90% ya Car Wash ni wezi

90% ya Car Wash ni wezi

Nilikuwa naosha mwenyewe siku hizi siwezi. Kama unapeleka car wash jitahidi kutoa vitu vya thamani na hela. Pia simamia gari yako usiwaamini waoshaji.
Siku moja nipo car wash kuna magari kadhaa. Vitz ikagoma kuwaka, kulikuwa na Audi pale vijana wa car wash wakataka kuitumia kuboost ile Vitz. Nikawauliza mnaijua vizuri hii gari? Wakabaki wananitolea macho nikawaambia mkipiga shoti hapo hii gari itakuja kubebwa hapa na spare mtaagiza Ujerumani. Wakaacha ile gari.
Ninachotaka kusema hapa wale vijana waosha magari hawathamini chochote pale, kama wewe hujali gari yako na mali zako utalia siku moja kwa kuwaachia gari waoshaji.

Ntaua mtu asee, gari inauma sana ndomana huwa siazimishi mkuu[emoji23]
 
Nilikuwa naosha mwenyewe siku hizi siwezi. Kama unapeleka car wash jitahidi kutoa vitu vya thamani na hela. Pia simamia gari yako usiwaamini waoshaji.
Siku moja nipo car wash kuna magari kadhaa. Vitz ikagoma kuwaka, kulikuwa na Audi pale vijana wa car wash wakataka kuitumia kuboost ile Vitz. Nikawauliza mnaijua vizuri hii gari? Wakabaki wananitolea macho nikawaambia mkipiga shoti hapo hii gari itakuja kubebwa hapa na spare mtaagiza Ujerumani. Wakaacha ile gari.
Ninachotaka kusema hapa wale vijana waosha magari hawathamini chochote pale, kama wewe hujali gari yako na mali zako utalia siku moja kwa kuwaachia gari waoshaji.

Basi nimeghairi nilichotaka kuuliza.

Maana labda walinionea huruma kuniibia mie mwanamke...
 
Nadhani wanatazama watu pia usipende kuosha gari usipojulikana. Naacha gari garage au hata car wash tena naweza acha asubuh nikarudi jion kuchukua saa zingine namuachia kijana anakua nalo na nikija hakuna kilichoibwa wala kupotea. Nikiosha gari ndani huwa sikosi ipad na laptop na vitu vingine na nikiacha hata mia naikuta vile vile.

Kikubwa naishi nao kama ndugu siku naweza pita nikawapa hela na hawajafanya kazi yoyote kwangu na siku naweza kupita nisiwape hela na kazi wakafanya basi naishi nao.
Nikiwapa kazi utasikia dah tupe tu chochote maana wanajua wanaweza taja kikubwa wasipate,wanaweza taja kidogo nikawapa zaidi na wanaweza taka kikubwa nikawapa kidogo.
 
Uzi mahususi kwa wamiliki wa magari... Tafadhali unapozungumzia uzoefu wako wa kwenye "Car wash" use unataja na aina ya gari lako...

Hii itatusaidia watafiti kujua walalamishi wengi ni wamiliki wa magari magari au wa " vi baby walker"

My dia Joanah tafadhali uje hapa uchukue takwimu, uniletee chumbani
 
Sio wote wezi. Hata mimi sijawahi kuibiwa car wash tena naenda car wash very local. Ila siwezi kuacha gari nikaondoka.
Sasa mtu kaibiwa sehemu mbili tu lakini anasema asilimia 90 ni wezi... Pathetic

Cc Kasie mahaba nibabue... lete lile lidabokebin lako nikuoshee
 
Anyway, hao umeshawazoea na wanakujua...lakini bado kuwa nao makini..

Kuna jamaa alikuwa na Subaru forster rangi ya damu ya mzee..akaipekea car wash muda wa asubuhi akawaachia vijana ili aifuate baadae, Vijana waoshaji walikuwa ni wanyaturu, si wakawasha ile gari, kusikiza exhaust imefungwa kibuyu, kinatoa mlio mzuri wa boxer engine..
Wanyaturu wakakanyaga moto, dakika 30 zilikuwa ni nyingi, mwenye gari akawa amekaa mahali akaambiwa mbona kama gari yako imebebwa kwenye break down..?

