 13 katika nchi zingine.
Abiria wa ki-israeli pamoja na wayahudi na wahudumu wa ndege waliokuwa waisrael, jumla wakiwa zaidi ya 100 walitenganishwa, kisha abiria waliobaki wapatao 148, raia wa nchi zingine waliachiwa huru pamoja na rubani, wakarudishwa Paris, Ufaransa.
Huko Paris, abiria wale wa nchi zingine walipofika walihojia na mawakala wa intelijensia wa Ufaransa na Israel. Wana-intelijensia walijifunza kadiri ilivyowezekana kuhusu watekaji na mahali walipohifadhiwa wayahudi na raia wengine wa Israel.
Wakati huo, Israel tayari ilikuwa na uhusiano wa siri na utawala wa Jomo Kenyatta wa Kenya. Uhusiano huo ulitengenezwa kwa makubaliano na jasusi David Kimche ambaye alitumia mwanya wa urafiki wa Jomo Kenyatta na mkulima wa kizungu mwenye asili ya Scotland, Bruce McKenzie. Mkulima huyo, Bruce Mckenzie alikuwa mzungu pekee kwenye baraza la Kenyatta, huku akitumiwa na shirika la intelijensia la Israel, MOSSAD. David Kimche aliyefanikisha urafiki huo anatajwa pia kutoa msaada kwa waasi waliopindua serikali ya kisultan ya Zanzibar, mnamo Januari 12 1964. Kazi yake ya kuzugia katika misheni zake za barani Afrika ilikuwa ‘kujifanya’ mwandishi wa habari wa kiingereza.
Basi kwa ya urafiki huo, Mossad kwa haraka walifika Kenya na kupatiwa msaada wa ndege ya mtu binfasi wa kenya ambayo waliittumia kupita juu ya anga la Entebe na kuchukua picha za maeneo ya mji huo ili kujua pa kuingilia na pa kutokea.
Wiki moja baadae, julai 4 1976, makomandoo wenye sare za kijeshi wa Israel, kikosi maalumu kilichoitwa sayeret Matkal (Scouting Generals) walitekeleza misheni ya kuwakomboa mateka kwa utulivu, ustadi mkubwa na kasi ya ajabu.
Ndege 2 kubwa za mizigo zilitua uwanjani kisha makomandoo 100 wa kiisrael walishuka wakiwa na magari yenye rangi za jeshi la Uganda kisha kuelekea eneo walipo watekaji. Wakati watekaji wakiduwaa na magari yale wakijua ni asjari wa Uganda, walistukia risasi zikimiminwa mfullulizo. Ndipo majibishano ya risasi yalipoanza huku michezo ya kutafutana na kujificha ikiendelea. Baada ya dakika 90, mateka waliokolewa. Watekaji wote 7 walikufa, askari 45 wa Idd Amin waliuawa na wengi kujeruhiwa. Mateka wanne walipoteza maisha, makomandoo wanne wa Sayeret Matkal walijeruhiwa na mmoja, aliyekuwa kiongozi wa kikosi hiko, Yonathan (Yoni) Netanyau, alifariki kwenye tukio hilo. Ilikuwa ni desturi katika vikundi vyote vya kijeshi na kiintelijensia vya Israel, kwamba kiongozi anakuwa mstari wa mbele katika misheni za hatari, kwanza kwa ajili ya kuwapa nguvu wengine na pia ni namna yao ya kuenzi utamaduni ulio katika simulizi zao za kale. Yonathan Netanyau alikuwa kaka wa Benjamin (Bibi) Netanyau, waziri mkuu wa sasa wa Israel. Waisrael hawakuwahi kuwa na furaha kubwa kuliko usiku ule wakati ndege za kijeshi zikitua kuwarudisha ndugu zao. Wanadamu wengi, marafiki na maadui walitamani kuwa waisrael usiku ule. Dunia iliitamani Israel kwa kukataa matakwa ya watekaji na kuwaokoa raia wake waliokuwa mateka katika ardhi ya mbali.
Sehemu ya Kitabu; Spies Against Armageddon, by Dan Raviv.
Imetafasiriwa na Christopher Cyrilo.