Jamaa kuchungulia, kweli ni gari lake wanyaturu wameshalipiga chini, bahati walitoka salam, wakadandia coaster, mpaka leo hakuna mtu anayejua walipoelekea..

Jamaa akaanza ugomvi na mweny car wash....sijui walikuja kumalizana vipi..?

Wale vijana si wakuamini hata chembe...
 
Sio wote wezi. Hata mimi sijawahi kuibiwa car wash tena naenda car wash very local. Ila siwezi kuacha gari nikaondoka.

Kuna kipindi nilimisi harufu ya upya wa gari, nikapeleka kijiweni waifumue siti zote na yale makava ya mlangoni na roof kwq ndani na kapeti lote chini, waioshe ikauke harufu ya upya itanadadi...

Hilo zoezi nililifanya kipindi cha kiangazi jua kali...

Saa 12 asubuhi nikaacha gari narudi saa 2 usiku haijakauka nikaambiwa nirudi kwasho jioni, lilikauka baada ya siku 3 ila lilitakataaa. Sikiweza kagua haraka haraka kama kuna kitu kimemiss kwa maana ya kudokolewa.

Ila uaminifu ni dhamana, wachache sana wanayo.
 
Uzi mahususi kwa wamiliki wa magari... Tafadhali unapozungumzia uzoefu wako wa kwenye "Car wash" use unataja na aina ya gari lako...

Hii itatusaidia watafiti kujua walalamishi wengi ni wamiliki wa magari magari au wa " vi baby walker"

My dia Joanah tafadhali uje hapa uchukue takwimu, uniletee chumbani

Babu unapenda kupelekewa chumbani.....!!??

Huchokii ...!!😜😜😜😅
 
Sasa mtu kaibiwa sehemu mbili tu lakini anasema asilimia 90 ni wezi... Pathetic

Cc Kasie mahaba nibabue... lete lile lidabokebin lako nikuoshee

Ntumie breki dauni lije kulivuta dabokibini langu ulioshe vizuuuuuriii litakate.

Halowezi tembea maana klachi na senta bolti zimekatika ......🤪😅😅😜🤣
 
Wakuu ni kara ya pili sasa inanitokea,

Mara ya kwanza nilipeleka gari yangu ikiwa mpya, kwa kuwaamini madogo kwa kuwa ndo car wash pekee iliyopo mtaani, nikaiacha gari nikaifata baada ya masaa 2 na nusu hivi nikaendesha kwenda home, asbh kuwasha inagoma as if battery low, kufungua bonet jamaa wame temper, wamefingua battery yangu mpya wakaweka kimeo, nikawafata wakalipa sikuipata ya awali maana walishauza tayari.

Nikaenda town siku moja, nikaweka gari car wash tena, awamu nikasema nitasimamia show, ila nikapokea simu ya dharura ambapo ilinibidi niende bank kutoa pesa nikafanya chap, kisha nikarud, badae wakakamilisha nikaondoka nilipokuja kukagua baada ya siku mbili, hazard zote zimebebwa na fire extuingsher.

Aiseee pia tank langu maji ya wiper nalo likawa linavuja vibaya sana, kila ukiweka maji yanapitiliza sijui waliifanyaje gari yangu maskini.

Nimekata tamaa kwenda car wash bora nikomae home na wanangu.
Kama una kwako unaosha gari mwenyewe tu! Mie mara ya mwisho nimeosha gari car wash ilikuwa kwa jamaa yangu na sikutoa hata 100!

Huwa siwezi mlipa mtu anioshee gari ikiwa nina mikono na maji na kitambaa kipo!
 
Sio mbaya kuwaungisha vijana wetu pale parking za bar.
 
Back
Top Bottom